KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Ya mungu mpeni mungu ya kaisar mpeni kaisar mada yako ilikua pombe
 
itabaki kuyaheshimu kama maoni yako binafsi. Biblia haisemi hivyo na nimeshaandika kwenye post za nyuma kwa nini naamini hivyo. Basi kama kuna umuhimu wa kuendelea na mjadala huu ni vyema ukazipitia objection zangu na kuzijibu.

Cha msingi tu sijaribu hata kidogo kumbadili mtu mtazamo wake ila kuuweka ukweli wazi kwa takaye kuuona!
Hayo sio maoni yangu Binafsi, nimeyatoa kwenye Biblia na nimekupa vifungu, si uende ukasome,
Wachungaji wengi wakifika kwenye hili andiko huwa wanakuwa surprised sana na hawaamini kama kwenye Biblia kuna kitu kama hicho nadhani na wewe ni mara yako ya kwanza kulisikia na kuliona hilo andiko

Mpe roho mtakatifu nafasi atakufunulia makuu kuliko uliyoyapa leo humu JF na utaiona kweli, nayo itakuweka huru

Alamsiki
 
K
YESU ALIITWA MLEVI KWA SABABU ALIKUWA ANAKUNYWA POMBE
Aliitwa anatoa pepo kwa beelzebub kwa sababu alikuwa mganga wa kienyeji

Umeelewa kitu hapo?

https://www.jamiiforums.com/neno://bible/Kiswahili UV.bib/40/12/22
"Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo"
 
Hayo sio maoni yangu Binafsi, nimeyatoa kwenye Biblia na nimekupa vifungu, si uende ukasome,
Wachungaji wengi wakifika kwenye hili andiko huwa wanakuwa surprised sana na hawaamini kama kwenye Biblia kuna kitu kama hicho nadhani na wewe ni mara yako ya kwanza kulisikia na kuliona hilo andiko

Mpe roho mtakatifu nafasi atakufunulia makuu kuliko uliyoyapa leo humu JF na utaiona kweli, nayo itakuweka huru

Alamsiki
Ni mawazo yako binafsi kwa sababu sicho mistari husika inachosema. Hakuna mahali mstari umesema Yesu alikuwa Mlevi. Mstari uko wazi kuwa ni mafarisayo ndio walimsingizia ulevi. Na hilo halikuwa jambo pekee walilomsingizia. Walishamsingizia uchawi kuwa anatumia mkuu wa pepo kutoa pepo kama ninavyomnukuu hapa:

"Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? "

Kwa hiyo kama masingizio ya Mafarisayo ndiyo msingi wako wa kusema Yesu alikuwa mlevi then inabidi kwa mantiki hiyo hiyo ukubali kuwa Yesu alikuwa mshirikina. Maana ni Mafarisayo haohao waliosema hayo.

Kama mafarisayo hawaaminiki katika hili la Beelzebub wanaaminikaje katika hilo la ulevi/unyaji pombe?

Mimi hilo andiko halinisumbui wala kunishangaza hata kidogo!
 
Dini ya kicristo ni dini inaobadilishwa mistari kila wakati, wanaotaka wenyewe

Nilisikia, redio idhaa, ya ujerumani wakisema hadi kufikia mwaka 2025 inatakia wabadili kipengele chochote kile kilichopo ndani ya, bibia, kisemacho mwanamke atakua chini ya mwanaume
 
Kwa hiyo kama masingizio ya Mafarisayo ndiyo msingi wako wa kusema Yesu alikuwa mlevi
Mbona mimi nimesoma post zote za Kituko hakuna mahali amesema Yesu alikuwa mlevi...

Alichokuwa anasisitiza na mimi kusistlitiza ni kuwa Yesu aliitwa na Mafarisayo mlevi...

Ndugu, hivi unajua kuna tofauti kati ya kunywa pombe na elevi...?

Nachokiona hapa kwako ni kuwa unataka kulazimisha pombe=ulevi..

Yesu alikunywa mvinyo(Pombe) ila hakulewa...Hivyo hakuwa mlevi...Kipi kigumu hapo kisichoeleweka..?
 
Mbona mimi nimesoma post zote za Kituko hakuna mahali amesema Yesu alikuwa mlevi...

Alichokuwa anasisitiza na mimi kusistlitiza ni kuwa Yesu aliitwa na Mafarisayo mlevi...

Ndugu, hivi unajua kuna tofauti kati ya kunywa pombe na elevi...?

Nachokiona hapa kwako ni kuwa unataka kulazimisha pombe=ulevi..

Yesu alikunywa mvinyo(Pombe) ila hakulewa...Hivyo hakuwa mlevi...Kipi kigumu hapo kisichoeleweka..?
jamaa anafanya strawman argument. andiko liko wwzi yeye anataka kumlisha kituko maneno.
 
Shida ni kuwa watu wanachanganya neno POMBE na neno ULEVI. Kilicho dhambi ni ulevi na sio pombe. Pombe ikitumika vizuri kwa makusudio yake ni jambo la kheri kabisa kwa mwanadamu, lakini ikitumika kama ulevi ni katazo kwa Mungu.
Hata Madaraka yaweza kutumika kama ulevi na kuleta madhara jee madaraka nayo ni dhambi? Kwa sababu Pombe na Madaraka vyote ukivitumia vibaya vinakuwa ulevi!
Kunywa pombe kistaarabu, burudisha nafsi yako. Na hasa kwa wakati huu ambao mambo ni vululu vululu kiuchumi basi ukipiga mbili tatu zako taratibu unajikuta unaburudisha ubongo na kukuepusha na ghadhabu au chuki kwa wengine.
Tusipende kujustify unywaji pombe kwa reasoning nyepesi hivyo........

Pombe ni haramu na hakuna lugha yoyote utakayoitumia kuihalalisha kuwa ni halali....

Ni vyema Maaskofu hao 2 wakaamua kwa hiyari yao wenyewe kulihama kanisa la KKKT na kuhamia kanisa la mzee wa upako, ili waweze kumjoin huyo Askofu mwenzao katika kupata ile kitu inaitwa bapa.........
 
Hata kama Mungu angeruhusu bado Pombe ni mbaya. Kabla ya kuinywa akili zinakua timamu ukishalewa unajikojolea hovyo na matusi kibao. Pombe mbaya na haifai acheni kujifariji. Hakuna maandiko yanayokataza kunywa sumu lakini mbona hunywi? Vitu vingine havifai by nature...
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.

Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”

Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.” Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”

Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”

Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano. Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?” Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.

Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe. Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT. Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.

Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.

Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.

Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.

Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.

Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake. Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.

Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake. Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Hata hivyo, Dk. Malasusa amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kuwanyooshea kidole waumini wanaotoka mikoa ya Kaskazini kuwa wanamsakama kwa vile katika uchaguzi mkuu uliyopita, limuunga mkono Rais Magufuli na kumsaliti swahiba wake wa miaka mingi, Edward Lowassa.

Chanzo: Mwanahalisionline
Hivi huyu si ndio alikumbwa na kashfa ya kupokonya mke wa mtu,na akaamua kumhamishia nje ya nchi?!!
Eeeh Mwenyezi Mungu utunusuru na hawa viongozi wa dini wanaojitoa ufahamu
 
Unaonekana kuwa na uelewa mdogo au bifu kwa Askofu Dr. Malasusa

Kilichokataliwa katika Biblia Takatifu ni "ULEVI"

ULEVI hata wa Chakula kingi ni dhambi kabisa kama ilivyo Uzinzi, Wizi n.k

Unaweza kunionesha mstari wowote katika biblia unaokataza POMBE?
Hata kama hakuna mstari ndani ya biblia uliokataza pombe,lkn kwa Askofu kukiri na kuhalalisha unywaji pombe,huko ni kupotoka na anatufanya tuwe na shaka na uaskofu wake,mimi ni mlutheri na ametuangusha kwa kweli
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Umenyoosha vizuri,kwa kweli Malasusa hapo amepotoka na anapaswa kutubu na kujivua uaskofu
 
Chanzo ni mwanahalisi mwanahalisi lilishapoteza sifa kwani haliaminiki toka lilipojaribu kumsafisha lowasa wakati kipindi cha nyuma likijisifu kuwa gazeti pekee lenye uthubutu was kuandika madhambi yake
 
Back
Top Bottom