Kondoo mwenye korani azaliwa

Salimia

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
665
103
KIJIJI cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimegeuka eneo la utalii baada ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo na maeneo jirani, kwenda kumshuhudia kondoo aliyezaliwa ameandikwa maneno mwilini kwa lugha ya Kiarabu. Waumini hao walifurika kijijini hapo juzi baada ya sala ya Ijumaa kumshuhudia kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita na kuacha watu midomo wazi kutokana na kuwa na maandishi yanayosomeka kiarabu ubavuni, yakitafsiriwa kwa Kiswahili kama Yasini. Kondoo huyo aliyezaliwa katika familia moja ya waumini wa dini ya Kikristo, aliwavuta waumini wengi kijijini hapo na kutoka nje ya wilaya na mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la ajabu na la kihistoria ambalo halijawahi kutokea. Akizungumza na HABARILEO Jumapili kijijini hapo, mmiliki wa kondoo huyo, Grace Massawe (55) alisema kondoo huyo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kwamba beberu huyo alikuwa na maandishi hayo, kutokana na kutotolewa nje na mama yake. Grace alisema baada ya kondoo huyo kuzaliwa, mama yake alibadilisha tabia na kukaa ndani ambapo awali alikuwa akila chakula nje na wenzake, lakini aligundua maandishi hayo baada ya kumtoa nje mwenyewe. Alisema awali aliona herufi ya W yenye rangi ya dhahabu, lakini siku zilivyozidi kwenda neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi, hali iliyompa wasiwasi na kutafuta msaada ili kutambua maana ya maandishi hayo kutoka kwa waumini wa Kiislamu. “Baada ya waumini wa Kiislamu kufika hapa nyumbani walibaini maandishi hayo ubavuni mwa kondoo huyo kuwa ya Kiarabu yanayosomeka kuwa Yasini,” alisema Grace. Alisema waumini hao walimweleza kuwa neno hilo ni muhimu sana katika Kitabu Kitakatifu cha Korani, ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho, pia ni moja ya sura muhimu ndani ya kitabu hicho. Katika hatua nyingine, Grace alisema katika ufugaji wake wa kondoo hakujawahi kutokea tukio la ajabu kama hilo na kueleza kuwa kondoo aliyemzaa alikuwa ni uzao wake wa mara ya pili ambapo awali alizaa kondoo wa kawaida. Alisema kutokana na kondoo huyo kuvuta hisia za watu wengi, pia viongozi wakubwa wa dini hiyo walifika kushuhudia maajabu hayo, akiwamo Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Lyimo. Baadhi ya waumini waliofika kumshuhudia kondoo huyo na kuzungumza na gazeti hili Aman Ramadhan na Yacoub Mushi wa Lyamungo, walisema tukio hilo ni muujiza wa Mungu uliojitokeza, hususan kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Juhudi za kumtafuta Shehe Mallya kuzungumzia tukio hilo, zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokewa. Source: Habari leo
 
Attachments

  • kondoo.jpg
    kondoo.jpg
    20.7 KB · Views: 690
Hiyo ni rangi tu ya tofauti yaani doa, haina uhusiano wowote, hata kama hilo neno ni la kiarabu itakuwa imetokea coincidence tu...msikauwe bure ka mwana kondoo ka watu, punguzeni ushirikina kiimani.(mwenye kujua imeandikwa nini atujuze)
 
Sasa mjomba, mbona unakurupuka? kila kitu kimeandikwa hapo, na hata maana ya neno imetajwa hapo juu, wewe unazuka ghafla unaanza kulaumu ushirikina nk,, inakuwaje mkuu? Ushagonga viloba vya fasta fasta au?
 
KIJIJI cha Uduru wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kimegeuka eneo la utalii baada ya waumini wa madhehebu ya Kiislamu kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo na maeneo jirani, kwenda kumshuhudia kondoo aliyezaliwa ameandikwa maneno mwilini kwa lugha ya Kiarabu. Waumini hao walifurika kijijini hapo juzi baada ya sala ya Ijumaa kumshuhudia kondoo huyo aliyezaliwa wiki tatu zilizopita na kuacha watu midomo wazi kutokana na kuwa na maandishi yanayosomeka kiarabu ubavuni, yakitafsiriwa kwa Kiswahili kama Yasini. Kondoo huyo aliyezaliwa katika familia moja ya waumini wa dini ya Kikristo, aliwavuta waumini wengi kijijini hapo na kutoka nje ya wilaya na mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la ajabu na la kihistoria ambalo halijawahi kutokea. Akizungumza na HABARILEO Jumapili kijijini hapo, mmiliki wa kondoo huyo, Grace Massawe (55) alisema kondoo huyo alizaliwa takribani wiki tatu zilizopita na hakuwahi kutambua kwamba beberu huyo alikuwa na maandishi hayo, kutokana na kutotolewa nje na mama yake. Grace alisema baada ya kondoo huyo kuzaliwa, mama yake alibadilisha tabia na kukaa ndani ambapo awali alikuwa akila chakula nje na wenzake, lakini aligundua maandishi hayo baada ya kumtoa nje mwenyewe. Alisema awali aliona herufi ya W yenye rangi ya dhahabu, lakini siku zilivyozidi kwenda neno hilo lilizidi kukua na kubadilika rangi na kuwa jeupe zaidi, hali iliyompa wasiwasi na kutafuta msaada ili kutambua maana ya maandishi hayo kutoka kwa waumini wa Kiislamu. “Baada ya waumini wa Kiislamu kufika hapa nyumbani walibaini maandishi hayo ubavuni mwa kondoo huyo kuwa ya Kiarabu yanayosomeka kuwa Yasini,” alisema Grace. Alisema waumini hao walimweleza kuwa neno hilo ni muhimu sana katika Kitabu Kitakatifu cha Korani, ambalo ni kama kitovu cha kitabu hicho, pia ni moja ya sura muhimu ndani ya kitabu hicho. Katika hatua nyingine, Grace alisema katika ufugaji wake wa kondoo hakujawahi kutokea tukio la ajabu kama hilo na kueleza kuwa kondoo aliyemzaa alikuwa ni uzao wake wa mara ya pili ambapo awali alizaa kondoo wa kawaida. Alisema kutokana na kondoo huyo kuvuta hisia za watu wengi, pia viongozi wakubwa wa dini hiyo walifika kushuhudia maajabu hayo, akiwamo Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) wa Mkoa wa Kilimanjaro, Shehe Rashid Mallya, na Shehe Mkuu wa Wilaya ya Hai, Juma Lyimo. Baadhi ya waumini waliofika kumshuhudia kondoo huyo na kuzungumza na gazeti hili Aman Ramadhan na Yacoub Mushi wa Lyamungo, walisema tukio hilo ni muujiza wa Mungu uliojitokeza, hususan kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Juhudi za kumtafuta Shehe Mallya kuzungumzia tukio hilo, zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokewa. Source: Habari leo
<br />
<br />
MASHAALLAH!ALLAHU AKBAR!
 
Huyo ,mamake atakuwa alikula kitimoto wakati waujauzito sio hivi hivi
 
Sasa mjomba, mbona unakurupuka? kila kitu kimeandikwa hapo, na hata maana ya neno imetajwa hapo juu, wewe unazuka ghafla unaanza kulaumu ushirikina nk,, inakuwaje mkuu? Ushagonga viloba vya fasta fasta au?
Ni kweli, nimekurupuka sibishi - msema ukweli mpenzi wa Mungu nakiri sikusoma thread mpaka mwisho, nikaingia kwenye keyboard! lakini sio sababu ya kiroba au valuu ila uvivu tu wa kusoma, which is very common in JF nowdays. Mimi nimekoma naomba na wengine wavivu wa kusoma muige mfano!!!
 
Waislamu ache ujinga! Hakuna maandishi yoyote hapo hilo ni baka la rangi nyeupe sio mchoro! Hivi mkienda umasaini si mtarudi na hadidu za maneno kibao maana kule wana michoro sio baka kama hilo!
 
hakuna cha ujinga kila mtu ana iman yake! So be careful with what u comment!! Never mess with anything that has 2 do with someone's faith.
 
Nendeni umasaini mkaone maajabu zaidi, kila neno lililoko kwenye kuran mtalikuta ubavuni mwa either mbuzi au kondo.
Kuna baadhi ya wadudu wakitembea wanaacha mchoro nyuma, wenye maandishi kama hayo. Na hapo vp mnasemaje? Wacheni hadithi za abunuwasi bana!!!
 
Back
Top Bottom