Kuajiriwa vs kujiajiri, Kipi bora kwako?

kuajiriwa ni utumwa sana.tumia akil.na uwezo wako kufanya kazi yko.mwenyewe inayokufanya pia kuwa huru
 
Kuajiriwa siku zote ni utumwa.
Kuajiriwa sio utumwa mkuu" ni sehemu ya maisha km ilivyo kujiajiri

kujiajiri ni kwa watu majasiri tu (risk takers) ambao ni wachache sana duniani

Wenye roho ya kuku broiler kujiajiri ni risk worth of not taking .
 
  • Thanks
Reactions: me1
Huu ndo mpango mzima.... unaajiriwa na unaajiri. Sucurity ya maisha bora wakati wowote.
Kuajiriwa ni jambo zuri endapo kama utageuza ajira yako kuwa capital ya kuwekeza katika miradi mbalimbali utakayoona inalipa na unapenda kufanya.

Ila sijakupata mkuu Asprini unaposema SECURITY YA MAISHA BORA WAKATI WOTE.
 
Mtupatie mawazo ya biashara na sisi acheni uchoyo wa kusema nimeajiajiri halafu husemi biashara gani, siyo kila mtu anakipawa cha kubuni.
 
Inategemea na maslahi yepi unapata, mfano kama kujiajili mwenyewe napata laki 4 kwa mwezi na kuajiliwa napata mil 1 kwa mwezi,haina maana ya kujiajili hapo
 
Ajira tamu chache sana.. Nyingi ajira uchwara tu za kukufanya uishi kwa stress!!

Huku kwenye kujisimamia kuna raha yake, niliacha kazi 3yes ago na hakuna ninachojutia... Biashara zimekuwa na nimeajiri vijana pia!!
Tuambie ulipata wapi mtaji na unawezaje kumanage hyo biashara yako.Vp mwanzo ulikuaje?
 
Kama nilivyoeleza mkuu kama hali ikiruhusu ipo siku nitajikuta nakuwa fully self employed. Muda wa kusimamia kazi zangu napata kutokana na aina ya biashara ninazofanya, watu niliowaweka na pia management systems nilizoweka katika kila biashara husika.

Kuhusu ufanisi wa kufanya kazi mbili naona ni kawaida tu kwa sababu naiona, naisimamia na kuichukulia kazi yangu ya kuajiriwa kama aina mojawapo ya biashara zangu. Nikimaanisha kwa vile inanipa riziki na exposure kama ilivyo kwa biashara zangu binafsi, naichukulia kama aina fulani ya sehemu mojawapo ya kuwajibika. Mfano kama nina biashara zangu tatu za binafsi kazi yangu ya kuajiriwa naihesabu kama eneo langu la nne la kunipa riziki kama ilivyo kwa mtu aliyejiajiri jumla kwa kuwa na biashara nne tofauti. Sijui kama nimeeleweka vizuri mkuu?
Hapo nimekupata mkuu,vip unaweza toa mfano wa kaz ambazo mtu anaweza kuzifanya pamoja na kuwa na ajira kwa mtu mwingine
 
Kwangu mm kutegemea kaz moja kwa awamu hii n kujitakia presha buree kwa ushauri hata kama umeajiriwa kujiajiri ni muhim
So mkuu kama hutak presha kwanin usichague upande mmoja ili uwekeze nguvu zote huko?
 
Kuajiriwa sio utumwa mkuu" ni sehemu ya maisha km ilivyo kujiajiri

kujiajiri ni kwa watu majasiri tu (risk takers) ambao ni wachache sana duniani

Wenye roho ya kuku broiler kujiajiri ni risk worth of not taking .
Ahsante mkuu,nadhani wengi hawako practical.Yani utaskia mtu anasema jambo ambalo hata yey hajalifanya
 
Inategemea na maslahi yepi unapata, mfano kama kujiajili mwenyewe napata laki 4 kwa mwezi na kuajiliwa napata mil 1 kwa mwezi,haina maana ya kujiajili hapo
Sio kwamba maslahi ni juhud ya mtu?
 
jiajiri kwanza sa hv ukiajiriwa na serikali hakuna kwenda kujiendelza
la sivyo likizo bila malipo
 
Binafsi naona bora tu kuajiliwa kwasababu;
Uspokuwa makini mtaji ukiyumba tu umehalibu biashara
Ukiendekeza uvivu utalala tu na kwenda job late hatimaye wateja watakuona mzembe na kukuhama
Zikitokea ajal kama kuvamiwa na majambaz na vitu kama hivyo ndio mwanzo wa kulazwa hospital kwa plesha
Sasa kuliko hayo yatokee bora tu uwe na mwajili wako atleast utaepukana na hayo.
Ila ukijiajili mwenyewe yakupasa uwe na umakini sana
 
  • Thanks
Reactions: me1
Back
Top Bottom