Kosa la Mwangosi: Waandishi warudia Makosa

Status
Not open for further replies.
Kwahiyo na Waandishi walioandamana leo na wao Walistahili kupigwa Bomu la Tumbo?
Bomu la tumbo is a new phenomena. Angalia hoja ya msingi na sio kitu kingine ili tuweze kumuenzi Mwangosi kwa kufanya mabadiliko.
 
kalikenye kumbe una hoja dhaifu...sheria si polisi kulinda waandishi tu ni kulinda watanzania. Kumbe sasa kama unataka kuleta hoja ya maana kwa kuwa polisi hawapaswi kumuua raia wa tanzania labda ungeleta hoja ya kuvaa vazi la taifa watanzania wote ili mapolisi wanaoua watutambue ili wakiua waue sijui wakenya au wazambia.

Kwa taarifa yako polisi aliumizwa na bomu lile na alikuwa amevaa sare kwa hiyo si suala hilo wala si hoja bali ni polisi wabaya tu katika utendaji wao.
 
Last edited by a moderator:
Akili yako yanaonyesha ulivyo kituko hata kwa familia yako.
Siku nyingine umuulize mkeo kama unae kabla hujaandika huu upuuzi.

Kwa hoja za kipuuzi kama hizi, nawe waweza kuwa kikwazo cha maendeleo. Changia mawazo endelevu na sio kuonesha upumbavu wako.
 
kalikenye

Hivi wewe huna taarifa kuwa Kamanda Kamuhanda alikuwepo wakati Mwangosi anapigwa na askari? Hivi hujui kuwa Mwangosi alikuwa mwandishi wa habari wa muda mrefu sana?

Hivi hujui kuwa ni masaa kama 6 yalikuwa yamepita tangu Mwangosi amuulize kamanda Kamuhanda swali kwenye press conference kati ya waandishi wa habari na polisi?

Vyovyote itakavyo kuwa, kama Mwangosi alivaa au akuvaa sare, kifo chake kilipangwa au ni uzembe wa polisi.
 
Last edited by a moderator:
Mkomamanga

Please read btn the lines not on lines. Hoja yangu ni kwamba, licha ya makosa ya polisi, kuna another contributory cause nayo ci nyingine bali mazoea ya waandishi ya kutovaa Sare kwa kudhani kuwa wanafahamika katika mazingira yote.
 
Last edited by a moderator:
kalikenye

Yani kabisa ukanunua Credit, ukaweka kwenye Modem sijui Vodacom au Any other operator, then ukapost haya Matope, So unataka kusema that day waandishi wote Iringa walivaa hicho kitu, Mbona sio kweli, na leo Mbona hawakuvaa na hawajapigwa Bomu.
Umetumwa nn
 
Last edited by a moderator:

Hivi wewe huna taarifa kuwa Kamanda Kamuhanda alikuwepo wakati Mwangosi anapigwa na askari? Hivi hujui kuwa Mwangosi alikuwa mwandishi wa habari wa muda mrefu sana? Hivi hujui kuwa ni masaa kama 6 yalikuwa yamepita tangu Mwangosi amuulize kamanda Kamuhanda swali kwenye press conference kati ya waandishi wa habari na polisi? Vyovyote itakavyo kuwa, kama Mwangosi alivaa au akuvaa sare, kifo chake kilipangwa au ni uzembe wa polisi.

Ni uzembe wa pande zote mbili
 
kalikenye Mkuu,

1. Hivi ni waandishi wangapi hapa Tanzania uliwahi wakitumia nguo hizo tofaufi na vitendea kazi na vitambulisho?

2. Una uhakika gani watu wengine hawawezi kuvaa nguo kama hizo unazosema wawe nazo na kujifanya waandishi?

3. Kama watu wengine wakiweza kuvaa kama waandishi, utawatofautishaje?

4. Unapoongelea sare unamgusia nani? Kwani katika hili kuna Journalist, Reporter, Camera man, Informant, nk kumbuka wapo ambao hawajaajiriwa na shirika/kituo fulani lakini huongozana na wanahabari(mfano informants), hawa je?

Jambo unalolisema ni sahihi kuvaa sare, na kwa mtazamo wangu ni kwamba wanahabari hawakuona ulazima wa kufanya hivyo kama Marehemu David Mwangosi akiwa na kitambulisho na vitendea kazi vyake, kwasababu tu ya ile "AMANI" watu fulani wanayoiongelea.

ila kwa hali ya kutumia mabavu kwa serikali kupitia vyombo vya dola ni hatari hasa pale itapofika "sisi" tukishindana na "wao"..

but yet i stand firm to say despite uniform agenda, it's not significant reason to take someone's life, not anybody's life.
 
Last edited by a moderator:
Awe alivaa sare ya utambulisho bado mwangosi alikuwa na haki ya kuishi kama raia,
pia nimejaribu kufuatilia video zilizopo mtandaoni nimejiridhisha pasi na shaka kuwa mwangosi rip alikuwa maarufu mno kwaa viongozi kwani kila kiongozi alikuwa akimwita kwa majina yeye pekee ndo nimesikia jina lake likitajwa na rco na rpc pia...
 
Yani kabisa ukanunua Credit, ukaweka kwenye Modemsijui Vodacom au Any other operator, then ukapost haya Matope, So unataka kusema that day waandishi wote Iringa walivaa hicho kitu, Mbona sio kweli, na leo Mbona hawakuvaa na hawajapigwa Bomu.
Umetumwa nn

Please read btn the line
 
Ni propaganda zile zile za kuhalalisha na kutetea mauaji.....Lulu kuwa na marehemu chumbani tu ilitosha kumpeleka moja kwa moja mahabusu.....hao askari walioonekana wakimsulubu Mwangosi bado wanafanya nini mtaani kama sio kuua ushahidi.....Dunia nzima inajua kuwa polisi waliua.......Polisi kama wanaangalia sare wasingekuwa wanawashambulia vijana wa chadema kwa sababu huwa wanavaa sare.......uvae sare usivae sare hakuna cha kutetea mauaji, hii ni kama kujichukulia sheria mkononi.
POLISI wenyewe ndio majambazi wewe unategemea kweli watakuwa na huruma?
 
Please read btn the line
Hakuna cha Between the Line hapa, haya maneno yako yanafanana sana na ya Tendwa, Badala ya kulaaani kitendo cha polisi Kuua Mwandishi asiye na hatia, yeye anabakia kulalamikia Chadema.
Acha Ubwegw.e Kaka
 
Kwataarifa yako Marehemu Daudi Mwangosi alikuwa anatambulika vizuri na wauwaji. Ukifatilia vizuri katika mahojiano na RPC katika eneo la tukio (Nyololo), RPC alimjibu kuwa mbona hujashiba na majibu tangu asubuhi (zaidi ya hapo walikutana mapema asubuhi).

RPC aliarifiwa kuwa Marehemu Mwangosia anashambuliwa na polisi, na aliombwa amuokoe lakini yeye alipuuzia na kuachia anaowaongoza waendelee na amri aliyowapa. Hicho ndicho kinachotufanya tuamini kuwa alitoa amri ya kumdhuru Marehemu Mwangosi ikiwa ni sehemu ya kulipiza gadhabu zake za kuulizwa maswali ambayo alishindwa kuyajibu na kuonekana alikuwa hajui tafasiri ya sheria "nini maana ya mkutano wa ndani".

Sawa sawa mkuu Lyimo. Kuna wakati hata RCO alimwita kwa jina, pale kwenye ufunguzi wa tawi sehemu ya kwanza. Inawezekana hata kufahamika kwake na yeye kuwafahamu wengi waliokuwa kwenye operesheni ile (askari), kwa sababu alikuwa mtu wa maeneo hayo, yaweza kuwa moja ya sababu pia.

Watu wanaanza kupindisha ukweli, kwa kujenga hoja zao hapa. Mtaupoteza kwa muda lakini hatimaye utarudi pale pale, hata causal relationship haiwezi kuwa hivyo, eti hakuvaa nini vile...
 
Umetiririka vzr ila kumbe aliyevaa 'journalist' ndiye hapaswi kuuawa? Mimi nadhani uhai ni haki ya kila mtu hata nikivaa rubega, na adhabu ya kuandamana siyo kifo, pls usiwatetee polisi.

C watetei polisi. Please read btn the lines
 
Swali linabaki pale pale, nguvu yote ile ya police ilikuwa ni kupambana na nini ? au tuseme Police walitaka kumuua nani, kiasi wakakosea na kujikuta wamemuua mwandishi wa habari ? lets think deeply !
Aliyeanzisha huu uzi akijibu hili swali litamsaidia sana kuongeza uwanja wake wa kufikiri....... Nimekugongea like mkuu
 
Duh kumbe ambao hatunakazi tanzania hii ni sawa na mbwa koko tu yani thamani yetu inazidiwa na nyumbu,eti angevaa kizibao asingeuliwa hivi kizibao kinathamani kubwa kuliko uhai wa mtu!
 
Hakuna cha Between the Line hapa, haya maneno yako yanafanana sana na ya Tendwa, Badala ya kulaaani kitendo cha polisi Kuua Mwandishi asiye na hatia, yeye anabakia kulalamikia Chadema.
Acha Ubwegw.e Kaka

***** ni wewe usiyejua kuwa baada ya kifo chake tunapaswa kusonga mbele huku tukipambana na changamoto alizotuachia
 
Kwa hoja za kipuuzi kama hizi, nawe waweza kuwa kikwazo cha maendeleo. Changia mawazo endelevu na sio kuonesha upumbavu wako.

Duh kalikenye, ni vigumu kuamini kuwa Tanzania inao watu wa aina yako...what a waste!
 
Last edited by a moderator:
Please read btn the lines not on lines. Hoja yangu ni kwamba, licha ya makosa ya polisi, kuna another contributory cause nayo ci nyingine bali mazoea ya waandishi ya kutovaa Sare kwa kudhani kuwa wanafahamika katika mazingira yote.

This is ujinga at the highest level.
Kwa hiyo polisi walimuua Mwangosi wakidhani ni raia wa kawaida, hence its OK kuua raia.
Matusi yakitukanwa kwenye nyuzi kama hizi MODS muwe mnasamehe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom