Kuacha na kuachwa! Ipi ni shughuli pevu

Duh nyamayao pole mpenzi nadhani it was a shock of the year to you. Hawatabiriki hawa ila nasikia people say ni bora uolewe na mwanaume anayekupenda sana kupita unavyompenda wewe sijui kama ina ukweli. Maana wakijua unawapenda huota mapembe hawa (Inawezekana sio wote but hao walopita katika dunia yangu walikuwa hivi wote.

Naungana na Ally Choki na Nyota Ndogo- Nimeamua sitopenda tena, Kila nikipenda mwishowe naumia!!





swithati hakuna mapenzi yacyo na vikwazo mami, komaa na ulie nae tu coz ukisema huyu ana kukwaza kwa hivi yule atakuwaza zaidi yake, gangamala!


haa cku hizi jamaa ameishia kugawa mbegu mjini tu, anaishi na m/mke muda kadhaa wakipata mtoto anatoweka! anaishia kuniambia"wewe ndio mke wangu tu mana mpaka sasa cjapata m'mke wa kuoa"., namuona kama zuzu anaetaka kuzirai!...lol
 
Kuachwa kusikie tu kwa wenzako kusikutokee ni balaa,
ila kuacha kama mtu amekukosea kosa kubwa ambalo umeshidwa kuvumilia unaona sawa tu mana unakuwa na hasira.
 
mh! Nyamayao umenikumbusha mbali sana tumshukuru Mungu ameweka kusahau sijui tungekuwa na majonzi ya aina gani mpaka leo.
 
Mahawala iwa hawaachani kamwe hata siku moja wewe aliyekufundisha ukubwa akiomba mrewind utamnyima?Lakini unajua wewe usiseme hapa iwe siri.

Wewe Fidel80 wewe!
Unatakiwa ukiacha uache kweli. ukirudi nyuma utageuka jiwe!
Ila kama unavyosema watu kama wameachana kistaarabu mara nyingi kuna hako ka tendency cha kukumbukana hasa kama huko walikoangukia ni kubaya...( ipo mifano hai mingi).. cha msingi ni kuwa ukiacha basi acha na usiangalie nyuma!
 
katika maisha nilichojifunza ni kuwa suala la kuacha haswa kwa wanaume ni gumu sana badala yake huwa wanatafuta sababu za kumchosha mwanamke ashindwe mwenyewe, ila kusema si kutaki ni wanaume wachache waliojasiri hufanya hivyo ila wengi huwa ni wasononeshaji huwapa wawapendao majonzi na maumivu ya moyo na kinachofuatia ni mwanamke kwa kukwepa maumivu ya kila siku anaamua kuumia once hivyo suluhisho ni kujiaachisha mwenyewe baada ya kuona simu hazipokelewi na kama ni mke basi ndio pale anapoanza kudai kuachwa kwa kuwa amechoshwa na mateso na karaha.

Labda wanaume wanisaidie hapa ni kwanini huwa wakiona mapenzi yameisha huwa hawasemi tu bibie wahi pengine hapa kwangu yameisha!! kwakweli huwa ni mateso!!Ukweli kuachwa ni kugumu na kunauma sana ila mie ni bora mtu aniache kuliko kunitesa na marazote huwa natamani mwanamme aniambie unajua sikupendi hata kidogo nataka kuachana na wewe lakini katika umri wangu haijawahi tokea zaidi ya mateso na maumivu ya moyo mwisho naamua kujiachisha mwenyewe maana unaweza maliza miaka mapenzi hamna na kuambiwa nakuacha sikutaki huambiwi!!

NAdhani kila atakayeweka hadithi ya kuachwa lazima kwnza itakuwa imeanza na vituko na kejeli ndio separation ...ningefurahi hasa mwenye experience ya kuacha akaniambia aliachaje...kwangu mie kuacha naona ngumu bora niachwe ila pia sijawahi kuachwa huwa najiachisha kwa kuona mapenzi hayapo (au hapo ndio nakuwa nimeacha???) na ukweli sitamani kumrudia niliyejiachisha kwake
 
WAKUBWA!
katika maisha ya mapenzi,malavidavi na mashamsham yote,lipo swala a UPANDE WA PILI WA MAISHA YA MAPENZI......!which is KUACHA,na KUACHWA.

Ninayo imani kwamba matukio haya mawili yana hisia tofauti,maumivu tofauti,n.k n.k

bila kuangalia chanzo kinachopelekea maamuzi haya YENYE UCHUNGU MKUU (hasa kama anaelifanya,au anaefanyiwa ALIPENDA),KUNA MOJA WAPO linaweza kuwa 'SHUGHULI PEVU'

NAOMBENI TUJADILI,ipi inaweza kuwa shughuli pevu?


Mkuu nadhani kwanza kabla ya yote inategemea kwanza imekuwaje mpaka ukaachwa au akaachika hihihi...Anyway ni kwamba kuachwa inauma sana na mtu asikuambie kabisa na pia nadhani hujawahi kuachwa ndio maana umeuliza ila hata mimi pia sijawahi kuachwa ningeachwa nisingecoment so ingekuwa vizuri angekuja mtu aliyeachwa au kuacha akatueleza ila kwa mtazamo na kuangalia kuachwa nadhani inauma sana....ila sasa pia vile vile inategemea mtu anayekuacha yupo vipi kama yupo yupo tu uu hapo unadhani utakuwa na mawazo???Hamna cha mawazo wala hautoumia kabisa...Upo na mwanamke kazaa watoto 4 akikuacha unadhani utakuwa na hudhuni gani kwanza nadhani utafurahi hapo kuachika ukachukue wengine wenye faida zaidi na wazuri!!:rolleyes:
 
Bora kuachwa kuliko kuacha,kuachwa unakuwa huru kumtafuta mwingine,kuacha hautakuwa huru kwani uliyemuacha aweza kukufuata wakati wowote.
 
Hakuna lenye uafadhali hapo ila tu kuacha kwa kuwa kunahusiana na matakwa ya moyo wa anayeacha maumivu hupungua kwa sababu kama angekuwa hataki maumivu au anayaogopa ni wazi asingeacha.

Ila usiombe ukaachwa na mtu ambaye bado wampenda ah! Mbona hutatamani kukuche.
 
Many people in poor countries goes in relation not becase they want and they aready to "relate", but rather they want "be related".
 
mh! Nyamayao umenikumbusha mbali sana tumshukuru Mungu ameweka kusahau sijui tungekuwa na majonzi ya aina gani mpaka leo.


kwanza ckuamini, nikasema wacha ni2lie 2 may b jamaa anatania au, haaa nikakaa cku 2 bila sms wala cal from jamaa nikajua sasa ndio bac tena, aliniuma vibaya sana!na kilichokuwa kinaniumiza zaidi ni kwamba cjui kosa/tatizo ni nini na hakuniambia lolote! nilikaa baada ya muda nikapata bfrnd ambaye alikuwa charming sana, yani nikikaa nae napunguza stress zote za kimaisha, nikafall, haa yakawa ya kuwa, nilimsahau mazimaaaa.
 
kuacha inauma zaidi, hasa kama umeacha mwanamke halafu ukachukua mwingine ambae unagundua baadae kuwa ni balaa! Unajuta kila siku hivi ni shetani gani alinifanya nikamwacha yule? Halafu kila siku ukikutana na uliyemwacha unaona ana maisha matamu na anakusikitikia sana unavyosota lakini hawezi kukusaidia!

Inauma sana kumwacha yule aliyekuwa anakuelewa vizuri na kukupenda halafu unaangukia kwa mtu ambae hakuelewi, anakusononesha tu! Inauma sana kumwacha mwanamke halafu unakuja kugundua baadae kuwa yule uliyemuacha ndie aliyekuwa anakupenda kikweli na huwezi kumpata tena! Kuacha ni balaa msiseme!
 
Wewe Fidel80 wewe!
Unatakiwa ukiacha uache kweli. ukirudi nyuma utageuka jiwe!
Ila kama unavyosema watu kama wameachana kistaarabu mara nyingi kuna hako ka tendency cha kukumbukana hasa kama huko walikoangukia ni kubaya...( ipo mifano hai mingi).. cha msingi ni kuwa ukiacha basi acha na usiangalie nyuma!

Ni ngumu WOS yaani kwa kile kitu kilicho kuwa kinakulusha roho alafu ukisahau dah kazii kweli kweli mi nitakuwa narewind tu kila tukionana...
 
Ni ngumu WOS yaani kwa kile kitu kilicho kuwa kinakulusha roho alafu ukisahau dah kazii kweli kweli mi nitakuwa narewind tu kila tukionana...
Na yeye awe tayari ku rewind basi! Kama yuko singo ndo unakuta anakubali hata kuwa nyumba ndogo.Kama kaolewa itakuwa shughuli.Mara nyingi mwanamke akishaolewa anajikita kujenga familia yake na kutunza ndoa yake.
 
.Mara nyingi mwanamke akishaolewa anajikita kujenga familia yake na kutunza ndoa yake.


HII KAULI INGEMEKWA INTO PRACTICE,sidhani kama watu wangefanikiwa kuchukuwa wake za watu..........!kizazi hichi cha nyoka dadaangu NI LAANA TUPU
 
These carry the same weight, depending the initiator, bcs kila upande una ulazima wake wa kudeclare interest and satisfaction
 
i don't understand yur statement!

Mimi nimesha-experience vyote kuacha na kuachwa. Labda nianze kuwa mie ni mwanaume. Nilikuwa na bibie nilikuwa nampenda kisawasawa. Siku ya siku nampigia simu akakataa kupokea. Niliporudia tena, akakataa kuwa siyo yeye!! What?? Wewe siyo Ltf? 'ndiyo siyo mimi'. Niliangalia tena namba ya simu na kupiga tena, the answer was the same. Nikajua nini kilikuwa kinaendelea.

Niliumia kidogo tuu, kwani nilijua amenisaidia. Unajua ukimpenda sana mwanamke na akajua hilo, ni hatari. Anaweza kukuaga wakati anaenda kumegwa na anajua kuwa unajua ila akafanya kwa sababu anajua huna jinsi. Nina self esteem ya kutosha na sikuona issue kubwa. Nikagundua baadaye sana she was involved elsewhere. Ni kweli the other guy had more money, ila hilo halikunisumbua sana kwani I knew huyu angenisumbua tuu. So I moved on.

Akatokea mwingine. Alikuwa chuma vile vile lakini aaa longo longo kibao. Ana njaa kila wakati. Hela hata umpe nusu ya mshahara wote bado haridhiki. Nikaamua kumpiga kibuti. Nikiri, nilikuwa na ugumu kufanya maamuzi ya kuacha zaidi na nilijihisi vibaya zaidi kuliko nilipoachwa. Niliona kama ananitegemea sana na nikajua kumuacha nitamuumiza. Sikupenda kumuumiza ila niliona ataniletea shida mbeleni. This was tough men! you simply cannot break the information to her. Hujui ata-react vipi, especially feelings unazo, ila ni compatibility issues.

Kwa ujumla, inatagemeana zaidi na your personality. Kuna watu kuwaumiza wengine is not an issue. Kwa hiyo huyu anaona kuacha si issue. Kuna mtu kuwaumiza wengine kwake ni vigumu, hata kama hao watu wanamuumiza yeye. Tunatofautiana. Kwa uzoefu niliokuwa nao, kwa wanawake wawili niliowapenda, niliyemuacha huwa naona inaniumiza zaidi. She was trully in love and the chemistry was OK. Ila sasa, huyu malezi yanamfanya aone kuwa mwanaume ni botomless pit. Simply mitazamo ili-differ. But she was fine. I mean huwa naona kama nilimuonea tuu. Hata leo nampa offer za kujiiba tu ila I can't lure her in bed. Siwezi. Nampa mshiko tu ninapokuwa na ziada na hajivungi, ingawa kumuacha kulimuumiza. She kind of understood.

No kuacha ni kugumu zaidi......of course kwangu.
 
Ikiwa mambo yote yako constant, kuachwa ni bora na rahisi. Huna mzigo wa kufanya maamuzi. Unarespond to the situation. eeezy!!
 
Ikiwa mambo yote yako constant, kuachwa ni bora na rahisi. Huna mzigo wa kufanya maamuzi. Unarespond to the situation. eeezy!!

Mkuu,
Kuna ving'ang'anizi wasiokubali kuachwa! Kila mara watakuvizia kukutilia fujo na kukukosesha raha utadhani una deni nae.Utashangaa mtu labda ni rafiki tu wala si mchumba lakini hakubali kuachwa!
Kuna wengine wao kuachwa ni kama kudhulimiwa kitu fulani.Wanachotaka wao ni waache tu!
 
Na yeye awe tayari ku rewind basi! Kama yuko singo ndo unakuta anakubali hata kuwa nyumba ndogo.Kama kaolewa itakuwa shughuli.Mara nyingi mwanamke akishaolewa anajikita kujenga familia yake na kutunza ndoa yake.

Aaaah wapi hii WOS hakuna kitu kama hicho eti mwanamke ajikite kulea familia na mabuzi ya nje amwachie nani na viserengeti boyz je?weweeeee....
Kwa nini wanawake wanawabambikia wanaume zao watoto?
 
Back
Top Bottom