Kosa la Mwangosi: Waandishi warudia Makosa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kosa la Mwangosi: Waandishi warudia Makosa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kalikenye, Sep 11, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Ndugu wanajf napenda kuungana na waandishi katika kuomboleza kifo cha mwanahabari Mwangosi.

  Baada ya kuomboleza napenda kuelezea masikitiko yangu juu ya hulka au kile kinachoweza kuitwa mazoea ya waandishi wa.habari wa Tz. Licha ya majukumu yangu ya leo na kawaida yangu ya muda wa kurejea maskani, lakini leo ilibidi nivunje ratiba yangu kwa lengo la kuwahi nyumbani ili niangalie habari kwenye katv kangu hasa hususani habari ya maandamano ya waandishi.

  Lakini nimejuta kwa kupoteza muda wangu. Kwa hiki kifuatacho:

  Kwa kawaida, kwa mujibu wa imani zote tunazoamini watz wengi, ni kwamba, tunahimizwa pindi tupatwapo na msiba, tuliyobaki tunahimizwa kutumia fursa hiyo kujitafakari na kutafakari juu ya chanzo cha kifo cha mpendwa wetu kwa lengo la kutorudia makosa kama yapo, yaliyosababisha kifo cha marehemu.

  Kama itakmbukwa, wakati tulipokuwa tukijadili msiba wa Mwangosi, kuna mwanabodi mwenzetu aliturai kutumia fursa ya msiba huo kujitazama upya badala ya kuwatupia lawama polisi pekee.

  Ni kutokana na rai hiyo, nilitarajia waandishi wetu wangeweza kubaini kuwa, licha ya kosa la polisi aliyefyatua bomu, kulikuwepo na sababu ya awali iliyosababisha kutokea kwa kuanza kupigwa kwa marehemu Mwangosi. Pamoja na sababu zingine ambazo zimetajwa na wadau mbalimbali, kulikuwa na sababu moja ambayo haijatajwa sana nayo ni: MAREHEMU Mwangosi HAKUWA AMEVAA SARE ZA UANDISHI ambazo ni kizibao chenye maandishi ya JOURNALIST.

  Hili ndo lilikuwa kosa kubwa ambalo naamini kuwa ndiyo chanzo cha marehemu kuanza kupigwa. Naamini kuwa, lau kama marehemu angekuwa amevaa sare yake, yasingetokea yaliyotokea.

  Ni kutokana na imani kuwa waandishi wetu wangekuwa wametambua hilo na hivyo leo wangerekebisha changamoto hiyo kwa kuvaa sare zao za kazi zinazowatambulisha bila ya kuhitaji ushahidi mwingine kuwa wao ni waandishi.

  Nimefuatilia habari za waandishi wote waliojitokeza leo, nathubutu kutamka kuwa waandishi wote leo wamerudia kosa la marehemu Mwangosi la kutovaa sare.

  Naamini hata kule walikoruhusiwa kuandamana, ni kwa sababu za kishkaji tu kwani polisi walikuwa na haki ya kuwatawanya kutokana na kutokuwa na utambulisho unaowatofautisha na wananchi wengine. Kutokana na udhaifu huo, hata vibaka wangeweza kujichanganya nao na kuanzisha vurugu.

  Nawasilisha
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa yako, Marehemu Daudi Mwangosi alikuwa anatambulika vizuri na wauwaji. Ukifatilia vizuri katika mahojiano na RPC katika eneo la tukio (Nyololo), RPC alimjibu kuwa mbona hujashiba na majibu tangu asubuhi (zaidi ya hapo walikutana mapema asubuhi).

  RPC aliarifiwa kuwa Marehemu Mwangosia anashambuliwa na polisi, na aliombwa amuokoe lakini yeye alipuuzia na kuachia anaowaongoza waendelee na amri aliyowapa. Hicho ndicho kinachotufanya tuamini kuwa alitoa amri ya kumdhuru Marehemu Mwangosi ikiwa ni sehemu ya kulipiza gadhabu zake za kuulizwa maswali ambayo alishindwa kuyajibu na kuonekana alikuwa hajui tafasiri ya sheria "nini maana ya mkutano wa ndani".
   
 3. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Na hayo ni matokeo ya kutoheshimu na kuzipenda kazi zinazotupatia riziki
   
 4. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,139
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo na Waandishi walioandamana leo na wao Walistahili kupigwa Bomu la Tumbo?
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Akili yako yanaonyesha ulivyo kituko hata kwa familia yako.
  Siku nyingine umuulize mkeo kama unae kabla hujaandika huu upuuzi.
   
 6. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 449
  Trophy Points: 180
  Umetiririka vzr ila kumbe aliyevaa 'journalist' ndiye hapaswi kuuawa? Mimi nadhani uhai ni haki ya kila mtu hata nikivaa rubega, na adhabu ya kuandamana siyo kifo, pls usiwatetee polisi.
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mleta mada ni hivi Mwangosi anajulikana mno Iringa na watu na askari pia. Hata walipokuwa wanampiga walijua walichokuwa wanafanya. Pole sana. He was a prominent journalist.
   
 8. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  hahaha chezea jf wewe
   
 9. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Lyimo

  Ndugu wakati unaendelea na lawama zako juu ya polisi, tumia fursa hii kutazama upande wa pili wa shilingi kwa kujiuliza swali lifuatalo: Je angevaa sare angukuwa treated kama hivyo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,213
  Trophy Points: 280
  I do not buy your shyt kalikenye. Better luck next tyme.
   
 12. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  kwani kibaka hawezi kuvaa sare ya journalist na kuanzisha vurugu?
   
 13. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo mwangosi angekuwa na sare asingepigwa bomu. Hivo ni sawa kumuua asiye na sare...raia wa kawaida! Ndo watz sie
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,825
  Trophy Points: 280
  Kwa iyo asiyevaa sare ya waandishi wa habari ndo anapaswa kufa??
  Pia kwa taarifa yako askari wanamjua mwagosi kuwa ni muandishi wa habari na walimuua kwa makusudi kwa amri ya kamhanda.
  No research no right to speak.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 15. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  UMEANZA VIZURI MWISHO Umeharibu.INA MAANA POLISI WANA HAKI YA KUUA WASIO NA VIZIBAO?NGUVU WALIYOTUMIA KUMDHIBITI MWANGOSI ILIENDANA SAWA NA HALI HALISI?UJUMBE WALIOPEWA POLISI NA MWANDISHI MWENZIE KABLA YA MAUAJI HAUKUTOSHA KUMTAMBULISHA MWANGOSI NI NANI?POLISI HAWANA KISINGIZIO
   
 16. K

  Kigano JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 349
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kalikenye

  Naomba nikukumbushe tu kuwa Police hawana haki ya kupiga na kuua eti kwa kuangalia sare. HAWAKUTAKIWA KUUA ndugu yangu. Kwa maelezo yako marefu, ni kwamba akiuwawa raia mwingine ni sawa. Police wanatakiwa kulinda raia na mali zao. Be it wamevaa sare au la ! HAWAKUTAKIWA KUUA.

  Mimi sioni kosa la marehemu. Vitendea kazi alivyokuwa navyo mkononi vilitosha kutambulisha kazi yake. I am sorry, but let's be realistic, objective, na tuyaangalie mambo kwa upana wake. Kizibao tu chenye neno "JOURNALIST" kingezuia police wale kufanya mauaji ya kikatili ? ingekuwa vitani, nakubaliana na wewe, maana ni pande mbili zenye hasira zinapigana, so mwandishi wa habari anatakiwa kujitambulisha. Pale ni kwenye ufunguzi tu wa tawi la chama cha siasa. HAKUNA VITA.

  Swali linabaki pale pale, nguvu yote ile ya police ilikuwa ni kupambana na nini ? au tuseme Police walitaka kumuua nani, kiasi wakakosea na kujikuta wamemuua mwandishi wa habari ? lets think deeply !
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. pinkmousse

  pinkmousse JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 228
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naanza kuhisi kitu kizito kinanipitia hapa kwenye screen.
   
 18. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Ndiyo ingekuwa rahisi zaidi kumjua mbaya wao.
   
 19. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mleta thread ni kama ana akili ila hataki kuzitumia kwa sasa....anareserve za kuja kutumia akiwa kikongwe kusimulia hadithi wajukuu zake...sijui hata kama ana familia...Daudi Mwangosi alikuwa ni Mwenyekiti wa wanahabari Iringa...kama ilivyo katika mikoa mingi,huwezi ukamaliza wiki bila kupita polisi kupata habari either kwa kuitwa au kwa kuvizia. Hivyo vinguo unavyovisema vinatumika zaidi zaidi kwenye vita...wenzio walikuwa wananyang'anya kamera wewe unasema alikuwa hajajulikana kuwa ni mwandishi!!!ina maana hujAangalia video zote zilizorushwa hapa!? I guess hatutakiwa kujadili na wewe you are very low
   
 20. Raiamwematz

  Raiamwematz Senior Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 104
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kalikenye

  Hata kama walikuwa hajavaa sare, je polisi wamefundishwa kuua?? Mahakama zipo kwa ajili gani??? uwe unaupeo wa mambo unapo andika vitu kama hivi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...