Korea Kaskazini: Tutazamisha meli ya Marekani

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945
_95755053_039100804-1.jpg

Haki miliki ya picha na AFP

Korea Kaskazini iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea, kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.

Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishw kwa shambulizi moja.

Kundi la meli za Marekani zikiongozwa na Vinson zinatarajiwa kuwasili katika rasi ya Korea wiki hii.
 
_95755053_039100804-1.jpg

Korea Kaskazini iko tayari kuzamisha meli ya kubeba ndege ya Marekani inayoelekea rasi ya Korea, kwa mjibu wa vyombo vya habari vya Korea Kaskazini.

Taarifa katika gazeti la Rodong Sinmun lilisema kuwa meli ya Marekani ya USS Carl Vinson itazamishwa kwa shambulizi moja.

Kundi la meli za Marekani zikiongozwa na Vinson zinatarajiwa kuwasili katika rasi ya Korea wiki hii.

BBC
 
Basi kumbe hufuatilii historia ya hawa jamaa tena wao usa walitoa taarifa kwa manwari yao ilipotea baada ya kupoteza mawasiliano baadae walipata kichwa cha komboralulilotumika kuhit

Kuna watu wanasukumwa na ushabiki na kuchukulia kuwa mambo huwa yako hivyo hivyo toka juzi, jana na hata leo.Nina Video Clip moja inayoonyesha tech ya hao Korea jinsi wanavyoweza kuzamisha hiyo Meli.Basi ninachokiona sio suala wa kuwagawia Wakorea mzaha hata kidogo.Ukitalii kauli za Trump na za Serikali ya Kim utaona dhahiri Marekani anafahamu vizuri uwezo wa NK. Na katika mshipa huo huo wa damu, NK wanafahamu ukweli wa wanachomuambia USA.
 
Nakumbuka mwaka 2006 walizamisha manwari ya USA na kuuwa wanajeshi 40
Si vile Bwana. Tarehe 26 Machi 2010 manowari ya Korea Kusini ilizama. Hakuna uhakika kama torpedo ya kaskazini ilikuwa sababu au kama iligongwa mwamba chini ya maji. Soma zaidi hapo https://en.wikipedia.org/wiki/ROKS_Cheonan_sinking.
Katika mapigano yote ya wazi kati ya manowari za Kusini na Kaskazini hao wa Kaskazini walishindwa.
Teknolojia ya kijehi ya kaskazini hadi sasa ni zaidi makumbusho ya kijeshi, walikopi vielelezo kutoka Urusi na China pia lakini hawana uwezo ila kupiga debe. nchi isiyoweza kulisha watu wake (na mara kwa mara wanajeshi wake wanaingia China kwa siri kutafuta chakula) itakuwaje? Manowari zao ni jeneza za kuelea majini.
Kuhusu tekonolojia yao ona picha hii:
220px-Korean_Peninsula_at_night_from_space.jpg

Sehemu ya giza ni Kaskazini, sehemu ya nuru ni Korea Kusini. Picha ilipigwa juu ya Rasi ya Korea kutoka angani wakati wa usiku.
 
Uzi kama hizi inafurahi tuu unafikiri kuna taifa litakubali kua wao ndio wako juu kwa teknolojia. Hizi ni propaganda za media tu. Hamna nchi inayopenda vita gharama zake ni kubwa mno uchumi ushuka kwa nchi zote iliyoshinda na iliyoshindwa
 
Si vile Bwana. Tarehe 26 Machi 2010 manowari ya Korea Kusini ilizama. Hakuna uhakika kama torpedo ya kaskazini ilikuwa sababu au kama iligongwa mwamba chini ya maji. Soma zaidi hapo https://en.wikipedia.org/wiki/ROKS_Cheonan_sinking.
Katika mapigano yote ya wazi kati ya manowari za Kusini na Kaskazini hao wa Kaskazini walishindwa.
Teknolojia ya kijehi ya kaskazini hadi sasa ni zaidi makumbusho ya kijeshi, walikopi vielelezo kutoka Urusi na China pia lakini hawana uwezo ila kupiga debe. nchi isiyoweza kulisha watu wake (na mara kwa mara wanajeshi wake wanaingia China kwa siri kutafuta chakula) itakuwaje? Manowari zao ni jeneza za kuelea majini.
Kuhusu tekonolojia yao ona picha hii:
220px-Korean_Peninsula_at_night_from_space.jpg

Sehemu ya giza ni Kaskazini, sehemu ya nuru ni Korea Kusini. Picha ilipigwa juu ya Rasi ya Korea kutoka angani wakati wa usiku.
DPRK imewekeza uchumi wake kwenye zana za kivita kitambo kwahiyo usishangae kusikia kuna njaa nchini mwao lakini kwenye masuala ya zana za kivita mtasubiri sana.
 
Af sijui watu mnaichukuliaje US,,,Kwa kifupi sidhan kma ipo nchi inayoweza kumpiga marekani,,,labda kwa muunganiko wa nchi nyingi
Ujue mtoto akiwa na ndevu nae anajiona anaweza akafanya kitu chochote.
Kama Jimbo la California pekee yake lipo juu kiuchumi na kiteknolojia na katika silaha kuizidi Russia. Tutegeemee kusambaratika kwa Korea yote, maana kitu watakachofanya kuwagonga na nyuklia na kupoteza kizazi chote cha North Korea
 
9737237f85dd34889a441594a10032b7.jpg
 
Back
Top Bottom