Rais Magufuli, Dkt. Antony Diallo alikuongopea kuhusu Bollen Ngetti, anatia huruma

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
396
1,377
Wanabodi nawasalimu.

Kama wewe ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania hasa miaka 10 iliyopita huwezi kusahau jina la kijana Bollen Ngetti aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Sauti Huru. Kati ya Mwaka 2013-2015 kijana huyu alikuwa mwiba kwa Chadema na viongozi wao.

Ni huyu kijana aliyeibua utapeli wa Dk. Slaa na Mbowe kwa CDU Cha Ujerumani hadi CDU kuvunja uhusiano na Chadema. Ni huyu huyu Bollen Ngetti aliyeibua hoja ya Dk. Slaa kupora mke wa mtu akiweka na picha ya Slaa na Mushumbuzi front page. Jakaya alimtumia sana kijana huyu 2010 kummaliza Dk. Slaa kupitia maandiko yake. Tundu Lissu amewahi kukiri, "huyu Ngetti ni hatari kwa Upinzani Tanzania". Huyu ndiye aliyesanifu "ujinga" kuwa Lowassa ni mgonjwa na watu wakaamini.

Mhe Rais Magufuli, nafasi ya uDC Arumeru na Kisarawe zilipokuwa wazi, wengi tulijua na kubashiri lazima ataongoza wilaya moja. Haikutokea. Badala yake tukasikia yuko jela kwa kukosoa Serikali yako. Sijui kama ametoka jela au la! Kijana huyu amekipigania chama chako kama Cha ukoo!

Si nia yangu kumpigia debe lakini nakuonesha unavyopoteza watu muhimu na adhimu kukisaidia chama. Naambiwa uliambiwa na Dk. Antony Diallo kuwa kijana huyo ni mfuasi wa Membe ukakasirika ukamwacha. Inawezekana kina Bollen Ngetti ni wengi CCM waliotelekezwa. Vijana wenye tarjiba kama hawa ni Hazina si wa kuwatupa. Je, kweli bado yuko jela kwa kosa la uchochezi? Kwa nini asisamehewe? Hivi kweli kina Jerry Muro, Jokate Mwigelo ni zaidi ya kina Ngetti?

Mhe Rais, namuombea Bollen Ngetti aachiwe then fanya naye kazi. Huyu ndiye Mwalimu wa David Mwakiposa. Usiwasikilize kina Diallo maana hawana nia njema.

Wadau, mwenye picha yake adondoshe hapa kiboko wa upinzani. Nina nia njema kujenga nchi yetu.
 
Kumbe ni kitu liongo liongo na lizandiki la kuzushia ugonjwa wenzake, kuua upinzani wakati ulimwenguni kote upinzani ndio sauti ya wasio na sauti halafu unakuja kulisifu jitu la hovyo kiasi hicho? Bollen Ngeti abaki hukohuko maana Kaka shetani hana rafiki
Kada mtiifu wa CCM lkn ndo mwanaCCM pekee mwenye ujasiri wa kukikosoa chama chake na Serikali. Naambiwa yuko Segerea sijui
 
Boleni Ngeti huyu mpinzani wa CCM toka lini akawa CCM? Soma machapisho yake humu toka Magufuli aingie madarakani 2015 ndipo utamjua uhalisia wake kuwa ni Lichadema
Eti na wewe ni LI CCM KWELI?
 
Pathetic. Eti unajiita critical thinker na wewe. My foot!
Yaani umbea umbea kuchongea watu ndio uhazina wa mtu.
Oh boy! where are we heading to these days?!
Uko serious we mjamaa. Anyhow, hayanihusu nsijetukana bure.
Haya ndiyo matunda ya siasa za CCM na sasa wanatoka hadharani kutuonyesha utendaji wao wa kazi.
 
Back
Top Bottom