Kuanzisha kijikampuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuanzisha kijikampuni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by YeshuaHaMelech, Oct 21, 2010.

 1. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Jamani naomba kujuzwa process, kutoka sifuri mpaka kuanzisha kampuni. Nahitaji kujua legal processes na recommendation zenu. najua tu lazima upitie sehemu kama Brela/TRA et al lakini sijui Full process.

  Ahsanteni saana! :bowl:
   
 2. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Mkuu mimi najua utaratibu wa kuanzisha kampuni, na kusajili business name, ila kuanzisha Kijikampuni sijui kwa kweli, wana JF wenzetu watusaidie
   
 3. Meale

  Meale Member

  #3
  Oct 22, 2010
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama unamaanisha kampuni, kwanza unapanga kampuni inatakiwa ijishughilishe na nini. Unaandaa vile vinavyohotajika kwa kazi hiyo ikiwamo ofisi. Unaweza kwenda ofisi za Brela na kuandika barua kuulizia jina unalotka kutumia (name search) au kutumia web yao kuona kama jina la kampuni unayotaka kufungua halijatumika bado na kampuni nyingine.

  Kwa kusaidiana na mwanasheria unaandaa company memorandum na article of association kwa mujibu wa sheria (companies act 2002) then unapeleka Brela. Mengine utaelekezwa huko Brela.
   
 4. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sasa hawa Jamaa wa TRA wanaingia wakati gani?
  Kuna mambo ya TIN nasikiaaaaa tu, hebu wana JF nielimisheni
   
 5. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nitaeleza hatua:


  1. Unaenda BRELA (Jengo la Ushirika Mnazi mmoja floor ya 4). Hapo utapewa form ya kujaza kutegemeana na Unachotoka kusajili, aidha Business Name (kijikampuni cha mtu mmoja - sole propriator) au kampuni ya watu zaidi ya mmoja yaani Limited Company. Usajili wa Business Name (kuna confusion kuita kampuni, anyway tuite kijikampuni cha mtu mmoja) ni sh. 6,000/= (Elfu sita). Kusajili kampuni Kubwa Ltd NADHANI ni aidha 150,000/= au 250,000/=, cheki BRELA-Home for more info. Kwa kampuni ambayo si ya mtu mmoja basi ni lazima upeleke BRELA Maelezo yaitwayo Articles of Association (Ni aina ya mkataba/katiba utakaoonesha Wanahisa ni akina nani na kila mmoja anamiliki hisa ngapi, actually unaweza kuandika mwenyewe maana Articles of Association zimetapakaa hivyo itakuwa ni suala la kuedit tu na kuweka details zako kisha unaenda kwa mwanasheria akugongee mihuri kuliko mwanasheria kukuandikia Articles of Association ambapo utalipa pesa nyingi). Ukiishajaza form husika utaelekezwa kwenda floor ya pili jengo hilo hilo ili ulipie form hizo. Ukishalipia Cashier atakwambia siku ya kurudi floor ya nne ili ujue kama jina limekubalika, kama halijakubalika utaambiwa ubadilishe, ila wakati wa kujaza forms za kusearch majina ni vizuri ukataja at-least matatu ili kuwe na option. Kwa kawaida process za BRELA ni kama wiki moja. Kama usajili umepitishwa utapewa CERTIFICATES za kuthibitisha usajili (photocopy ya hizi watu huziweka kwenye ofisi zao ili TRA wakija wasikusumbue kuwa hujasajili). Hapo kinachofuatia ni TRA.
  2. Pembeni ya jengo la Ushirika kuna Access Bank. Ukiingiia hapo Access Bank kuna ngazi panada hadi floor ya kwanza utakuta afisa amekaa hapo nje kwenye dawati. Mwombe form ya TIN namba, anaweza asikupe akakwambia nenda Tawi fulani la TRA baada ya kukuuliza iliko ofisi yako. Lakini anaweza akakupa pia maana form ni bure tu. Ila kama akikupa muulize ukishajaza upeleke tawi lipi la TRA. Utapewa forms 2 hapo TRA. Moja ni kwa ajili ya Ofisi ya Serikali za mitaa kujaza (itahitaji passport moja) ya pili ni taarifa a kampuni unayofungua. Ukirudisha form TRA watataka forms walizokupa pamoja na photocopy ya mkataba wa pango la ofisi ikiwa umepangisha ili wakate kodi (ni ndogo sana, nadhani ni 1% ya pesa uliyolipa). Pia naaamini watahitaji copy moja moja ya Certificates ulizopewa BRELA. Ukiwa TRA utapewa mtu wa kukusaili ili ajue makisio ya mapato ya biashara utayofungua ili ufanyiwe makisio ya kodi utayolipa. Hili likiisha utapewa TIN number. Mchakato wa TRA ni wa siku moja kwa kawaida kama hautaenda hujakamilisha vitu. TIN number huwa ni bure nijuavyo. NB. katika form za TRA kuna sehemu za kujaza taarifa chache za Benki. Ni vizuri ukitoka BRELA ufungue akaunti ya benki kwa msaada wa form za BRELA au unaweza kutumia akaunti binafsi ambayo tayari unayo, haina shida hapa. Baada ya TRA ni Leseni ya Biashara.
  3. Leseni ya Biashara itahitajji uwe na TIN number, na Certificates za BRELA. Leseni hutoleewa katika ofisi zilizoteuliwa na Manispaa inakopatikana ofisi yako. Kwa Ilala unakwenda Arnaotouglu mnazi mmoja. Hapo utapewa form za kujaza ambazo baadhi zitaenda kwa afisa mipango miji wa Manispaa au jiji kama sijakosea na zingine utapeleka Makao makuu serikali za mitaa kwa bwana afya, utaelezwa vizuri hapo kwenye leseni. Kuna pesa fulani utalipia hapo kabla ya kupewa forms, sikumbuki lakini ni chini ya elfu kumi, nadhani ni kati ya elfu mbili hadi tano. Kwa habari ya Arnaotoglu huwa pana vimizengwe vidogo. Utaullizwa vimaswali-maswali. Huenda ukaambiwa "Utachelewa kupata leseni kama ..................takrima. Kuna baadhi ya vitu tunaweza kukusaidia kama mambo ya afisa mipango miji ikiwa utachangia.............." Ah, nchi yenu hii, wanaomba vi buku mbili mbili. Ni haki yako kupata Leseni bila kutoa rushwa by the way. Ukikamilisha leseni kinachofuatia ni kufanya biashara, kuvuta wateja, kulipa kodi na kuwa raia mwema. ALL THE BEST.
  NB. Naamini siko sahihi 100% kwa maelezo niliyoyatoa lakini nadhani ni around 98% accurate. Ni vizuri piaukawa unauliza katika ofisi unazopita ili wakueleze hatua baada ya hapo ulipo.

  Nawasilisha.
   
 6. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante Three D.
   
 7. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lazima nikupe senkyuu!
  Concise and clear. Ahsante sana!
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135

  Mkuu 3D Nimependezwa sana na Maelezo yako ila nataka nkuulize Swali Moja tu, kwamba mimi Brela nimesajili kampuni ambayo itakuwa itatoa services mbali mbali ila katika kuanza Biashara yangu nataka nianze na baadhi tu ya Service na nataka nifanye Biashara kwa kutumia jina ambalo linarfelect Service ambayo nataka kuanza nayo mfano, Kampuni yangu inaitwa X na itashughulika na mambo 1,2,3 nk lakini kwa kuanzia na kutokana na Mtaji nilio nao nataka kutoa huduma 1 kwa mfano je naweza kutumia jina lingine katika biashara ambalo ni tofauti na lilisajiliwa na Brela? Mfano ni kampuni ya IPP ambayo ina Radio one, ITV etc au MIC (T) ambapo wao wanatumia tiGO

  Asante sana
   
 9. Avocado

  Avocado Member

  #9
  Nov 25, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Helpful info thanks
   
 10. M

  Malila JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Usiseme kijikampuni, kumbuka mbuyu ulianza kama mchicha. Sema tena Kampuni, rudia tena, nataka kufungua Kampuni yangu, sema tena nataka kufungua kampuni yangu nijiajiri mwenyewe.Teheeeeeeeeeeee
   
 11. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  ahsante!! that is thinking big psychology
   
 12. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapa kuna mambo mawili ya kutazama. Nitaeleza kwa mifano uliyotoa:

  1. ITV, Radio One, EATV, CAPITAL etc, haya ni makapuni na yamesajiliwa kabisa. Ila ni makampuni ndani ya kampuni kubwa (Ippmedia Group of companies). Makampuni haya madogo huitwa makampuni tanzu (sub-company). Yamesajiliwa na hivyo yana aina fulani ya independence katika maamuzi ie ITV ina maamuzi yake nje ya Capital TV etc, ila kunaweza kuwa na board inayounganisha wakurugenzi toka sub-companies. In short haya yamesajiliwa na yanalipa kodi na kuajiri kivyao.
  2. tiGO siyo kampuni (to my knowledge, care is needed here) ila ni jina la biashara (trade name), kampuni ni MIC Tanzania Ltd. Usually trade name husajiliwa kwa nia ya kuzuia watu wasiige japo si lazima kusajili, ila mtu akiiga na akasajili huna wa kumlaumu. Ila watu wengi hata vyombo vya habari husema "Kampuni ya tiGO......" makosa kama haya yanavumiliwa kwa kuwa yako katika maongezi yasiyo rasmi ila kama kuna sherehe rasmi tiGO hujiita MIC (T) Ltd
  Sasa kujibu swali lako, kama utataka kutumia majina mengine mbali na ulilosajili, itategemea kama yataoperate kama makampuni au majina tu ya product za kampuni yako. Mfano umesajili kampuni kwa jina la Ndege Ltd ambayo itafanya kazi ya kuuza mafuta ya ndege, tiketi za ndege, kumiliki mahoteli na usafirishaji watalii kisha ukaona huwezi kufanya mambo yote haya kwa sasa kuna mambo mawili ya kufanya:

  1. Unaweza kuendelea na jina hilo na ukafanya biashara kwa kile uwezacho tu kwa kuwa sheria haikulazimishi uweze kufanya vyote kwa wakati mmoja. Ukisoma nyaraka za watu kufungua makampuni utashangaa. Utakuta Matonya ana kampuni inayodai itashughulika na kuombaomba mtaani, kujenga barabara na utalii mwezini!! Sheria inakutazama tu... ila kama biashara haziko related sana mfano kuombaomba mtaani na kujenga barabara BRELA hawana neno ila kwenye hatua ya kuomba leseni ya biashara watakwambia lipia leseni mbili tofauti.... kama kawa ukiongea takrima wanauchuna......
  2. Unaweza ukafungua kampuni nyingine mfano kwa jina la "Uchumi Hotels" ambapo katika usajili wa BRELA ni lazima iwe indicated kuwa ni kampuni tanzu ya Ndege Ltd na watu watakosa uwezo wa kisheria kufungua Uchumi Hotels zao. Option nyingine hapa unaweza kufungua Uchumi Hotels bila kusajili kama jina au kama kampuni (Nadhani ndiyo mzizi wa swali lako) ila itakugharimu sana pindi mtu akiiga halafu akasajili, mtasumbuana sana mahakamani hadi upate haki yako. Ila kama hutasajili, which is still fine, itafahamika kuwa hili ni jina la kibishara chini ya kampuni Ndege Ltd na kampuni hii (Ndege Ltd) ndiyo itakuwa responsible na mambo ya kodi etc.
  Nadhani nitakuwa nimejibu angalau kwa kiasi fulani kwa mambo ambayo ni major japo kuna uwezekano kuna viprocess naweza kuwa nimeviruka mf. namna ya kujaza form nk.
   
 13. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kanyagio huenda umeweka hii post yako huku na wewe una mawazo ya kijikampuni kichwani. Unasema kampuni unawaza kijikampuni. Kanyagio sema Kampuni, rudia tena kampuniiiii, waza tena kampuni. Wakuu huu si utani. Thanks Malila and Kanyagio.
   
 14. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #14
  Nov 27, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  That is why you are called GREAT THINKERS-Big Up All!
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Nov 27, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wasiliana na vijana fulani wana Kampuni yao inaitwa Business Services & Consultancy Ltd., wapo pale Business Millenium Park, Office Namba 7, Morogoro Rd. kona na Shekilango. Mimi nilikuwa nataka kulibadili shamba langu toka binafsi kuwa kampuni, nikajulishwa na hao vijana, kweli nimefurahishwa na service yao, watakufanyia shughuli yako, zako, zote zinazohusiana na mambo ya biashara kwa bei nafuu kabisa. Namba zao ni +255767277422
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Nov 27, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mmhh
   
 17. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #17
  Nov 27, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  unaguna nini CHEZO ! najua akili yako itakuwa imeenda mbali kutafuta calculator!!
   
 18. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #18
  Nov 27, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Safi Sana,ushauri-maelekezo yapi fasaha kabisa,mimi nilisajili business name,nikaenda TRA,hapo nilipigiwa hesabu nika-Blow ,sikuamini kwani nilikuwa nazungumza habari za kijikampuni jamaa akanitolea Calculator na kukutoa figure za mapato,kodi ilikuwa kubwa mmno,na inalipwa upfront,
  nilichofanya niliaga nimeanza ku-operate kienyeji kwani kampuni inatoa huduma hewa-Software solutions etc ,sihitaji duka la brick and mortar,kila kitu kipo online etc.mpaka hapo TRA watakapojipanga na kutoa huduma kwa kuzingatia startup positions.
  sasa nimepanuka nataka kuifanya Ltd,with Vat etc,
  Je usajili wa VAT ukoje
   
 19. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #19
  Nov 28, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  3D Hujasaidia mmoja, umetusaidia wengi sana! THANK YOU! Mimi nimemamliza mchakato wa BRELA, ila bado hapo kwenye TIN na Business License so umenipa urahisi wa kuelewa where to start! Kwa kifupi na-cut & paste maelezo yako iwe mwongozo kwangu!
  Heshima kwako mkuu!!

   
 20. t

  tajirisana Member

  #20
  Nov 28, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  3D, nakushukuru sana kwani hata mimi niko kwenye mchakato huo wa kuanzisha kampuni yangu, unaweza pia kunipa dondoo kama unataka kuanzisha taasisi ya fedha Microfinance institution(NGO na kampuni) mchakato ukoje na gharama zake
   
Loading...