Tetesi: Kondakta asema nauli za Daladala kupanda kwa shilingi 200/=

Tunakosa MTU wa kutoa statement kimamlaka ,rais kusema vitu vitapanda ni dhahiri wengine wanapandisha kiholela .mh rudi tena tengua kauli watu wanaumia na huu mfumuko wa bei

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo mafuta yameongezeka kwa asilimia ngapi? Na mafuta ni asilimia ngapi ya jumla ya gharama za urndeshaji? Na nauli imepanda kwa asilimia ngapi?
 
Hivi kwann vocha za airtime hazipandi bei?
Au haziusiani na vita vya urusi na Ukraine?

Juzi nimepeleka nguo kwa fundi cherehani nae pia kapandisha,

Anasema hujasikia vita huko urusi?
Mafuta ya cherehani bei juu?

Inchi hii ishakuwa ya hovyo Sana.

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Hujui kwamba wanapunguza ukubwa wa kifurushi

Mfano Airtel zamani ukinunua kifurushi unapata cha dakika, chabdata na cha sms ila sasa vifurushi vinajitegemea
 
Hujui kwamba wanapunguza ukubwa wa kifurushi

Mfano Airtel zamani ukinunua kifurushi unapata cha dakika, chabdata na cha sms ila sasa vifurushi vinajitegemea
Kwanini wafanyabiashara wasingetumia mbinu hizo za vocha kuliko kutuongezea bei za vitu kila kukicha?

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
 
Wadau nipo kwenye daladala kutoka Bunju kwenda Makumbusho, kondakta anatutangazia abiria kuwa kesho nauli zitapanda kwa shilingi 200 kwa hiyo tujiandae.

Sijui kama lina ukweli wowote, ila kondakta anazidi kusisitiza. Tujiandae kwa lolote.

Asanteni, naomba kuwasilisha
Yy Mwenyewe Ndio aliwambia wapandishe Nauli
 
Kwanini wafanyabiashara wasingetumia mbinu hizo za vocha kuliko kutuongezea bei za vitu kila kukicha?

Sent from my M2101K7BG using JamiiForums mobile app
Mbona kuna baadhi ya bidhaa wamepunguza ukubwa/uzito.

Mimi kuna sehemu nilikuwa nanunua chapati kwa Shs. 1,000 zilikuwa kubwa yaani kumaliza ni kazi sasa hivi zimekuwa ndogo.

Hata mafuta kwenye vituo vya kuuzia mafuta (filling stations) bao wamepunguza ujazo kama ulishazoea kununua lita 1 ya petrol kwa Tshs. 2,400 ukienda na hiyo 2,400 utapata chini ya lita 1!
 
Wadau nipo kwenye daladala kutoka Bunju kwenda Makumbusho, kondakta anatutangazia abiria kuwa kesho nauli zitapanda kwa shilingi 200 kwa hiyo tujiandae.

Sijui kama lina ukweli wowote, ila kondakta anazidi kusisitiza. Tujiandae kwa lolote.

Asanteni, naomba kuwasilisha
Nauli haitakiwi kupanda zaidi ya 50 tsh kwa gari za abiria yan daladala kama suala ni kupanda kwa mafuta......nasema hivi kwa sababu ifuatayo mafuta yamepanda kwa sh 300 kwa litre 1 .kwa mfano daladala inatumia litre 150 kwa siku nzima maana yake ongezeko ni kama ifuatavyo
Litres 150x300=45,000 total

Endapo wataongeza gharama za nauli na kuwa 200 zaidi itakuwa ni wizi wa wazi kabisa na kuwanufaisha konda na dereva wake kwa kuwa wao wanaongeza nauli kama kila abiria.hapo kimahesabu wanatakiwa kucover ile hela yao tu iloyopanda kwenye mafuta na sio kujifichia humo na kuongeza 200 nzima.

Tuje kimahesabu ikiwa wataongeza 200

Tuassume kwa siku anabeba abiria 1500 kuanzia asubuhi mpaka analaza gari jion au usiku
Twende sawa hapa
(1) njia ya kwanza
Abiria 1500
Ongezeko la nauli 200

Calculation

1500x200=300,000 total

(1) njia ya pili
Kwa siku atabeba abiria 1000
Ongezeko nauli 200

Mahesabu
1000x200=200,000

Note .kwa maana hiyo ongezeko la 200 ni kubwa mno halifai kuwepo .chama cha madereva wanatakiwa kutulinda abiria na uhuni wanaotaka kutufanyia .wasijifiche kwenye kichaka cha mafuta kupanda kuumiza watu.

Endapo wataongeza 50 itakuwa suitable kwao na wananchi hatutalalamika sana maana hata faida yao pia wataiona ndani kwa ndani....

Assume abiria 1000x50=50000

Hapo dereva ameshacover hela ya ongezeko la mafuta.

Over.........
 
Back
Top Bottom