Ni kweli watu wao wanakufa njaa kwa sababu uongozi unaweka pesa nyingi kwenye jeshi. Lakini uchumi wote umeanguka. Soma hapa
Korea Kaskazini - Wikipedia, kamusi elezo huru. Je nchi isiyoweza kukarabati trekta zake itaundaje mitambo ya kijeshi? Au kutengeneza ramia kwa mizinga zitakazolipuka wakati inayotakiwa? Basi soma hii
"Jeshi huwa na idadi kubwa ya vifaa lakini kuna tatizo kubwa ya kwamba
vifaru,
ndege za kijeshi na
manowari ni za kale sana na teknolojia ni ya miaka ya 1950-1970. Hakuna uhakika kiasi gani zinafanya kazi kutokana na hali bovu ya tasnia na uhaba wa vipuli. Korea Kaskazini ilijitahidi kutengeneza makombora na vifaa vingine kwa kunakili sampuli kutoka Urusi na China lakini inaonekana idadi iliyoweza kutengenzwa ni ndogo. Imekadiriwa na watazamaji kuwa wanaanga wanakosa mafuta ya kufanya mazoezi ya kutosha."
Korea Kaskazini - Wikipedia, kamusi elezo huru
Mapigano michache walipoingia dhidi ya Korea Kusini katika miaka 20 iliyopita walishindwa hadi sasa. Wanajeshi wa mpakani wanakimbia China kuomba au kuiba chakula ingawa wanaweza kuadhibiwa mno.