Kodi ya simu yapingwa rasmi mahakamani

Kodi ya simu yapingwa rasmi mahakamani

Sikutegemea FF kuwa ungekuwa na majibu mepesi namna hiyo,mi nina laini 2 moja natumia kwenye modem ambapo ikiwa kwenye modem hainiwezeshi kupiga wala kupokea simu zaidi ni msg tu ,kwa kuwa siwezi kuitumia kwa kupiga na kupokea simu inabidi niwe na laini nyingine kwa jili ya kupiga na kupokea kwa hiyo kuwa na hitaji la laini ya pili,kumiliki laini zaini ya moja sio UPEDESHEE bali ni hitaji muhimu katika zama hizi za usasa

Kama unatumia line moja kamili kwa ajili ya "msg tu" basi wewe ni Tuu (ya ki-Mombasa).

Na kama huwezi kulipia hizo line na hazina manufaa kwako, si zifunge na usilipie tu?

Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
 
usiwe KILAZA jaribu kujifikirisha,sio kila kitu utafuniwe.Haya meza basi ngoja nikutafunie.
Mimi kwa sasa nipo Dar kwa bussines zangu na bussines partiners wengi wanatumia sim card za tigo,hivyo kuepusha gharama za kupiga kati ya voda(line yangu )na tigo{partiners} itanibidi niachane na voda kwa muda ili hamie tigo,licha ya hayo Nimeiacha familia yangu mtwe mafi,kigoma mwisho tena kijijini kabisa,kule nertwork inayo patikana ni airtel pekee na wao(my family)kwa kigezo kilekile cha kuepusha gharama itabidi wanipigie kuptia line yangu niliyo tokanayo huko shamba(airtel).
Sasa hapo tayari ninakuwa na line ngapi?
Iwapo kampuni za mitandao yoote Tanzania zingekuwa na gharama moja ya kupiga kwenda mtandao wowte hapa Tz,naamini tusingekuwa tunabeba line 3'3
Umenisoma wee KILAZA.

Dah nimecheka tu
 
hivi kuna kodi ngapi zinakusanywa na hazisaidii chochote.uache kukusanya kodi ya maana kwenye madini na vitu vya maana tunakimbilia kodi za kipuuzi.na kama mwanzoni yalikwepa kodi serikali ilikuwa wapi.hii nchi ni kama kaburi la kuzika watu wakiwa hai.k....... mayo.
 
Nawashangaa Watanzania mnabeba simu tatu halafu mnakataa kulipia kodi.

Hii kodi iwepo na nnaikubali kwa roho kunjufu kabisa.

Na hizo kampuni za simu zitashindwa hii kesi na kila zitakavyochelewesha kuanza kukata hii kodi ndivyo tutalimbikiza kodi na tutaumia sisi zaidi na wao watajichotea humohumo. Ni wajanja tu hao.

Serikali iwaambie kama wanahuruma sana na wananchi wapunguze bei zao kufidia hii kodi.

Na Mitanzania ijinsi tulivyo mingine itaingia kichwachwa na kuwaunga mkono hizi kampuni ambazo hazitazami maslahi ya Mtanzania zaidi ya bishara yao tu.

Unatumia makalio kufikiria???
 
Ushasema "Mkuu" na yule katibu wa magwada anaendesha siasa zake za porojo JF ushaona siku hizi anakwenda kula bata na mje wa mtu kwa fedha za ruzuku? sasa kama hamtaki kulipa kodi mchumba atasusa.

Makalio yako
 
Unatumia makalio kufikiria???

Hako kasimu kako ndio kanakufanya hata leo umeijuwa JF na unaweza ukaingia na kuandika utumbo wako humu, halafu unaona tabu kukalipia elfu moja kwa mwezi. Unanshangaza!
 
Kama unatumia line moja kamili kwa ajili ya "msg tu" basi wewe ni Tuu (ya ki-Mombasa).

Na kama huwezi kulipia hizo line na hazina manufaa kwako, si zifunge na usilipie tu?

Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.


We ni kijinga sana, tumbafu kabisa
 
Kama unatumia line moja kamili kwa ajili ya "msg tu" basi wewe ni Tuu (ya ki-Mombasa).

Na kama huwezi kulipia hizo line na hazina manufaa kwako, si zifunge na usilipie tu?

Kodi ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
mie nina miaka 50 sasa nimelipa kodi tangu nikiwa na 25 yrs lakini leo kila kitu natoa mfukoni yaanj dawa hospital shule kunyonya mavi kuzoa takataka kuzima moto yote ...umeme tunasikia ni mcc msaada wa amerka barabara jika nk maji tu ni issue ndoo sh 700
 
mie nina miaka 50 sasa nimelipa kodi tangu nikiwa na 25 yrs lakini leo kila kitu natoa mfukoni yaanj dawa hospital shule kunyonya mavi kuzoa takataka kuzima moto yote ...umeme tunasikia ni mcc msaada wa amerka barabara jika nk maji tu ni issue ndoo sh 700

Unataka upewe hivyo vyote bure? nenda peponi aka mbinguni. Hapa uko duniani "kula uliwe".
 
Tena kodi yenyewe ndogo mnalalamika mijitu mingi humu Mibahili
 
ZIKIWA zimebakia siku mbili kabla ya serikali kuanza kuwatoza kodi ya laini (sim card) watumiaji wa simu, Taasisi ya Watumiaji wa Bidhaa na Huduma imefungua kesi Mahakama Kuu kupinga sheria hiyo.

Taasisi hiyo ya Consumers of Goods and Services Across the Country ilifungua kesi hiyo juzi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya hati ya dharura na kuanza kusikilizwa jana mbele ya jopo la majaji watatu.


Majaji waliosikiliza kesi hiyo ni Lawrence Kaduri, Aloysius Mujuluzi na Salvatory Bongole.

Katika kesi hiyo walalamikaji wanaiomba mahakama itangaze kwamba sheria iliyopitishwa na Bunge inayotaka kila mtumiaji wa simu ya mkononi kukatwa sh 1,000 kila mwezi ni kandamizi.


Walidai kwamba watumiaji wengi wa simu za mkononi hawana uwezo wa kukatwa fedha hiyo kwa mwezi, huku wakisisitiza kuwa itawaathiri watumiaji wa huduma hiyo.


Kwa mujibu wa madai ya walalamikaji hao, sheria hiyo inakiuka matakwa ya katiba ya nchi ya uhuru wa kupashana habari na kuiomba mahakama kuifuta sheria hiyo waliyoiita kuwa kandamizi.


Mawakili wa walalamikaji kutoka Kampuni ya uwakili ya Rex, Lugano Mwandamo na Merkizedeki Lutema walidai kuwa wateja wao wanataka mahakama imzuie Waziri wa Fedha kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoza kodi hiyo hadi hapo maombi yao yatakapotolewa uamuzi.


"Kuanzia sasa hivi mahakama itoe amri ya muda kuzuia utekelezaji wa sheria hiyo usitendeke," alidai Mwandamo.

Kutokana na maombi hayo, jopo la majaji liliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 3 mwaka huu, likimtaka wakili wa serikali, Kelley Mwitasi kuwasilisha maelezo yake kwa njia ya maandishi.

Wakati huo huo, majaji hao waliutaka upande wa walalamikaji kujibu maelezo ya upande wa serikali kwa njia ya maandishi na kuyawasilisha mahakamani hapo kabla ya Oktoba 7, ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa saa saba mchana siku hiyo.


Kufunguliwa kwa kesi hiyo kutasitisha utekelezaji wa utozaji wa kodi hiyo unaotakiwa kuanza Septemba 30 mwaka huu, baada ya TRA kuziandikia kampuni za simu waraka wa kuzitaka zianze utekelezaji wa sheria hiyo.


Sheria hiyo iliyopingwa na wanasiasa wengi bila kujali itikadi za vyama vyao, ilipitishwa kwa nguvu ya wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa Bunge la Bajeti na kutaka utekelezaji wake uanze Julai 30.

Bunge kupitia Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM) lilitaka kuwapo kwa kodi hiyo ili kusaidia shughuli za bajeti ya serikali kuu.

Kupitishwa kwa kodi hiyo kuliibua malalamiko ya wanasiasa hata wa CCM dhidi ya Chenge anayelazimisha kuwapo kwa kodi hiyo, huku akishindwa kuamini kwamba kuna Mtanzania anayekosa sh 1,000 kwa mwezi kwa ajili ya laini ya simu.


Malalamiko hayo, yalimlazimu Rais Jakaya Kikwete kukutana na wadau wa mawasiliano ambao ni wamiliki wa kampuni za simu Tanzania (MOAT), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, kisha kuwaagiza waiondoe kodi hiyo.

"Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la sh bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu," alisema rais kwenye kikao hicho.

Licha ya agizo la rais kutekelezwa kwa MOAT kutakiwa kuongeza kodi nyingine iitwayo ‘Excise duty' kutoka asilimia 14 hadi 17 bila kujali kwamba katika Bunge la bajeti kodi hiyo iliongezwa kutoka asilimia 12 hadi asilimia 14, kodi ya laini za simu haijaondolewa.

Wachambuzi wa masuala ya siasa na mawasiliano walisema kutojadiliwa kwa mabadiliko ya kodi hiyo ya simu ni dalili kwamba Waziri wa Fedha amezidiwa nguvu na kiti cha spika kinachounga mkono hoja hiyo ya Chenge na kushindwa kutekeleza agizo la rais.


Takwimu zilizotolewa na kampuni za simu zinaonyesha kuwa miongoni mwa wamiliki wa laini za simu milioni 22; milioni nane wanatumia chini ya sh 1,000 kwa mwezi.


Tanzania Daima
 
Ma CCM sometimes they do understand this kind of language manaa hayana utu kabisa na kila siku hawakusanyi kodi ina wanawabana masikini walio wengi .
 
Baba ritz akiacha safari zake zisizo na tija, gharama zake ni zaidi ya hii ya simu kadi.
 
Lakini pia yaipasa Serikali kuueleza uma inapata kiasi gani katika transaction za hela zinazofanyika kupitia simu (tigo pesa, m pesa, airtel money nk) make jamaa wanachinja mbaya siku hizi.
 
hizo wanazokata kwenye vocha na transaction za pesa ni nyingi sana bado wanataka tena na 1000? Kweli nchi hii mnyonge hana haki
 
Sisi wenyewe twajichimbia kaburi. Watu wako chitchat. Wala hawajui suala la tozo za simu.
 
Back
Top Bottom