Kombe la Dunia Qatar sheria lukuki zinazidi kumiminika, FIFA wayakanyaga

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
323
902
Wakuu ni hivi, kila panapokucha kumekuwa na lundo la sheria zinazozidi kutungwa nchini Qatar kwa mashabiki na watu mbalimbali watakaoingia nchini humo kipindi hiki cha michuano ya Kombe la Dunia, na mbaya zaidi hizo sheria zinawawekea vikwazo hadi wadhamini wakuu na washirika wa karibu wa FIFA na mashindano haya makubwa duniani.

Kwa ujumla hali hii aliiona Sepp Blatter ambapo hivi karibuni aliwahi kutamka hadharani mbele ya waandishi wa habari kuwa wanajuta kuipa Qatar uenyeji wa mashindano haya. Ni nini hasa kitakachotokea?

1. Hasara kwa makampuni wadhamini kushindwa kujitangaza kutokana na sheria zilizopo?
2. Mashindano kukosa mvuto?
3. FIFA kupoteza baadhi wa wadhamini na washirika wake wakubwa?
4. Mashindano haya kutopelekwa tena katika nchi za Kiarabu?

Karibu tuchangie mdau.
 
Back
Top Bottom