KKKT waunga mkono uwekezaji Bandarini, TEC nao wataunga tu

Hujui kitu wewe,kwani TEC wanapinga uwekezaji au wanapinga mkataba mbovu?
Hâta Kkkt wamemwambia atumie busara katika mkataba huo
Unajua maana ya kutumia busara?
 
Kama kuna namba ya simu katika waraka wao kuwa huru kuwapigia.
Haina haja ya kuwapigia maana wameshasema wazi kuwa wanaupinga mkataba na wala si uwekezaji..!! Na wakaenda mbali zaidi kwa kuweka vipengele vya kwenye mkataba vinavyowafanya waupinge mkataba huo wa DPW. Nimeuliza swali hilo kwa namna hiyo ili mtoa hoja aweze kuelewa kwa urahisi hoja yangu ilipo..!!
 
Sehemu ya 3 na 4 na nyinginezo TEC wanasema kwamba Watanzania wana uwezo wa kuendesha hizi bandari na kwamba waongezewe uwezo zaidi jambo linaloonesha kwamba sio wanapinga mkataba bali wanapinga uwekezaji. Nashangaa baadhi ya watu walioongea hapo juu kama kweli wameupitia huo waraka.
 
Hao ni KKKT na wale wa jana ni Rc watakuja wengine waliokua tiyari kuuza nchi kwa vipande 30 then wataunga mkono ila kwa Rc ni Big No shida mnadhani Watanzania wa sasa ni wale wa Enzi za Kinjektile Ngwale hakuna mjinga tena nashauri #TEC huu waraka uendelee kusomwa zaidi hadi ngazi ya familia ili watu wajue madudu yaliyomo ndani ya huo mkataba wa kimangungo.
 
....usome ndani ya familia yako MWAKA MZIMA....

#Nchi Kwanza

Wewe ndio mnafiki huna tofauti na mafarisayo upo hapa kutetea ujinga siyo huo mkataba hata ukimpa mtoto wa Darasa la kwanza ataishia kuuchanachana hakuna kitu mule kiongozi aliyesaini ule mkataba alitakiwa awe Jela sasa
 
"Naomba ieleweke wazi Kanisa linaunga mkono uwekezaji, hatupingingi uwekezaji na tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji, hata hivyo jambo hilo limekuwa na maoni mbalimbali ya wananchi na vyombo vya habari, lakini Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba sisi viongozi wa dini zote tuliomba kuja kukuona pale mwanzoni na ulitupokea na tulikuletea maoni yetu kama viongozi wakuu wa dini, ukaahidi kuwa maoni yatafanyiwa kazi, tuna imani na wewe"

"Ninatambua kuwa ulipokea kijiti katika mazingira magumu sana, lakini pia pamoja na mazingira yale wewe ukaanza historia mpya ya nchi yetu ya kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Urais, kuna wengi hawakuamini, hawakutaki na mpaka leo wamebaki na jinamizi la namna hii, huu ulikuwa ni mpango wa Mungu"

"Najua katika jambo hilo linaelekea mahali tunataka kugawanyika kabisa, wengine wanatumia sababu za kidini, wengine wana maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi, nashukuru Mungu amekujalia hekima kama mama na kiongozi, umekaa kimya" - Askofu Dk Fredrick Shoo, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Miaka60YaKKKT


Hakuna mtu haungi mkono uwekezaji acheni upotoshaji. Tatizo ni mkataba na vifungu sio uwekezaji. Je unaunga mkono mkataba kama ulivyo? Hilo ndilo swali lakini mnatumia muda mrefu kupotosha watu badala ya kusaidia. Mkataba ukirekebishwa hakuna haya ya mashindano ya maneno kwasababu hiyo bandari sio ya chama. Wamesema wananchi wasikilizwe!
 
Mods hakikisheni kama ni kweli KKKT wamesema wanaunga mkono uwekezaji,licha ya mkataba kuonekana una kasoro katika baadhi ya vipengele.Kama habari iliyoletwa humu,ni upotoshaji,basi mfute uzi.Baadhi ya wadau,hutumia JF kama rejea.
 
Sehemu ya 3 na 4 na nyinginezo TEC wanasema kwamba Watanzania wana uwezo wa kuendesha hizi bandari na kwamba waongezewe uwezo zaidi jambo linaloonesha kwamba sio wanapinga mkataba bali wanapinga uwekezaji. Nashangaa baadhi ya watu walioongea hapo juu kama kweli wameupitia huo waraka.
Ni kweli watanzania wana uwezo wa kuendesha kama wakiongezewa uwezo. Kama ni ngumu basi DPW aje afanye ubia na serikali kwa kipindi maalumu kisichozidi miaka 30. Aendeshe bandari ya Dar essslam tu. Na mgawanyo wa fedha uwekwe wazi
 
Ila nchi hii jamani imejaza matakataka mengi sana, mleta mada naye ni takataka! Ulisoma wapi ambako TEC wanapinga uwekezaji?
 
Back
Top Bottom