Klabu ya Yanga hawajachangia CCM pesa yoyote!

Klabu ya Yanga hawajachangia CCM pesa yoyote!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,652
Reaction score
860,937
Mimi ni SIMBA damu najuikana hivyo.. Na kama mtani wa jadi wa Yanga! Inapopata madhila nafurahi.. Ila kwa hili la kuchangia million mia moja nawatetea hawajafanya hivyo

Vilabu vyetu hivi vya soka vingi vinaongozwa na wafadhili na wadhamini, hawana vyanzo vya uhakika vya kuwaingizia mapato binafsi kama wao

Kilichotokea kwenye ile harambee ni michezo michafu ya kisiasa kupitia makundi yanayosigana kuelekea uchaguzi mkuu ili kuonesha kuungwa mkono kwenye kila kaliba

Kundi maarufu la wanamtandao waliopewa jina la wahuni ndio wamecheza mchezo huo mchafu kupitia kada wa CCM ambaye pia ni rais wa YANGA.

Huyu kwa kujua ama la akatwishwa zigo la kutangaza kiwango tajwa kuwa kimechangwa na Yanga (Young African Sports Club)

Nina hakika hakuna mwana Yanga kupitia viongozi wao aliyeshirikishwa kwenye hili.. Wote walishangaa tu kama wengine

Rai yangu kwa wana Yanga

Msiharibu mali za club, msichome moto jezi zenu kuonesha hasira na kutokubaliana na kilichofanyika.. Klabu yenu ni nzuri sana ikikaa mbali na wanasiasa.. Michezo ni furaha.. Siasa ni fadhaa!

Jipangeni mshikamane mumuwajibishe rais wenu! Huyu ndiye mchawi wenu.. Mumbane kupitia njia sahihi aseme alipata wapi hizo hela na ni nani alimpa mamlaka ya kuihusisha klabu na harambee ya kisiasa

Kwenye hili sisi SIMBA tunaweza kushirikiana nanyi kukomesha tabia hii mbovu ya wanasiasa wachovu kuvitumia vilabu vyetu kwa maslahi binafsi

Sisi SIMBA tunaojitambua tuko na Wana Yanga wote waliokasirishwa na tukio la harambee na tutakuwa nao bega kwa bega mpaka wanasiasa wakae mbali na michezo
 
Kosa lililofanyika ni la kiongozi wa Yanga kuihusisha timu ya Yanga (timu inayoshabikiwa na watu wenye itikadi tofauti za kisiasa) na hiyo harambee ya ccm, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo. Hiyo hela angetangaza ametoa yeye kama yeye, wala ingekuwa siyo shida.
 
Rais wao anasimama anasema sisi kama yanga tumechangia 100M arf unakuja kupinga ,ndg mwandishi unabisha Nini Kwan ww ulikuwepo?
Ukipenda ndugu msomaji unaweza kurudia kusoma kwa utulivu nilichoandika..lakini pia ukumbuke Yanga ina msemaji wake
1755048451427.jpg
 
Hizo conspiracies hatuzijui. Tunachojua Rais wa klabu kaiwakilisha klabu kutoa mchango wa milioni 100. Mashabiki na wanachama imetukwaza. Propaganda za yanga kushiriki kupigania uhuru ni upumbavu tu. Tumeipenda yanga kwa sababu za kimpira sio za kisiasa. Binafsi morali ya kuelekea msimu mpya imeshuka sana. Bila viongozi kujitokeza kuomba radhi siwezi kutoa ushirikiano wowote wa kishabiki kwa hii timu.
 
Rais wao anasimama anasema sisi kama yanga tumechangia 100M arf unakuja kupinga ,ndg mwandishi unabisha Nini Kwan ww ulikuwepo?
Ukipenda ndugu msomaji unaweza kurudia kusoma kwa utulivu nilichoandikaView attachment 3440484
Kosa lililofanyika ni la kiongozi wa Yanga kuihusisha timu ya Yanga (timu inayoshabikiwa na watu wenye itikadi tofauti za kisiasa) na hiyo harambee ya ccm, jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo. Hiyo hela angetangaza ametoa yeye kama, wala ingekuwa siyo shida.
Nadhani ukiongea wewe watakuelewa
 
Back
Top Bottom