Kuachiwa kwa Dkt. Slaa na wenzie, Upinzani muangalieni kwa macho ya kijasusi Mwandishi Bollen Ngetti

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Wakati mwingine tuongee ukweli. Mimi ni muumini wa demokrasia. Kuna mtu nchi hii asiyeeleweka. Ni Mwandishi Bollen Ngetti. 2010 huyu Dk. Slaa alimtuhumu kutumiwa na TISS na kuhadharisha viongozi wa Chadema wasimpe ushirikiano.

Wiki tatu zilizopita alisambaza clipu ya video akiliomba Jeshi la Polisi kuwakamata wote wanaomkebehi na kushambulia mkataba wa DP World.

Jana ameandika na kusambaza andiko akimuomba Rais Samia kuwaachia huru bila masharti Dk. Slaa na wenzake. Tunashuhudia leo Slaa akiachiwa na wenzake.

Huyu ni rafiki wa viongozi wengi sana wa Upinzani akiwemo Zitto Kabwe, James Mbatia, Mbowe, Mdee. Ifike mahali, tumshuku, tukae naye mbali. Si Mwema Kwa upinzani Tanzania. Chukueni hilo.
 
Ni kinyume chake, ananusa na kujua kinachofuata kupitia vyanzo vya jikoni, kisha anaandika kabla mipango haijatekelezwa kama maoni yake binafsi. Inamwongezea credibility.

Advantage yake ni kwamba siku akiandika propaganda inakuwa vigumu kwa wananchi wa kawaida kung'amua kuwa kaandika uongo.

Ile akaunti ya twitter ya kigogo ilikuwa na style hiyo hiyo kipindi cha JPM. Japo siku hizi credibility imepotea kabisa.
 
Kwa wale tunaopenda mabadiliko ya kweli nchi hii tumuepuke huyu jamaa ni jambazi wa Upinzani.
 
Back
Top Bottom