Kosa la Mwangosi: Waandishi warudia Makosa

Status
Not open for further replies.
Every answer is a correct answer, but not every answer is the right answer for a respective question.

As you propound on a particular issue, you need to leave no stone un-turned, with a proof beyond reasonable doubt.

Ndugu zangu, tusimshambulie mleta mada kwa matusi na maneno ya kejeli, hayo maswali yatatakiwa kupatiwa majibu wakati wa kesi...of course yanaweza kuibuliwa while trying to justify the validity of the killing.

Mtoa mada, nionavyo mimi anania nzuri tu ya kuwakumbusha waandishi wa habari kuvalia sare zao za kazi, japo kuwa sare sio kigezo cha wewe kuwa mwandishi.

Kama kuna mtu amepata kuangalia documentary za Witness za Aljazeera, kuna moja inaonesha jinsi waandishi wa habari walivyoshambuliwa na majeshi ya marekani nchini Iraq kwa kigezo cha kutokuwa na sare au rebo ya Press.

Jamani waandishi, ndio kifo cha mwenzetu kinasikitisha na kinaonekana ni cha kudhamiria, lakini tuipende na kuiheshimu kazi yetu, when it comes to attacks, no matter how prominent you are, they can kill you and come to justify later as a mistake of fact. Make reference to the death of Gen. Imran Kombe.

Narudia tena, mleta mada amewakumbusha kitu cha muhimu sana waandishi, kuwa ndani ya sare zetu za press wakati tukiwa kazini, tuzingatie hilo tafadhalini.

 
kumjua au kutokumjua hakuhalalisha mtanzania (mwanadamu) kuuliwa tena kwa bomu,wewe unajaribu kuwatetea polisi,uko sawa kwa sababu nawewe ni miongoni mwao upo ndani ya system.
 
Wewe mtoa mada sikuungi mkono hata kidogo katika yote uliyoyaandika;


  • hujui kutofautisha kati ya raia na kazi
Waandishi wote nchini ni raia lakini pia wanafanya kazi ya uandishi kama ilivyo kwa raia wengine wanaofanya kazi tofautitofauti kama Ulinzi, uhasibu, ugavi, uhandisi,udereva n.k. Leo waandishi hawakukusanyika kufanya kazi ya uandishi, maana yake walikusanyika kama raia wenye taaluma ya uandishi ili kufanya kazi ya kiraia ya kuomboleza msiba wa mwanajamii mwenzao. uniform huvaliwa pindi unapokuwa kazini tu. Hata polisi au wanajeshi wakienda msibani hawavai uniform isipokuwa kama wamekwenda kikazi tu.


  • kukosea au kuvunja sheria hakukufanyi kuwa mkosaji bali mtuhumiwa
Hata kama Mwangosi alikosea kwa kutokuvaa uniform, bado alistahili kupelekwa na kushitakiwa kwenye vyombo vya sheria ili uchunguzi ufanyike na haki ichukue mkondo wake. Mbona aliyemuua hajauwawa badala yake anachunguzwa? Kwanini haikuwa hivi kwa Mwangosi?


  • Tangu lini TZ kosa la uniform ni jinai?
Haya tuseme alikosea kwa kutokuvaa uniform, Je hilo nalo ni kosa linalostahili adhabu ya kifo? Tangu lini kisheria adhabu ya kifo TZ inatekelezwa kwa Bomu badala ya kunyongwa?

Mimi naona yote uliyo andika ni pumba tu, hamna hata punje ya mchele.
 
Nadhani mleta mada kuna kitu ukijui, ni vuzuri leo tukuelimishe. Mara nyingi kizibao cha mwandishi wa habari uvaliwa hasa maeneo yenye machafuko ya kivita ili wanajeshi waweze kumtofautisha na adui. Anza kufuatilia hata waandishi wa CNN au BBC uone kama wamevaa vizibao kama si kwenye tukio la kivita, mwandishi pia uweza julikana kwa vifaa vyake alivyoshikilia. Waliomuua Daudi walikuwa wanamfahamu sana maana walikuwa nae toka asubuhi
 
Mkuu Lyimo, huyu kalikenye anaweza kuwa ndiye Kamhanda mwenyewe anatafuta mlango wa kutoke, kwani anataka kutuaminisha kuwa polisi wanaruhusiwa kuua watanzania wasiovaa sare. Hawa magamba wanakera sana kuanzishia uzi kwenye masburi yao lol.
 
Last edited by a moderator:
Kulya

Usiwe mvivu wa kufikiri,kuvaa nembo ya press ni sawa kama wangekua vitani,mazingira ya kumuua mwandishi kwenye ufunguzi wa shina la chama huwezi kufananisha na vitani,walimjua na walikusudia kumuua.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu wakati unaendelea na lawama zako juu ya polisi, tumia fursa hii kutazama upande wa pili wa shilingi kwa kujiuliza swali lifuatalo: Je angevaa sare angukuwa treated kama hivyo?

Ni sare au utu wa mtu? Sidhani kama polisi wetu wanazingatio lolote katika kazi zao zaidi ya kutumika kama mbwa. Ni mbwa ndio akiambiwa kamata anakamata bila kuhoji makosa wala kutazama haki ya mkamatwaji.

Nadhani tuzungumzie uadilifu wa policcm na serikali dhidi ya mtu yeyote na si dhidi ya sare za kazi fulani.

Ukiendelea kukazana na hoja zako za nguo nitaomba uniambie na WAFANYABIASHARA YA MADINI wavae sare gani ili nao wasiuawe kama walivyouawa wale wa5 kule msitu wa Pande na baadae wauaji wakaonekana hawana hatia. Msalimie Shigela, naamini mnafahamiana kwani mna akili sawa
 
Kigano

Polisi wetu hawana akili, akli yao inawatosha kutambua kuwa tumbo lina njaa, sasa ni saa ya kula. Ukitaka kujua kuwa ni wajinga nenda kituo cha polisi usikilize lugha zao CHAFU
 
Last edited by a moderator:
Umetiririka vzr ila kumbe aliyevaa 'journalist' ndiye hapaswi kuuawa? Mimi nadhani uhai ni haki ya kila mtu hata nikivaa rubega, na adhabu ya kuandamana siyo kifo, pls usiwatetee polisi.
Waandishi wa habari wasije kubweteka kwa kufukiri kuwa indignation ya matukio yaliyotokea ni kutokana tu na mwandishi wa habari kuuliwa.
la hasha.

Tatizo kubwa ni kuuwawa binadamu,mtanzania asiye na utetezi wala hatia.
Day light murder-thats the issue.

Wananchi tunapinga ile ku- cheapen life, a gift from God.
 
Usiwe mvivu wa kufikiri,kuvaa nembo ya press ni sawa kama wangekua vitani,mazingira ya kumuua mwandishi kwenye ufunguzi wa shina la chama huwezi kufananisha na vitani,walimjua na walikusudia kumuua.

Ahsante sana mkuu, sio mvivu wa kufikiri, ila lengo hasa mahsusi la mleta mada, pamoja na mengine ni kukumbushia kuhusu kuvalia sare. Pitia kwa upya comment yangu!
 
Ni kutokana na rai hiyo, nilitarajia waandishi wetu wangeweza kubaini kuwa, licha ya kosa la polisi aliyefyatua bomu, kulikuwepo na sababu ya awali iliyosababisha kutokea kwa kuanza kupigwa kwa marehemu Mwangosi. Pamoja na sababu zingine ambazo zimetajwa na wadau mbalimbali, kulikuwa na sababu moja ambayo haijatajwa sana nayo ni: MAREHEMU Mwangosi HAKUWA AMEVAA SARE ZA UANDISHI ambazo ni kizibao chenye maandishi ya JOURNALIST.

Hili ndo lilikuwa kosa kubwa ambalo naamini kuwa ndiyo chanzo cha marehemu kuanza kupigwa. Naamini kuwa, lau kama marehemu angekuwa amevaa sare yake, yasingetokea yaliyotokea.

Hakika wewe ni hatari zaidi kuliko hata Askari walioua. Askari wao waliamrishwa kufanya vile lakini wewe unatumwa na akili yako mwenyewe. Unataka kutuambia kuwa kule Iringa kulikuwa vita iliyokuwa inapiganwa kiasi cha mwandishi kujitambulisha kama vile waandishi wafanyavyo wanapokuwa katika uwanja wa vita?

Je, unasemaje kuhusu yule ndugu yetu wa Morogoro? Ulitaka naye alitakiwa avae mavazi gani maana yeye hakuwa mwandishi wa habari. Hivi ndugu yangu kwanini uutumie ubongo wako vibaya kwa kufikiria hoja kama hizi? Kwani una ulazima gani kuonesha ujinga wako huu humu jamvini?
 
mbona alikuwa na laptop na camera! Mbna wote walikuwa wanamjua...ikumbukwe yule walmtagt toka mwanzo, pia kwahyo ata kama sio mwandsh na hakuvaa hicho kikot ndo wauwe? Ni sheria hp inayo mruhusu polic kuongoa uhai wa m2 asie na kosa?
 
Ndugu wakati unaendelea na lawama zako juu ya polisi, tumia fursa hii kutazama upande wa pili wa shilingi kwa kujiuliza swali lifuatalo: Je angevaa sare angukuwa treated kama hivyo?

Hivi unajua maana ya kuvaa sare??? Kama hujui ngoja nikwambie.

Tunavaa sare ili tutambulike kwa urahisi. Mwanafunzi wa zanaki na yule wa Jangwani wanatofautishwa na sare zao na kutambuliwa kirahisi na sare zao. Mfanyakazi wa CRDB utamjua kwa sare anayovaa hata akiwa wapi.

Now back to your point:

Mwandishi Mwangozi alikuwa anatambulika bila hata ya sare. Hivyo kuvaa sare peke yake kusingemuokoa kama target ya polisi ilikuwa kwa waandishi. Pili Kuvaa sare kungerahisisha sana kazi kuliko hata kutokuvaa sare na hasa mtu anapokuwa na nia ya ku-target watu wa aina fulani.

Nimefundishwa kwamba, niepuke kuvaa sare, ziwe za chama, za kazini ama za aina yoyote ile na hasa katika mahali ambapo nahisi kunaweza kuwa na vurugu na aina fulani ya watu kuwa katika target. Likewise kwa waandishi hawashauriwi hata kidogo, unles kama wanakwenda Ikulu, Maelezo, makanisani, nk.

Nikukumbushe:

Mwandishi wa ITV na wa Star TV mwaka 2005 siku chache kabla ya uchaguzi walishambuliwa kirahisi na wafuasi wa CUF maeneo ya Buguruni na kujeruhiwa vibaya kwa kipigo kwenye makao makuu ya chama hicho kwa kuwa walikuwa wamevaa sare zao za vizibao kuwatambulisha. Waandishi waliokuwa hawana sare hawakujulikana kirahisi na wala hawakushambuliwa.

Naamini darasa hili limekuingia vema.
 
Mleta mada umeleta mada sahihi!!! Utambulisho wa PRESS ama JOURNALIST/MWANDISHI ni kweli kwamba huleta treatment tofauti na mwingine yeyote!
Tunajaribu kupinga lakini tunaona wapi tumekosea na kwa kuwa ni kawaida kutokuwa na vizibao hivyo tunaona ni sawa!
Moja ya treatment kama mwandishi amevaa utambulisho wa wazi ni kutohusishwa na kadhia iliyopo naye kuonekana kama ni miongoni mwa waliopewa amri ya kutawanyika na kukaidi!mfano ulio wazi ni kwamba angeweza hata kuambatana na askari wakati wanatawanya kusanyiko lililokaidi amri ya kutawanyika
Kusubiri kusema "mimi ni mwandishi" wakati wa kutekeleza ni kujipalia makaa ambayo mwisho wake si mwema!
Vitambulisho vya wazi tunaona ni kama RED CROSS/PRESS nyakati za vita,hawa hawalengwi moja kwa moja labda iwe bahati mbaya
 
Na hayo ni matokeo ya kutoheshimu na kuzipenda kazi zinazotupatia riziki

Sasa ni sawa unaposema Bw. Daudi Mwangosi akuwa amevaa sare,wewe unafahamu kazi ya askari polisi?
Kazi ya askari polisi ni kulinda raia na sio kupiga raia. Na nina hakika Daudi akuwa na kosa lolote lile.
 
Ndugu wakati unaendelea na lawama zako juu ya polisi, tumia fursa hii kutazama upande wa pili wa shilingi kwa kujiuliza swali lifuatalo: Je angevaa sare angukuwa treated kama hivyo?

Kalikenye usitutafutie ban ina maana chama chako cha hovyohovyo kimeidhinisha polisiccma wawe wanatuua kwa kosa la kutovaa sare? Kama sio, basi Didasi Masaburi anakuambia unafikiri kwa kutumia masaburi yako lol.
 
Ndugu wakati unaendelea na lawama zako juu ya polisi, tumia fursa hii kutazama upande wa pili wa shilingi kwa kujiuliza swali lifuatalo: Je angevaa sare angukuwa treated kama hivyo?

Hii si reasoning ya great thinker MODS tafadharini wekeni qualifying test ya watu kuwa members wa jamii forums..hii sasa aibu..1.The right to life is not based on what you wear, 2.The role of Police is to protect the society and not kill people, thats why even when they caught you torturing a thief, they will stop you and take him to Police for other legal proceedings and face charges at the court 3. Is the uniforms the only indicator as to who is a Journalists? Please MODS take my advice seriously
 
Mwana Mpotevu

Well said, kumbe anatakiwa kuvaa sare ili atambulike kirahisi?! Good.

Despite being a target, claim ambayo mahakama pekee, kwa ushahidi usio acha shaka ndio inaweza kuthibitisha as to whether he was targeted to be murdered, sare ingeweza kumtofautisha na mtu asiye mwandishi kwa urahisi, kitu ambacho in one way or another kingeweza kuokoa maisha yake, and not whether he is prominent or not.

Kwanini hakuvaa sare?

Hayo matukio ya waandishi kupigwa Buguruni thats another case ambayo siyo excuse ya mwandishi kutovaa sare!

Polisi au wanajeshi wangapi wameshapigwa au kuuawa mitaani wakiwa hawana sare? Make reference kwa kifo cha polisi mpelelezi huko Tabora kwa kupigwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi, alikuwa hana sare na ni kwasababu tu walimwona ni stranger kwenye maeneo yao na kulikuwa na tukio na wizi alilokuwa anapeleleza.

Sawa, sare sio uandhishi, ila ni muhimu sana kwa kazi yako!

 
Last edited by a moderator:
Hiv weye Kalikenye unatumia unataka kuleta hoja yako? Alama ya mwandishi au kutokuwa nayo ni haki ya polisi kuua?Kazi ya polisi ni kulinda raia na mali zao,na ile nyumba ilopingwa bomu nayo haikuvaa sare?Watu mfanowe mna tatizo kubwa.
 
Kulya

Mpendwa, maswali hayo yaweza kuwa sahihi. Haki ya kuishi ni ya kila mtu kwa mijibu wa Katiba ya Tanzania. Kwa kumuenzi marehemu apumzike kwa amani na tuache kuendelea kukosoa kosoa kutafuta alikosea wapi. Hivi REST IN PEACE maana yake ni nini?

Mwisho mwandishi wa habari anakuwa kazini Wakati wowote whether ana vazi au la. Kitendea kazi chake Kama ilivyo jembe kwa mkulima ni kamera. Mara ngapi tumeona madaktari wasio na makoti wakihudumia hasa kwenye dharura? Je akuhudumie au akatafute kwanza koti?

Stay blessed and kaka Mwangosi R.I.P na Mungu awe baba aw watoto wako na mume wa mjane. Kamwe wasipungukiwe na kitu chochote.

Queen Esther
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom