Kremlin yasema hakuna mipango ya Putin kuzungumza na Trump

Kremlin yasema hakuna mipango ya Putin kuzungumza na Trump

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Msemaji wa Ikulu ya Urusi Dmitry Peskov, amesema rais Vladimir Puin hana mipango yoyote ya kuzungumza na rais wa Marekani Donald.
Hivi Karibuni Trump ameonesha hadharani kukasirika kwake na rais huyo wa Urusi, akionya wiki hii kwamba Putin anacheza na moto kwa kukataa kujihusisha na mazungumzo ya kusitisha mapigano na Ukraine, huku vikosi vyake vikiendelea kupata ushindi katika uwanja wa mapambano.

Licha ya kauli hiyo ya Trump, Kremlin ilisema jana kwamba kipaumbele cha rais Putin ni matakwa ya taifa lake kuliko kitu kingine chochote.
Kuhusu kufanyika kwa mazungumzo ya amani, Urusi ilisema bado inaisubiria Ukraine kuweka wazi, iwapo itahudhuria mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika mjini Istanbul siku ya Jumatatu, baada ya Kyiv kutaka Moscow itume masharti yake ya amani kabla ya kukubali kuhudhuria.
 
Indoda iyateta,.Kauli ya kiume hiyo,haina kumfagilia mpuuzi yoyote.Kanyaga twende Putin.
 
TRAMP yeye kapata Madini sasa ndio anapiga kelele za Aman!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom