denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,511
- 68,141
Askofu Dkt. Frederick Shoo
Alitoa agizo hilo katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Arthur Shoo.
"Hata tunapoelekea katika kipindi cha Pasaka najua huwa kuna mikesha, mikutano ya injili, makongamano mengi. Haya yote nafikiri kwa hali tunayopitia sasa, tusitishe wimbi hili lipite", alisema.
Askofu shoo pia amesema panahitajika elimu sahihi ya kujikinga na ugonjwa huo, akiwataka watanzania kuacha kufanya mzaha, huku akikemea tabia ya baadhi ya watu kushangilia pale viongozi wa kitaifa wanapopata ugonjwa huo.
Pia ametoa angalizo kwa wanaotengeneza na kuuza dawa za asili kutofanya kwa maslahi binafsi tu.
"Mnaotoa dawa za asili, msitumie kama fursa y kutengeneza biashara kwa kuwa tu, watu wanataka kupona na kujikinga"
Amewataka Watanzania kuacha mizaha na kushirikiana na wataalamu wa afya pamoja na kumuomba Mungu.
"Katika janga la Corona hatari sio kwa wale waliokwishafariki bali ni sisi hapa tunaopumua na kukohoa ndio wenye hatari ya kuambukizana. Nawaombeni sana, isiwe aibu wala isionekane ni kosa la imani kuvaa barakoa" alisema
====