Sisi wenyewe twajichimbia kaburi. Watu wako chitchat. Wala hawajui suala la tozo za simu.
Nawashangaa Watanzania mnabeba simu tatu halafu mnakataa kulipia kodi.
Hii kodi iwepo na nnaikubali kwa roho kunjufu kabisa.
Na hizo kampuni za simu zitashindwa hii kesi na kila zitakavyochelewesha kuanza kukata hii kodi ndivyo tutalimbikiza kodi na tutaumia sisi zaidi na wao watajichotea humohumo. Ni wajanja tu hao.
Serikali iwaambie kama wanahuruma sana na wananchi wapunguze bei zao kufidia hii kodi.
Na Mitanzania ijinsi tulivyo mingine itaingia kichwachwa na kuwaunga mkono hizi kampuni ambazo hazitazami maslahi ya Mtanzania zaidi ya bishara yao tu.
Ana simu moja, anachobadili ni sim card, kwa maana kwamba ni mteja wa makampuni matatu ya simu, Hivyo basi hana simu tatu, ila ana line tatu za simu kila line ikiwa ni ya shirika pekee la mobile phone.
Mimi moja wapo na line zaidi ya moja, moja Voda, moja Tigo na moja niendapo nchi za nje, hili ni jambo la kawaida nashangaa unashangaa kwa kushangazwa na mshangao wa line tatu.
Jambo la msingi hapa wewe unatazama nafasi uliyo nayo, huangalii wengine walio katika mazingira magumu ndio tunaowaonea huruma. Mimi binafsi kulipia line hiyo si tatizo, lakini je, shangazi yangu, binafu yangu, wakulima huko vijijini ambao wana simu hutumia kupita tu wanapokuwa na shida pengine mara mbili au tatu kwa mwaka tu.
Lipia zote tatu ni shillingi 3,000 tu, halafu una uwezo wa kwenda nchi za nje kama unavyojigamba na kulipia 3,000 inakushinda?
Toa porojo zako. Unanshangaza!
Jibu swali langu, tunaowaonea huruma na ndugu zetu na wananchi wetu walio na uwezo mdogo wa kulipia, wengi huko vijijini wanazo simu kwa matumizi ya dharura tu na pengine huzitumia mara moja au mbili kwa mwaka wawapo na tatizo, hao wewe huna uchungu nao unataka warudi mazingira ya zamani?
Nimeshakuambia mimi sina shida kulipia lakini kinachoniumiza moyo ni hawa wananchi wasio na kipata ambao uwezo wao wa kulipia simu line hawana, hutumia simu kwa kiwango ambacho ni chini ya hiyo 1000 kwa mwaka, wewe unaona ni sawa?
Wazo lilitokana na vijisenti haliwezi kuwa tetezi kwa wananchi. Chenge ni bepari aliyejawa kiburi cha pesa, amtetee nani? Jina sahhihi ni maccm na miccm...tutawaheshimu ktk lipi kama mahamuzi wanayoyatoa bungeni ni kandamizi!
Wadau nimepokea taarifa Kuwa Umoja wa Chama cha Kampuni za simu (MOAT) sio kile cha baba Mengi. . .
Leo wanaenda mahakama ya Kodi kuweka pingamizi kwa kila Mtanzania kukatwa shilingi 1000 kuanzia Mwezi Julai. Sasa niko njiani kwenda kuwaunga Mkono hawa jamaa...... Mimi nina Laini tatu inamaana nadaiwa elfu 9.
Mungu anisaidie. Watanzania tunaumizwa si mchezo.
usiwe KILAZA jaribu kujifikirisha,sio kila kitu utafuniwe.Haya meza basi ngoja nikutafunie.
Mimi kwa sasa nipo Dar kwa bussines zangu na bussines partiners wengi wanatumia sim card za tigo,hivyo kuepusha gharama za kupiga kati ya voda(line yangu )na tigo{partiners} itanibidi niachane na voda kwa muda ili hamie tigo,licha ya hayo Nimeiacha familia yangu mtwe mafi,kigoma mwisho tena kijijini kabisa,kule nertwork inayo patikana ni airtel pekee na wao(my family)kwa kigezo kilekile cha kuepusha gharama itabidi wanipigie kuptia line yangu niliyo tokanayo huko shamba(airtel).
Sasa hapo tayari ninakuwa na line ngapi?
Iwapo kampuni za mitandao yoote Tanzania zingekuwa na gharama moja ya kupiga kwenda mtandao wowte hapa Tz,naamini tusingekuwa tunabeba line 3'3
Umenisoma wee KILAZA.
Lipia zote tatu ni shillingi 3,000 tu, halafu una uwezo wa kwenda nchi za nje kama unavyojigamba na kulipia 3,000 inakushinda?
Toa porojo zako. Unanshangaza!
uwe unasoma na kuelewa we nae kakwambia yeye ndio anaweza ila vipi kwa wale wasio na uwezo? umejawa na wivu sasa waona kwenda nje ni kujigamba? kila mtu anakazi yake na mtu kwenda nje ni kawaida kutokana na ishu anazofanya. duh kweli tumetofautiana.