KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Juzi nilialikwa kwenye. Misa moja huko shinyanga,ilikuwa ikifanyikia nyumbani kwa mtu! Basi baada ya Misa ukawadia wasaa wa misosi na vinywaji,baada ya mlo vijana wakaanza kusambaza vinywaji mchanganyiko,pale mbele kwenye meza kuu alikuwepo padri,zikapelekwa kreti mbili za bia,padri akafunuliwa chupa ya Safari lager! Akaipiga paaaaap!! Ikabaki nusu! Akairudia tena paaap!! Ikawa empty!! Jamaa aliyeandaa Misa hiyo akanniita nikajumuike nao hapo mbele nikamwambia tu asante mkuu!!japo nnnnilikuwa natamani ila nisingekuwa comfortable kuchapa kinywaji na mtumishi wa Mungu.
Achaga ushamba msukuma. Ungeenda kukata kiu. Pombe sio mbaya ikitumiwa kwa kiasi. Hata waislamu wanalijua hilo
 
Ni mawazo yako binafsi kwa sababu sicho mistari husika inachosema. Hakuna mahali mstari umesema Yesu alikuwa Mlevi. Mstari uko wazi kuwa ni mafarisayo ndio walimsingizia ulevi. Na hilo halikuwa jambo pekee walilomsingizia. Walishamsingizia uchawi kuwa anatumia mkuu wa pepo kutoa pepo kama ninavyomnukuu hapa:

"Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? "

Kwa hiyo kama masingizio ya Mafarisayo ndiyo msingi wako wa kusema Yesu alikuwa mlevi then inabidi kwa mantiki hiyo hiyo ukubali kuwa Yesu alikuwa mshirikina. Maana ni Mafarisayo haohao waliosema hayo.

Kama mafarisayo hawaaminiki katika hili la Beelzebub wanaaminikaje katika hilo la ulevi/unyaji pombe?

Mimi hilo andiko halinisumbui wala kunishangaza hata kidogo!

Kwa nini Mafarisayo walimsingizia Yeye kuwa ni Mlevi na sio Yohana?
 
Hata kama Mungu angeruhusu bado Pombe ni mbaya. Kabla ya kuinywa akili zinakua timamu ukishalewa unajikojolea hovyo na matusi kibao. Pombe mbaya na haifai acheni kujifariji. Hakuna maandiko yanayokataza kunywa sumu lakini mbona hunywi? Vitu vingine havifai by nature...

Hakuna kisichofaa by nature, Mungu aliumba kila kitu kwenye ubora wake na kwa jinsi yake hivyo aliona kila kitu ni chema alivibariki na kuvitukuza

Kiasili sumu sio kitu cha kula, lakini sumu ni njema kwa jinsi yake, KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA
 
Tusipende kujustify unywaji pombe kwa reasoning nyepesi hivyo........

Pombe ni haramu na hakuna lugha yoyote utakayoitumia kuihalalisha kuwa ni halali....

Ni vyema Maaskofu hao 2 wakaamua kwa hiyari yao wenyewe kulihama kanisa la KKKT na kuhamia kanisa la mzee wa upako, ili waweze kumjoin huyo Askofu mwenzao katika kupata ile kitu inaitwa bapa.........

Luka 7:33-34
 
Aliitwa anatoa pepo kwa beelzebub kwa sababu alikuwa mganga wa kienyeji

Umeelewa kitu hapo?

"Wakati ule akaletewa mtu mwenye pepo, kipofu, naye ni bubu; akamponya, hata yule bubu akanena na kuona. Makutano wote wakashangaa, wakasema, Huyu siye mwana wa Daudi? Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo"

Usitunge vitu mkuu, Hakuna andiko linalosema Yesu alikuwa Mganga wa Kienyeji,
Hoja hapo ni je Yesu alikuwa anatoa pepo?,
jibu ni ndio na ndio wakaanza kumpa majina kuwa huyu anatoa pepo kwa nguvu ya shetani

Swali la pili, Je Yesu alikuwa anakunywa Pombe?
Jibu ni ndio na ndio wakaanza kumpa jina la MLEVI

Inawezekana majina aliyopewa yote sio sahihi, hilo la kiwa anatumia Belzebuli na hilo la ULEVI, lakini hayo majina yametokana na matendo aliyokuwa anafanya
 
Hata kama hakuna mstari ndani ya biblia uliokataza pombe,lkn kwa Askofu kukiri na kuhalalisha unywaji pombe,huko ni kupotoka na anatufanya tuwe na shaka na uaskofu wake,mimi ni mlutheri na ametuangusha kwa kweli
Wewe ulimsikia akikiri na kuhalalisha?
 
Kaka hebu elewa basi, Yesu aliitwa na alijiita majina mengi mno, mengi yalikuwa ya maana na machache aliitwa kwa minajili ya kudharaurishwa
1: Mwana wa Seremala (watu walimwita)
2: Mwana wa Adam (Yeye alijiita)
3: Mwana wa Mungu (yeye na Wengine walimwita)
4: Mfalme wa Wayahudi (Watu walimwita)
5: Mlevi (watu walimwita)
6: Mzabibu (yeye alijiita)
7: Nuru ya Ulimwengu (yeye alijiita)
8: Bwana wa Sabato (yeye alijiita)
9: Maji ya Uzima (yeye alijiita)
10: nk nk nk

YESU ALIITWA MLEVI KWA SABABU ALIKUWA ANAKUNYWA POMBE, sasa usichokielewa hapo ni nini?
Hebu kariri hili ALIITWA
Kumbuka sio kila mtu anaekula chakula ni mlafi
 
Kimuingiacho mtu si haramu bali kimtokacho. Umekunywa pombe ukalewa ukaanza tukana watu dhambi iyo.
Ndo maana tunashauriwa kufanya kitu kwa kiasi, kama kula, kunywa n.k
 
Unaonekana kuwa na uelewa mdogo au bifu kwa Askofu Dr. Malasusa

Kilichokataliwa katika Biblia Takatifu ni "ULEVI"

ULEVI hata wa Chakula kingi ni dhambi kabisa kama ilivyo Uzinzi, Wizi n.k

Unaweza kunionesha mstari wowote katika biblia unaokataza POMBE?
Yesu aliwapiga watu pombe ya kutosha kwenye harusi....
Afu akapiga wine ya kutosha tu na wanafunzi wake kabla hajapewa kichapo na kutundikwa msalabani
 
Mkuu huwezi tumia tamko la mtu mmoja au wawili ku generalize kwamba kanisa limebariki unywaji wa pombe, halaf pia huwezi tumia mijadala ya kwenye vikao kuweka consensus yako kwamba ni kanisa limesema.
 
Tusipende kujustify unywaji pombe kwa reasoning nyepesi hivyo........

Pombe ni haramu na hakuna lugha yoyote utakayoitumia kuihalalisha kuwa ni halali....

Ni vyema Maaskofu hao 2 wakaamua kwa hiyari yao wenyewe kulihama kanisa la KKKT na kuhamia kanisa la mzee wa upako, ili waweze kumjoin huyo Askofu mwenzao katika kupata ile kitu inaitwa bapa.........
Pombe ni haramu kwako kwa imani yako (ambayo hujaiweka wazi) lakini kwa Waluteri hakuna mahali palipo sema Pombe ni haramu ila inasemwa Ulevi ni dhambi.
Sasa jee kwa uelewa wako Pombe ndio ulevi?
 
Walutheri pombe hunyweka kama kawaida hakuna katazo wala fundisho la unywaji pombe.Wasiokunywa pombe ni wapentekoste,akitokea kiongozi wa madhehebu ya kipentekoste anashadidia unywaji pombe jamii ya wakristo wa kipentekoste watashangaa sana juu ya fundisho la kunywa pombe.
Si kweli
 
Back
Top Bottom