Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,557
Wakazi wa Kwa Mrombo mkoani Arusha wamelazimika kutembea kwa miguu baada ya madereva wa daladala kugoma kutoa huduma ya usafiri kwa kile wanachoeleza kuwa ni kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.
Madereva wa Daladala katika Mkoa wa Arusha wamegoma kuendesha magari yao kwa madai ya kupanda kwa gharama za uendeshaji ikiwemo ongezeko la mafuta huku bei ya nauli ikiwa ni ileile.
“Tumegoma kwa sababu mafuta yamepanda bei sana na nauli zipo chini zimetumika ndani ya miaka 15 nauli ni ileile na Matajiri wanalalamika” Fatma, Kondakta
Kwa upande wake Meneja wa LATRA Mkoa wa Arusha Aman Mwakalebela amesema utaratibu wa kisheria ni lazima siku 14 zipite na nauli zilizotangazwa zibandikwe kwenye magari hivyo kwa sasa Madereva hawaruhusiwi kupandisha nauli.
Chanzo ITV