BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,357
- 8,069
Wakati Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yakiwa karibu kabisa kuanza, kupitia video fupi Mhariri wa uchambuzi kutoka shirika la habari la BBC Ros Atkin ameiongelea miaka ya tuhuma za rushwa ndani ya FIFA inayosadikiwa kupelekea Qatar kutunukiwa uwenyeji wa Kombe la Dunia 2022.
”Jumatatu iliyopita Rais wa zamani wa FIFA Sepp Blatter alitamka kuwa ”kufanya mashindano haya nchini Qatar ni kosa”
Jumanne, Balozi wa Kombe la Dunia nchini Qatar Khalid Salman alisema kuwa ”mahusiano ya jinsia moja ni uharibifu katika akili”
Swali kubwa ni je ”iliwezekanaje kwa nchi yenye watu milioni 3 , joto kali sana, na ambapo mahusiano ya jinsia moja ni kinyume na sheria kuchaguliwa kuwa wenyeji wa Kombe la Dunia?”
Kabla ya kupigwa kura, wanakamati wawili wa kamati kuu ya FIFA walitolewa baada ya uchunguzi uliofanywa na Sunday Times kubaini kuwa watu hao walikuwa wametoa ofa ya kuuza kura zao. Wanakamati wengine wote waliichagua Qatar na kuiacha Marekani ambayo ilionekana kupendwa zaidi.
Mwaka 2011 gazeti la Sunday Times liliripoti kuwa wanakamati wengine wawili walikuwa wamelipwa dola milioni moja na nusu kila mmoja ili kuipigia kura Qatar.
Siku chache baadae, barua pepe ilivuja iliyoonyesha Katibu wa FIFA wa kipindi kile Jerome Valcke akiwaongelea maafisa wa Qatar kwa kusema ”alidhani inawezekana kununua FIFA kama walivyonunua Kombe la Dunia.”
Kufikia mwaka 2012 uchunguzi mzito kuhusiana na mienendo ndani ya FIFA ulishaanza. Baadae ilijulikana kuwa FBI imekuwa ikiichunguza FIFA kwa miaka mingi na iligundua rushwa, utakatishaji fedha, malipo haramu yakiwa kama sehemu ya kufanya biashara ndani ya FIFA.
Hata hivyo mambo hayo hayakuhusiana moja kwa moja na jinsi Qatar iliyopata uwenyeji wa Kombe la Dunia.
Tunachofahamu ni kuwa hadi sasa wanakamati 11 kati ya 22 wa Kamati Kuu ya FiFA waliofikia uamuzi ule wamesimamishwa, kulipishwa faini, kufungiwa na wengine kushtakiwa kwa sababu mbalimbali.
Wiki hii Blatter amesema, "Ni hakika hii ilihusu pia pesa, kwa hili namaanisha nchi na siyo watu."
Miaka 12 baadae Qatar bado inakanusha kuhusika na lolote ambalo ni kinyume na sheria au maadili. Swali linabakia, kwanini mashindano haya yanafanyikia Qatar?