Kosa la Mwangosi: Waandishi warudia Makosa

Status
Not open for further replies.
Thread hii imekosa nguvu za kisheria,no one is above the law,kuua tena kwa kukusudia haikubaliki hata kidogo. Sheria ichukue mkondo wake,
 
Mwandishi wa habari kutokuvaa sare si sababu ya msingi ya kuhalalisha mauaji au ukatili na unyama wa polisi. Jukumu la polisi ni kulinda usalama wa raia awe mwandishi wa habari au raia wa kawaida, Kitendo walichokionyesha polisi kule Nyololo Iringa ni picha halisi ya Polisi wa Tanzania walivyo wakatili na wasio na utu kwa raia walipakodi wa Tanzania. N a hii inajithihirisha kwa kuwa kamanda wao ndiye aliyeongoza unyama huo.
Swali ni je? kama kamanda wa polisi mkoa ( RPC) ambaye anatakiwa awe mfano kwa vijana wake anakuwa katili kiasi hicho, je hao walio chini yake watakuwa wanya kiasi gani.
Hivyo basi kutokukuvaa sare si sababu ya kuuwawa ndugu Mwangosi, bali ni kidhihirisho tosha kuwa polisi wa tanzania siku zote huwatendea unyama raia wa tanzania (RAIA WOTE WA TANZANIA WANA HAKI SAWA AWE NI MKULIMA, MFANYA BIASHARA AU MWANDISHI WA HABARI). Jeshi la polisi limeoza kufumuliwa na kujengwa upya.
 
Thread hii imekosa nguvu za kisheria,no one is above the law,kuua tena kwa kukusudia haikubaliki hata kidogo. Sheria ichukue mkondo wake,
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Wakati sipingi umuhimu wa waandishi wa habari kuvaa kizibao kwenye matukio, ni dhahiri mleta mada ni kibaraka wa waliokula njama kufanya mauaji yale.

Tazama idadi ya wanaounga mkono halafu tafakari jinsi serikali yetu inavyomwaga pesa kuendesha propaganda za kuwatetea madhalimu
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Usipende majibu mepesi kwa maswala magumu, this an oversimplification of the whole affair!!
tafakari tena urudi jukwaani! pole sana.

Hivi kweli katika akili yako umeridhika kabisa kwamba kutokuvaa sare au kitambulisho kunajustify mwananchi kutolewa uhai! kama issue ni sare kwa nini polisi hawakumkamata na kumfungulia mashtaka kwa kosa la kuwaingilia katika kazi yao?

Mabomu ya machozi ni kwa ajili ya crowd control, could David alone have constituted a crowd?!

Badala ya kuwalaumu waandishi kutovaa sare na vizibao ungejiuliza hivi polisi wanaisoma na kuielewa GPO (general police orders) ambao ndio msahafu wao wa kazi?!
 
kalikenye hebu acha longolongo zako hapa nimesoma nikidhani nitakutana na point yoyote itakayonifanya niendelee kutafakari kitu hata sijaona( kwa kifupi kubali kuwa Police wamechemka )
..Hivi unataka kunambia hao Police ama huyo sijui boss wao hawawajui waandishi wa habari..Na kama Mwangosi alikuwa mwenyekiti wa waandishi wa habari iweje wasimjue??????????????????????
...Na hata kama angekuwa si mwandishi wa habari ina maana alikuwa na haki ya kulipuliwa na Bomu...?????????????????????
::::umeambiwa walikuwa vitani hata kuanza kulipua mabomu?????????????????????????????????????????????
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom