Klabu ya Yanga hawajachangia CCM pesa yoyote!

Klabu ya Yanga hawajachangia CCM pesa yoyote!

Msiharibu mali za club, msichome moto jezi zenu kuonesha hasira na kutokubaliana na kilichofanyika.. Klabu yenu ni nzuri sana ikikaa mbali na wanasiasa.. Michezo ni furaha.. Siasa ni fadhaa!
Sina ushabiki maandazi wa kuchoma jezi ila kwa hili lazima wawajibike waliohusika. Sitonunua jezi wala sitakwenda uwanjani kuishabikia timu yangu. Naamini wapo wengine wengi waliochukizwa na hili.
 
 
Sina ushabiki maandazi wa kuchoma jezi ila kwa hili lazima wawajibike waliohusika. Sitonunua jezi wala sitakwenda uwanjani kuishabikia timu yangu. Naamini wapo wengine wengi waliochukizwa na hili.
Kuna watu wana support kilichofanyika! Nimegundua ni mbogamboga ndani ya club
 
Hizo conspiracies hatuzijui. Tunachojua Rais wa klabu kaiwakilisha klabu kutoa mchango wa milioni 100. Mashabiki na wanachama imetukwaza. Propaganda za yanga kushiriki kupigania uhuru ni upumbavu tu. Tumeipenda yanga kwa sababu za kimpira sio za kisiasa. Binafsi morali ya kuelekea msimu mpya imeshuka sana. Bila viongozi kujitokeza kuomba radhi siwezi kutoa ushirikiano wowote wa kishabiki kwa hii timu.
Naungana na wewe ndugu. Morali imekata ghafla viongozi wameinajisi klabu na sisi mashabiki hatuna PAWA tena.
 
Muda Sio Rafiki Kwasasa!
Barua Zimesha-jam Kwenye ethics@fifa.org
utetezi wowote kwasasa inatakiwa upitie huko.
Basi na sisi wana Chadema,Act,Nccr tulioko Yanga mnachangia lini vyama vyetu. Yanga si ya wana CCM tu hilo ni kosa la kiufundi siasa itavunja club zetu. Michango ya ukombozi 1957 kwa TANU ni mazingira tofauti na sasa tuwe makini. Pesa zetu zirudishwe haraka.
 
Basi na sisi wana Chadema,Act,Nccr tulioko Yanga mnachangia lini vyama vyetu. Yanga si ya wana CCM tu hilo ni kosa la kiufundi siasa itavunja club zetu. Michango ya ukombozi 1957 kwa TANU ni mazingira tofauti na sasa tuwe makini. Pesa zetu zirudishwe haraka.
1957 kilikua chama cha ukombozi sio siasa.
 
Na je body ya wadhamini wanajua? Mweka hazina je!?
Hersi huwa hahitaji mweka hazina, anamruka tu kama kwenye usajili. Wadhamini wana mikataba yao. Hapo ilikuwa ni weledi, busara na hekima za Hersi
 
Baada ya mashabiki wa timu ya Yanga kulalamika kuhusu klabu kutoa milioni 100 kuchangia Harambee ya CHAMA cha CCM sasa Msemaji wa timu ya Yangafc Allikamwe amejibu malalamiko hayo. “Historia ya Klabu ya Yangasc kwenye ushiriki wake katika kuleta maendeleo ya Taifa la Tanzania, Kiuchumi, Kisiasa na Kimichezo haijaanza Leo wala jana .. Ni Klabu hii ya Wananchi iliyobeba sehemu ya Ukombozi wa Taifa hili.. Tumebeba Nembo ya Umoja, Amani, Upendo,Mshikamano na ukarimu wa Raia wa Tanzania Sio kwa Bahati mbaya Tukawa TIMU YA WANANCHI. Tuko kwenye Mikono salama WANANCHI wenzangu na Tunapaswa kujipongeza kwa kuibeba Taswira ya Tanzaniakwenye MICHEZO. Viongozi wetu wote waliopita, waliopo na watakaokuja Baadae In Shaa Allah, Jukumu lao kubwa ni kuilinda Klabu hii kama ilivyoasisiwa na wakubwa Matimu ambayo kiasili yalianzishwa kwa ajili ya MIGOGORO na CHOKOCHOKO hawawezi kuelewa Hii Falsafa yetu Young Africans Sports Club..” Una maoni yapi? Je umeridhishwa na majibu ya Msemaji? Tuandikie hapa
1755171523216.jpg
 
Hatimaye aliyetoa pesa kajitokeza... I was damn right.. Mashabiki maandazi njoni msome hapa😂
IMG_5912.jpeg
 
Iwe imetoa hizo pesa au haijatoa kitendo Cha club ya Mpira wa miguu kujihusisha na siasa wakati kina jua fika kwamba Sheria za FIFA haziruhusu ni makosa na wanapaswa kupigwa ban ,

Kitendo Cha kujihusisha na siasa wakati club Ina mashabiki wenye itikadi tofauti huo ni ushenzi , Wafungiwe tu
 
Stephen Munga FB anaandika

TUWAPE NAFASI YANGA KULIHESHIMISHA TAIFA

Kwenye mitandao yanaripotiwa mengi yaliyo ya kweli na yasiyo na kweli. Hata wachonganishi waliobobea wamo mitandaoni. Tunaendelea kujifunza kuikubali hali hiyo. Hata hiyo picha hapo chini si rahisi kubaini kama ni ya kweli ama hapana. Tunalazimika kujifunza kutokuwa na pupa ya kufanya maamuzi. Nyumba yetu imejaa moshi kwa hiyo hatuoni wala hatuonani vizuri.

Kwa hiyo basi, kwa manufaa mapana ya taifa na soka la TZ tuone kwamba klabu ya Yanga na wanachama wake hawakushiriki kuchangia CCM. Tuwape nafasi timu ya Yanga ambayo kwa sasa ni miongoni mwa timu kubwa barani Afrika ili wawakilishe na kuheshimisha taifa letu. Kwenye mkutano wa wanachama ujao waagize ukaguzi wa fedha ili kubaini ukweli na hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika kama kuna lolote baya.

Wanachama wa Yanga msiikimbie timu yenu. Makosa ya uongozi yasipanuliwe kuyafanya ni ya klabu. @Ninyi washabiki ndio Yanga na ipeni timu yenu sapoti kubwa zaidi. Na hata jezi mpya zinunueni kabisa na kuchangia kama kawaida yenu. Nijuavyo mimi Yanga haijawahi kushindwa kutatua matatizo yake ya ndani pasipo kuathiri nguvu ya klabu. Mliokasirishwa na habari za Yanga kuchangia CCM wekeni silaha chini na kurejea kambini kisha kaeni pamoja ili kujua ukweli na kufanya maamuzi kama taasisi.
FB_IMG_1755224661273.jpg
FB_IMG_1755224667708.jpg
 
Mimi ni SIMBA damu najuikana hivyo.. Na kama mtani wa jadi wa Yanga! Inapopata madhila nafurahi.. Ila kwa hili la kuchangia million mia moja nawatetea hawajafanya hivyo

Vilabu vyetu hivi vya soka vingi vinaongozwa na wafadhili na wadhamini, hawana vyanzo vya uhakika vya kuwaingizia mapato binafsi kama wao

Kilichotokea kwenye ile harambee ni michezo michafu ya kisiasa kupitia makundi yanayosigana kuelekea uchaguzi mkuu ili kuonesha kuungwa mkono kwenye kila kaliba

Kundi maarufu la wanamtandao waliopewa jina la wahuni ndio wamecheza mchezo huo mchafu kupitia kada wa CCM ambaye pia ni rais wa YANGA.

Huyu kwa kujua ama la akatwishwa zigo la kutangaza kiwango tajwa kuwa kimechangwa na Yanga (Young African Sports Club)

Nina hakika hakuna mwana Yanga kupitia viongozi wao aliyeshirikishwa kwenye hili.. Wote walishangaa tu kama wengine

Rai yangu kwa wana Yanga

Msiharibu mali za club, msichome moto jezi zenu kuonesha hasira na kutokubaliana na kilichofanyika.. Klabu yenu ni nzuri sana ikikaa mbali na wanasiasa.. Michezo ni furaha.. Siasa ni fadhaa!

Jipangeni mshikamane mumuwajibishe rais wenu! Huyu ndiye mchawi wenu.. Mumbane kupitia njia sahihi aseme alipata wapi hizo hela na ni nani alimpa mamlaka ya kuihusisha klabu na harambee ya kisiasa

Kwenye hili sisi SIMBA tunaweza kushirikiana nanyi kukomesha tabia hii mbovu ya wanasiasa wachovu kuvitumia vilabu vyetu kwa maslahi binafsi

Sisi SIMBA tunaojitambua tuko na Wana Yanga wote waliokasirishwa na tukio la harambee na tutakuwa nao bega kwa bega mpaka wanasiasa wakae mbali na michezo
Yeye ni Rais wa vilabu Africa. "
He should have known better " .
 
Back
Top Bottom