Korea Kaskazini: Kuzimu iliyopo duniani

Korea Kaskazini: Kuzimu iliyopo duniani

Hii ni picha iliyopigwa kutoka angani.

Tizama Korea ya Kusini, ina umeme wa kutosha. Nchi inang'ara.

Korea ya Kaskazini ipo gizani mpaka mpakani na China ndiyo unaona taa tena.

ImageUploadedByJamiiForums1455813260.913622.jpg
 
Hivi Kim Jong Un tokea ashike madaraka keshawahi kutoka kwenda ncho yoyote ya nje?
 
Umu watu wanaona north korea ni tishio kwa usa. Ni upuuzi kuwaza hivyo north kawekewa vikwazo kama ni tishio mbona anashindwa kuwapiga waliomwekea vikwazo?. Wanaishi katika utumwa wa vikwazo tu.
kwanini na yeye kama anajiamini amuwekee vikwazo, unapigana na mtu huku umemfunga kamba kuguzoni halafu unashangilia, ni kama leo tunawavyo wacheka zimbabwe,mambo mengine ya ajabu kweli, sasa kufua mtoni imekuwa ajabu, hebu nenda chiwata wilayani masasi halafu uje hapa kuleta majibu ebooh
 
Inawezekana ni kweli ukijaribu kufuatilia historia ya nchi za ujamaa huwa ndio inakuwa hivyo.
Hata nyerere mwenyewe aliwatesa sana mababu zetu na sera zake za ujamaa.
 
Mkuu Tokyo 40 hao wafanyakazi wa Kikorea waliopo China wanaweza vipi kuwatumia ndugu zao fedha (nasoma wana vikwazo vya kiuchumi/kifedha).

Nilisoma mahali wana simu zao zinaitwa ararrang, inakuwaje inasemwa wananchi hawana/ wamezuiwa kutumiwa mawasiliano ya Kiteknolojia?
 
DUUU kweli akili za kibongo shikamooo...mtu anadiriki kusema IQ za Wakorea wa Kaskzni ni ndogo?..Ni nchi pekee duniani isiyodaiwa hata sh.100 na taifa lolote...elimu ya anga za juu(space exploration) wapo vizuri hadi NASA wenyewe wanabaki mdomo wazi...Ukiwa na akili ndogo propaganda za kimarekani zitakufanya ujidharau kinomaaa...
 
aisee maajabu hayeshi duniani.asante sana kwa mada ya kusisimua
 
Mkuu Tokyo 40 hao wafanyakazi wa Kikorea waliopo China wanaweza vipi kuwatumia ndugu zao fedha (nasoma wana vikwazo vya kiuchumi/kifedha).

Nilisoma mahali wana simu zao zinaitwa ararrang, inakuwaje inasemwa wananchi hawana/ wamezuiwa kutumiwa mawasiliano ya Kiteknolojia?

Fedha za kigeni haziruhusiwi. Kila kitu wananchi lazima wasubiri kupewa na serikali.

Hata viwanda ambavyo Korea ya Kusini wameruhusiwa kuzalisha mali ndani ya Korea Kaskazini (Kaesong Industrial Region) vilikuwa vinalipa mshahara kwa dola lakini serikali ya Kaskazini inachukua hizo pesa za kigeni na kuzitumia kijeshi na wafanyakazi kulipwa kidogo kwa pesa zao. Wiki hii serikali ya Kusini ikaamua kufunga viwanda kabisa, kuwabana kiuchumi waliporipua bomu tena, kinyume cha matakwa ya Umoja wa Mataifa.

Ulanguzi upo na pesa zinatumwa kutoka China na Korea ya Kusini kisiri, siyo kwa kutumia benki. Kuna wananchi wengi raia wa China wenye asili ya Kikorea mpakani. Hawa ndio wanasaidia sana wakimbizi na kupeleka misaada kisiri kusaidia ndugu zao.

Kumbuka hata wakati wa Ujamaa wa Nyerere, tulikuwa tunapata dawa ya meno na vitu vingine adimu kwa njia ya ulanguzi. Hata dola ilikuwa hairuhusiwi lakini watu walikuwa nazo.

Simu ndani ya Korea Kaskazini hazina mtandao na kila kitu kinatazamwa na serikali kwanza. Lakini kuna wengine watu wenye connection na serikali na jeshi, wanaweza kutumia mtandao wa kawaida katika simu zao.

Hata kilugha sasa wanatofautiana. Kikorea cha Kusini kina maneno ya kigeni na kiteknolojia, Kikorea cha Kaskazini hakijabadilika. Wakimbizi wa Korea ya Kaskazini hapo Seoul wanasema lugha imekuwa kama ya kigeni, hawaelewi vizuri baadhi ya maneno.
 
si ajabu bunge liko mbioni kutunga sheria ya marufuku kwenda haja kubwa
 
DUUU kweli akili za kibongo shikamooo...mtu anadiriki kusema IQ za Wakorea wa Kaskzni ni ndogo?..Ni nchi pekee duniani isiyodaiwa hata sh.100 na taifa lolote...elimu ya anga za juu(space exploration) wapo vizuri hadi NASA wenyewe wanabaki mdomo wazi...Ukiwa na akili ndogo propaganda za kimarekani zitakufanya ujidharau kinomaaa...

Ni bila shaka Wakorea wa Kaskazini wana akili sana. Ila wanatumia pesa na nguvu nyingi katika mambo ya kijeshi na pesa kidogo sana katika kuendesha uchumi na kuwapa maisha bora wananchi wao.

Pia kumbuka, teknolojia zinauzwa pia. Ukiwa na pesa, hata Malawi au Nepal wakitaka elimu na vifaa vya kutengeneza kombora la Nyuklia wanaweza kununua kwa Wapakistani, Waisraeli, Warusi au Wahindi kwenye black market. Lakini watu watakufa njaa kama uchumi wa nchi ni mdogo.

Siyo kweli, Korea ya Kaskazini haidaiwi na nchi yoyote.

China ndiyo mfanyabiashara na mtoaji mkubwa wa misaada na mpelekaji wa watalii Korea ya Kaskazini.

China hataki jeshi la Marekani katika mpaka wake na atafanya kila kitu kusaidia Korea zisiungane kwa kuisaidia serikali ya Korea Kaskazini isipinduliwe au uchumi kuanguka kabisa. China ni Lifeline ya Korea Kaskazini. Inawakopesha sana ili wanunue vyakula na vitu kwao na uchumi wa China unanufaika pia na hiyo biashara. Na China ana monopoly ya biashara hapo, anafaidika sana katika vikwazo vya uchumi vilivyowekwa.
 
Hii ni picha iliyopigwa kutoka angani.

Tizama Korea ya Kusini, ina umeme wa kutosha. Nchi inang'ara.

Korea ya Kaskazini ipo gizani mpaka mpakani na China ndiyo unaona taa tena.

View attachment 324052
Kuna picha iliwahi kuchukuliwa kule Australia kwenye msitu mkubwa usio na watu. Ikaonyesha mwanga mkubwa kuliko .maeneo yanayokaliwa na watu yakiwemo pwani pwani. So hizi picha sio zA kuzingatia sana...
MpAka leo hawajui sababu sembuse nk wasikoruhusiwa kwenda...
 
Kuna vitu vingi mimi na wewe hatuwezi kujua. Picha nyingine ni mambo ya siri ya Kijeshi, camera tricks na kadhalika.

Kitu kimoja najua kwa uhakika:
Raia wa Korea Kaskazini wanateseka sana. Wasioteseka ni wanajeshi na familia na rafiki wa Kim Jong- un.

Wanaishi bila uhuru wa aina yoyote chini ya Dikteta, kizazi cha tatu.

Na hii ni rahisi kuthibitisha. Jiendee kama mtalii kutoka China kama nilivyoeleza katika mabango ya juu.

Mimi sijasoma katika magazeti na mitandao tu kuhusu ninayoandika hapa kuhusu Korea Kaskazini na siamini kila kitu kinachoandikwa.
 
Back
Top Bottom