KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Baba Askofu yupo sahihi Bosi wangu,On a jinsi Biblia inavyoruhusu Pombe/Mvinyo-Mhubiri 9:7-"Wewe enenda zako,ule chakula chako kwa furaha,unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka,kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubari kazi zako".

Kwa logic yako ya kuchukua mstari na kuutumia imediately bila kuangalia sheria za utafsiri itakuwa ni majanga kabisa. Ina maana ukikutana na mstari kama huu inabidi uanze kuandika mirathi kabisa

"Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana MUNGU. (Eze 28:10)"

Biblia imeandikwa kwa mikono ya wanadamu na lugha za wanadamu chini ya usimamizi wa Roho Mtakatifu. Kwa maana hiyo basi lazima sheria za kutafsiri maandiko zifuatwe na sio kwenda kiupofu. Biblia ina namna za uandishi mbalimbali (Ushairi, Mifano, Unabii, n.k.) na kila aina ina namna za utafsiri wake.

Nisisitize tena kama utachagua tu mstari na kuufuata unavyosema bila kujali kanuni za kutafsiri Maandiko basi hata huu mstari wa 8 nao utasema kila Mkristo anatakiwa kuvaa hivi "Mavazi yako na yawe meupe sikuzote; wala kichwa chako kisikose marhamu."

kama tutakubaliana na mstari wa 7 basi tukubali kuwa hatukupaswa kuvaa mavazi yeyote ila meupe n marhamu hayakupaswa kukauka mwilini mwetu.
 
Otorong'ong'o ,
Kwanza ujue sina mpango wa kubadili mtu anachoamua kuamini juu ya jambo lolote. Kwangu mimi jukumu langu ni kuusema ukweli na kila mtu aamue yeye mwenyewe. katika miaka yangu yote ya kusoma maandiko hakuna mahali nimekutana na andiko likiongelea vizuri kuhusu pombe na ulevi. Hakuna!
1. Baada ya kupona na gharika Nuhu alilewa akakaa uchi
2. Ajali nyingi sana na maamuzi ya kijinga yanatokana na Pombe.

Najua argument yako ni pombe sio mbaya bali ulevi. Ulevi unatokana na kunywa pombe. Unasema kunywa kiasi si dhambi. Bahati mbaya Biblia haijasema hivyo na hakuna kipimi cha kiasi. Je Mungu akiwa anahukumu siku hiyo atatumia kipimo gani kujua nilipita "kiasi"? Kiasi ni kipi na ni kwa andiko gani? Ulevi ni dhambi iwe wa Chupa moja au nusu glasi.

Nimeomba maandiko yanayoruhusu kwa sababu ninajua hayapo. "Nabii" Tito wa posta naye alikuwa hivyo hivyo lakini pamoja na kuwa "nabii" naye alikosa andiko akaja na hilo hilo.

Tim 5:23 hairuhusu Pombe kwa maana ya Safari Lager, John Walker, Vodka au Sijui nini Wine. Inaruhusu Tomotheo kunywa Mvinyo kama sehemu ya dawa. Na leo tuna dawa nyingi tu zenye pombe ndani yake. Lakini hatunywi kujitafutia furaha humo, la Hasha! Tunakunywa kama dawa kama ilivyokuwa kwa Tim.

Hiyo ya Yesu hata sio ushahidi. Neno la Kigiriki lililotumika ni ambiguous kwa maana linaweza kumaanisha Divai au Mvinyo. Hatujui ni aina gani ya Divai Yesu alitengeneza kutoka katika mstari huu.

Kwa kuongezea tu Mungu anawazaje juu ya Pombe hebu tazama mistari hii:
Walawi 10:8-9 - "Kisha Bwana akanena na Haruni, na kumwambia, Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;

Hesabu 6:3 - [Mnadhiri] atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.

Waamuzi 13:4 - [Mama yake Samsoni] Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

Isaya 5:11 - Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!

Isaya 5:22 - Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;

Mingine iko kwenye Biblia yako utaipitia!

Ukweli ni kwamba kitu pekee ambacho kinawafanya watu wapende Pombe ni sawa kabisa na kile kinawafanya wengine wavute sigara au madawa ya kulevya. Nacho ni kutafuta furaha na kutosheka. Mungu anaichukia Pombe kwa sababu anataka furaha na uteshelevu wetu uwe kwake. Ndio maana andiko kama alilonukuu FaizaFoxy la Waefeso 5:18 linasema tulewe Roho Mtakatifu. Kwa maana nyingine furaha yetu inapaswa kuwa ndani ya Roho Mtakatifu na ili ujazwe na Roho Mtakatifu lazima Utubu dhambi zako ikiwemo ulevi na Kuulilia msaada na msamaha alioununua Kristo katika Msalaba wa Kalvari!

Unaweza kuutete unywaji wa pombe aka ulevi kwa nguvu zote, na ni haki yako kufanya hivyo wala sitakuzuia. Ila nikualike kwa Yesu Kristo ambaye kwake kuna pumziko na raha ya moyo ambayo walevi, wavuta unga na wengineo wanaitafuta kwa gharama hata ya maisha yao.

Ukijazwa na Roho Mtakatifu hutahitaji pombe tena.

Kumbuka kila mlevi chakari alianza kidogo kidogo. Hakuna mlevi alianza na chupa kumi!

Shalom!
Mkuu naweza kuleta mistari inayokataza kula nguruwe kutoka agano la kale ....je unakubali kula nguruwe ni haramu? Unajua hata kutahiri ilikuwa amri si hiyari? Acha kunukuu vifungu bila kujifunza kusudio la Mungu kwa mwanadamu na jinsi alivyotengeneza mpango wa wokovu baada ya uasi wa Adamu. Ukitaka kuelewa vyema soma na vifungu vya agano jipya vinavyogusia Pombe na ulevi. Kasome 1Timotheo 1-9 then tafakari vyema. Usisome ukiwa umejaa roho ya kupinga bali kuelewa.
 
Kaka nyie (Walokole/ Wasabato) huwa mna matatizo sana kwwnye maandiko matakatifu, Wakatoliki wamekaa na hiyo Biblia mamia ya miaka kabla hayo madhehebu yenu hayaja anzishwa,
Umeona kuna sehemu nimetaja dhehebu langu au la mtu yeyote? Je kushambulia wenzio unaojadiliana nao ni sehemu ya kujua Biblia au ni sehemu ya kuonyesha arrogance kuwa wengine si malikitu?

Wakatoliki wanaijua sana hiyo Biblia na hawachagui kitabu cha kusoma ndani ya hiyo Biblia
Jifunze kwenda na hoja za mtoa hoja. Whether Wakatoliki (au watu wengine wowote) wanaijua sana Biblia au la hilo ni irrelevant kwa argument nilizotoa ambazo zinatoka katika Biblia.

Kama unaijua sana Biblia tulitarajia uwe mnyenyekevu kwenye majibu yako kama 1Pet 3:15 inavyofundisha. Na sio kuanza kushambulia wengine kwa namna uliyoanza nayo. Arrogance sio tabia ya kikristo bali unyenyekevu.

Hebu tusome andiko la Luka 7:33-34,
" kwa Yohana alikuja hali Mkate wala anywi mvinyo, wakasema ana mapepo, Mwana wa Adamu (Yesu) amekuja AKILA NA KUNYWA, wakasema ni mlafi na MLEVI rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi"

Swali, Yohana alikuwa ANYWI NINI mpaka waseme ana MAPEPO?, Na Yesu ALIKUWA ANAKUNYWA NINI mpaka waseme ni MLEVI?
Sasa sijui unauliza swali gani. Kwa sababu mstari huo uko wazi Yohana hakuwa anakunywa mvinyo. Wala huo mstari haujasema Yesu alikuwa akinywa nini. Maana kama unataka kusema Yesu alikuwa Mlevi maana yake unakubaliana na wenzio waliosema ulevi ni dhambi. Kama ni hivyo Yesu alikuwa na dhambi ya Ulevi anawakomboaje wenye dhambi wenzake?

Tunajua toka katika mistari mingine kuwa si hicho pekee walichomsingizia Yesu. Kuna kipindi walisema anatoa pepo kwa kutumia Beelzebub mkuu wa mapepo. Je nalo lilikuwa sawa kwa sababu walisema?

Kama ukiwa mkweli mstari huu hauoneshi kuwa Yesu alikunywa mvinyo achilia mbali kulewa. Infact unaonyesha kuwa mlevi wa mvinyo halikuwa jambo jema. Vinginevyo kwa nini iwe issue kama Yesu alikunywa au la kama halikuwa ni tatizo kwa mtakatifu kwa alivyowaambia siku zote kukitumia?
 
Ndugu kumbuka utasimama peki ako mbele ya hukumu na hutamwambi Mungu niliambiwa pombe si dhambi maana wao wanajua zaidi maadii ya Ukristo kuliko sisi kumbuka adam alivojitetea lakini aliadhibiwa so hata hawa viongozi wanaweza kukuangamiza bila kujua kila mtu anapaswa kujua kwa undani anachoamini kwa kusoma neno la Mungu, binafsi maana kila mtu atajibu yake so tujiongeze.Pombe ni dhambi maana ina kilevi na walev wote moton period.

Ni muda gani pombe inakuwa dhambi?? Kwa kunywa tu ndo dhambi au yatokanayo na kulewa ndo dhambi??
 
Mkuu naweza kuleta mistari inayokataza kula nguruwe kutoka agano la kale ....je unakubali kula nguruwe ni haramu? Unajua hata kutahiri ilikuwa amri si hiyari? Acha kunukuu vifungu bila kujifunza kusudio la Mungu kwa mwanadamu na jinsi alivyotengeneza mpango wa wokovu baada ya uasi wa Adamu. Ukitaka kuelewa vyema soma na vifungu vya agano jipya vinavyogusia Pombe na ulevi. Kasome 1Timotheo 1-9 then tafakari vyema. Usisome ukiwa umejaa roho ya kupinga bali kuelewa.
Kwa maana hiyo Amri kumi zime expire kwa kuwa ziko Agano la kale? Ukiambiwa Dunia ilitokea wapi utajibu kwa agano Jipya pekee?

Ukweli ni kuwa kujifunza tabia ya Mungu tunahitaji kujifunza toka Mwanzo mpaka ufunuo. Nadhani concern yako kama nimeielewa ni kuleta sheria juu ya Neema. Kama ni hivyo umeelewa vibaya. Ukisoma hilo bandiko halihusiani na Neema na Sheria bali tabia ya Mungu na kama ana approve hii kitu.

Suala la kula nguruwe halikuwa Amri kwa kila binadamu lakini Amri kumi ni kwa kila mtu. Hayo tuyaache kwa mnakasha mwingine. Nadhani utasoma tena bandiko langu ili upate kile hasa nililenga wasomaji wakipate.

Shalom!
 
Umeona kuna sehemu nimetaja dhehebu langu au la mtu yeyote? Je kushambulia wenzio unaojadiliana nao ni sehemu ya kujua Biblia au ni sehemu ya kuonyesha arrogance kuwa wengine si malikitu?

Jifunze kwenda na hoja za mtoa hoja. Whether Wakatoliki (au watu wengine wowote) wanaijua sana Biblia au la hilo ni irrelevant kwa argument nilizotoa ambazo zinatoka katika Biblia.

Kama unaijua sana Biblia tulitarajia uwe mnyenyekevu kwenye majibu yako kama 1Pet 3:15 inavyofundisha. Na sio kuanza kushambulia wengine kwa namna uliyoanza nayo. Arrogance sio tabia ya kikristo bali unyenyekevu.

Sasa sijui unauliza swali gani. Kwa sababu mstari huo uko wazi Yohana hakuwa anakunywa mvinyo. Wala huo mstari haujasema Yesu alikuwa akinywa nini. Maana kama unataka kusema Yesu alikuwa Mlevi maana yake unakubaliana na wenzio waliosema ulevi ni dhambi. Kama ni hivyo Yesu alikuwa na dhambi ya Ulevi anawakomboaje wenye dhambi wenzake?

Tunajua toka katika mistari mingine kuwa si hicho pekee walichomsingizia Yesu. Kuna kipindi walisema anatoa pepo kwa kutumia Beelzebub mkuu wa mapepo. Je nalo lilikuwa sawa kwa sababu walisema?

Kama ukiwa mkweli mstari huu hauoneshi kuwa Yesu alikunywa mvinyo achilia mbali kulewa. Infact unaonyesha kuwa mlevi wa mvinyo halikuwa jambo jema. Vinginevyo kwa nini iwe issue kama Yesu alikunywa au la kama halikuwa ni tatizo kwa mtakatifu kwa alivyowaambia siku zote kukitumia?

Ni kweli hujataja Dhehebu lako, lakini kwa kwenda kinyume na Wakatoliki ndio nimekuweka kwenye hilo kundi la Walokole ama Wasabato

Kaka hivi umesoma hilo Andiko?, wapi nimesema Yesu Mlevi, Yesu ANASEMA, WAKASEMA Yohana ana Mapepo, Yesu anasema. WAKASEMA yeye ni Mlevi

Aliyesema sio mimi bali hao anaowasema Yesu

Jipe muda wa kusoma Biblia kwa undani na mpe Roho Mtakatifu nafasi ya kukutafakarisha unayoyasoma
 
Hilo la madhehebu ya watu sio la msingi. Kuna mbingu moja na ni Ya Mungu Baba na Yesu anaandaa makao. Hayo madhehebu hayana mbingu ya kupeleka mtu kwa hiyo ni useless topic. Tubakie kwenye topic husika na Biblia. Inatosha!

Tukirudi kwenye mada, Ulichotaka kuonesha hapo katika bandiko lako nililonukuu ni nini hasa?
 
Kwa maana hiyo Amri kumi zime expire kwa kuwa ziko Agano la kale? Ukiambiwa Dunia ilitokea wapi utajibu kwa agano Jipya pekee?

Ukweli ni kuwa kujifunza tabia ya Mungu tunahitaji kujifunza toka Mwanzo mpaka ufunuo. Nadhani concern yako kama nimeielewa ni kuleta sheria juu ya Neema. Kama ni hivyo umeelewa vibaya. Ukisoma hilo bandiko halihusiani na Neema na Sheria bali tabia ya Mungu na kama ana approve hii kitu.

Suala la kula nguruwe halikuwa Amri kwa kila binadamu lakini Amri kumi ni kwa kila mtu. Hayo tuyaache kwa mnakasha mwingine. Nadhani utasoma tena bandiko langu ili upate kile hasa nililenga wasomaji wakipate.

Shalom!

Kaka unajichanganya vibaya sana, huwezi kusema kula Nguruwe lilikuwa ni agizo kwa wachache na Amri kumi ni kwa wote

Waliopewa Amri ya kutokula Nguruwe ndio haohao waliopewa Amri Kumi
 
Hilo la madhehebu ya watu sio la msingi. Kuna mbingu moja na ni Ya Mungu Baba na Yesu anaandaa makao. Hayo madhehebu hayana mbingu ya kupeleka mtu kwa hiyo ni useless topic. Tubakie kwenye topic husika na Biblia. Inatosha!

Tukirudi kwenye mada, Ulichotaka kuonesha hapo katika bandiko lako nililonukuu ni nini hasa?

Asante kwa kunielewa
 
Huku Bayern beer ni chakula hata wakati wa breakfast unapiga Weissen beer na Weiss wurst. Wakati wa kazi unaruhusiwa kwa siku beer chupa mbili.
Daaa....umenikumbusha mbali kaka. Nimepiga sn Berlina larger hapo Alexanda Platz
 
Kaka unajichanganya vibaya sana, huwezi kusema kula Nguruwe lilikuwa ni agizo kwa wachache na Amri kumi ni kwa wote

Waliopewa Amri ya kutokula Nguruwe ndio haohao waliopewa Amri Kumi
Hilo tuliache kwa sababu litaleta mada mpya juu ya mada. kukupa hint tu amri ya Usiue Ipo kitabu cha Mwanzo na sio kutoka. Na kipindi hicho hakukuwa na Musa wala Haruni.

Anyway tujikite na mada husika
 
Hebu tusome andiko la Luka 7:33-34,
" kwa Yohana alikuja hali Mkate wala anywi mvinyo, wakasema ana mapepo, Mwana wa Adamu (Yesu) amekuja AKILA NA KUNYWA, wakasema ni mlafi na MLEVI rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi"

Swali, Yohana alikuwa ANYWI NINI mpaka waseme ana MAPEPO?, Na Yesu ALIKUWA ANAKUNYWA NINI mpaka waseme ni MLEVI?

Asante kwa kunielewa
Wala sijakuelewa ulichomaanisha katika post yako na nimeinukuu hapo juu incase umeisahau. Ukitumia logic una imply kuwa kwa kuwa Yohana hakunywa mvinyo basi walisema ana mapepo. Hilo liko wazi mstari umesema wazi. Sehemu ya pili ni wazi unamaanisha Yesu likunywa Mvinyo ndio maana wakamwita mlevi.

Kama Yesu alikuwa mlevi anakuwaje mwokozi? Maana kulingana na Otorong'ong'o (sorry kama nimelikosea jina) ulevi ni dhambi na hivyo Yesu alikuwa na dhambi kama watu wengine wote na hivyo anakosa qualification ya kuwa Masihi!
 
Hilo tuliache kwa sababu litaleta mada mpya juu ya mada. kukupa hint tu amri ya Usiue Ipo kitabu cha Mwanzo na sio kutoka. Na kipindi hicho hakukuwa na Musa wala Haruni.

Anyway tujikite na mada husika
Swali hilo alilokuuliza linaumuhimu maana ni kama unaonesha double standards..
 
Hilo tuliache kwa sababu litaleta mada mpya juu ya mada. kukupa hint tu amri ya Usiue Ipo kitabu cha Mwanzo na sio kutoka. Na kipindi hicho hakukuwa na Musa wala Haruni.

Anyway tujikite na mada husika

Sio Usiue tu, hata usizini, usitamani mke wa mwenzio nk, zilikuwepo kabla ya Musa na Aroon

Kwa kweli hiyo ni mada nyingine, tukijite kwenye hii mada ya Malasusa

Kiufupi Biblia imekataza Ulevi na hata Ulafi, lakini sio unywaji wa Pombe, Sisi kama Wakristo pamoja na kusoma vitabu vya Kihistoria na vya manabii mbalimbali vilivyomo ndani ya Biblia, lakini msingi wetu Mkubwa upo kwa Bwana wetu Yesu Kristo, yeye ndio Manabii, yeye ndio Sheria, yeye ndio Ufunuo na yeye ndio injili iliyokamilika

Kwenye issue ya Pombe, yeye Yesu aliitengeneza na kuinywa pale kwenye Harusi ya Kana

Pia kwenye injili ya Luka 7:33-34, inaonyesha Yesu alikuwa ni mtumiaji mzuri wa kileo na sio kwa kujificha bali hadharani ambako kila mtu alikuwa anaona

So sijaona huyo Malasusa alipokosea kusema pombe haina shida kuitumia
 
Wala sijakuelewa ulichomaanisha katika post yako na nimeinukuu hapo juu incase umeisahau.
Swala la kuelewa au kutokuelewa ni wewe na utashi wako...Hujui unaweza pia kuamua kutokuelewa..?? Yes! Unaweza kuamua..

Ukitumia logic
Logic gani..?

una imply kuwa kwa kuwa Yohana hakunywa mvinyo basi walisema ana mapepo.
Yesu, ametumia mfano huo kuonesha unafiki wa Mafarisayo..Kwamba hawakosi la kuongea baya hata kama umetenda jema...

Hilo liko wazi mstari umesema wazi. Sehemu ya pili ni wazi unamaanisha Yesu likunywa Mvinyo ndio maana wakamwita mlevi.
Elewa Yesu katika kusema hayo alitaka kusisitiza nini hasa....

Kama Yesu alikuwa mlevi
Yesu hakuwa mlevi...Huo ulevi walimpachika Mafarisayo kwa unafiki wao....Yesu alikunywa mvinyo ila hakulewa....

anakuwaje mwokozi?
Inaelekea hujui kilichomleta Yesu hapa duniani...

Maana kulingana na Otorong'ong'o (sorry kama nimelikosea jina) ulevi ni dhambi na hivyo Yesu alikuwa na dhambi kama watu wengine wote na hivyo anakosa qualification ya kuwa Masihi!
Yes! Ulevi ni dhambi...Ila hakuna mahali Yesu alikunywa mpaka kalewa...Mbona unataka kumpakazia Yesu huku tunaona...?
 
Wala sijakuelewa ulichomaanisha katika post yako na nimeinukuu hapo juu incase umeisahau. Ukitumia logic una imply kuwa kwa kuwa Yohana hakunywa mvinyo basi walisema ana mapepo. Hilo liko wazi mstari umesema wazi. Sehemu ya pili ni wazi unamaanisha Yesu likunywa Mvinyo ndio maana wakamwita mlevi.

Kama Yesu alikuwa mlevi anakuwaje mwokozi? Maana kulingana na Otorong'ong'o (sorry kama nimelikosea jina) ulevi ni dhambi na hivyo Yesu alikuwa na dhambi kama watu wengine wote na hivyo anakosa qualification ya kuwa Masihi!

Kaka hebu elewa basi, Yesu aliitwa na alijiita majina mengi mno, mengi yalikuwa ya maana na machache aliitwa kwa minajili ya kudharaurishwa
1: Mwana wa Seremala (watu walimwita)
2: Mwana wa Adam (Yeye alijiita)
3: Mwana wa Mungu (yeye na Wengine walimwita)
4: Mfalme wa Wayahudi (Watu walimwita)
5: Mlevi (watu walimwita)
6: Mzabibu (yeye alijiita)
7: Nuru ya Ulimwengu (yeye alijiita)
8: Bwana wa Sabato (yeye alijiita)
9: Maji ya Uzima (yeye alijiita)
10: nk nk nk

YESU ALIITWA MLEVI KWA SABABU ALIKUWA ANAKUNYWA POMBE, sasa usichokielewa hapo ni nini?
Hebu kariri hili ALIITWA
 
Kwenye issue ya Pombe, yeye Yesu aliitengeneza na kuinywa pale kwenye Harusi ya Kana

Pia kwenye injili ya Luka 7:33-34, inaonyesha Yesu alikuwa ni mtumiaji mzuri wa kileo na sio kwa kujificha bali hadharani ambako kila mtu alikuwa anaona
itabaki kuyaheshimu kama maoni yako binafsi. Biblia haisemi hivyo na nimeshaandika kwenye post za nyuma kwa nini naamini hivyo. Basi kama kuna umuhimu wa kuendelea na mjadala huu ni vyema ukazipitia objection zangu na kuzijibu.

Cha msingi tu sijaribu hata kidogo kumbadili mtu mtazamo wake ila kuuweka ukweli wazi kwa takaye kuuona!
 
Swali hilo alilokuuliza linaumuhimu maana ni kama unaonesha double standards..
Double Standard zipi? Unataka tujadiliane kila kilicho ktk Biblia kwenye uzi mmoja inawezekana kweli?

Naona kama unashindana vile? Kama unatafuta ushindi au kuonesha kujua naomba nikupe vikombe vyote, vyote kabisa. Umeshinda na unajua sana ndugu yangu. Sidhani kama nina uwezo wa kujadiliana na mjuzi kama wewe.

Tafadhali usinirudie kama ulivyoahidi, usije kupasua ubongo wangu usioweza kuelewa elimu kuu uliyo nayo. Niwie radhi sana.
 
Back
Top Bottom