Kiwanja cha AVALON cinema: TIBAIJUKA acha unafiki

msipate taabu sana:

1. Babu mlalamishi ni huyo wa MWALIMU NYERERE FOUNDATION

2. Mlalamishi mwenzie ni Dr Dr HASSY KITINE ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa

Hivi ndivyo inavyotakiwa. Hamna haja ya kumung'unya maneno.

Amandla.....
 
Nadhani mna habari kuwa ile OPEN SPACE ya Avalon Cinema nacho kishapewa yule mzee aliyekuwa haishi kulalama kuwa serikali inakosa mwelekeo.

Yule Mzee ilikuwa sometimes mara 2 per day alikuwa haishi kuitisha press conference kutuambia maovu ya Serikali iliopo madarakani. Na kama siku hajaita yeye basi wanapeana zamu na mwenzie aliyekuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (ambaye naye alienda kulia apewe nyumba ya serikali 1) Masaki 2) kwa bei ya kutupa) na of course alipewa na shukran yake ilikuwa kuitisha mikutano pale Gymkana kumkandia huyo huyo aliyetoa ruksa apewe nyumba at the expense of Tax payers.(Ohh how can we forget lile benzi aliloagiza Ujerumani na baada ya kugundua kuwa Mwalimu keshapewa umbea, huyu mkurugenzi mstaafu akaamua kulitumbukiza baharini ili mwalimu asionyeshwe ushaidi !!!!

Sasa Mama Tibaijuka tunakuomba uache unafiki wa ku pick and chose battles zako ambazo unaonekana huna strategist wa kukusaidia mbinu za kivita.

Kama kweli unataka tukuone wa maana toa Tamko kuhusu AVALON kama kesho hatujaona babu anaakuja na tathmini ya uchaguzi

TATIZO LA TIBAIJUKA AMEZUNGUKWA NA MAFISADI HUSUSAN MKURUGENZI WA MIPANGO MIJI HAPO WIZARANI BIBI ALBINA BURRA
SOMA THREAD HII
Mwenyekiti tume ya lukuvi naye ni fisadi wa masuala ya ardhi

Wiki iliyopita Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam Mhe William Lukuvi alivamia ofisi za kitengo cha ardhi katika Manispaa ya Kinondoni na kuamuru Mkuu wa kitengo hicho kuwekwa rumande baada ya kutoridhishwa kuhusu maelezo yake kuhusu uuzaji wa viwanja va wazi hapa Jijini. Aliagiza pia milango ya ofisi hiyo pamoja na zile za Manispaa ya Ilala na Temeke kufungwa katika kile kinachodaiwa kuzuia watumishi husika kupoteza ushahidi wa vitendo vya uuzajji maeneo yaliyo wazi na ufisadi mwingine wa ardhi.
Mkuu wa Mkoa pia aliunda Tume ya watu 7 (saba) kufanya ukaguzi na kubaini vitendo vya kugushi na ufisadi mwingione unaohusu masuala ya ardhi katika Manispaa zote tatu. Tume hiyo inaongozwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Albina Burra.

Jina la Bibi Albina Burra sio geni masikioni mwa wakazi wa Kata ya Kibamba hususan Mitaa ya Luguruni, Kwembe Kati n.k katika Manispaa ya Kinondoni. Kati 2007 hadi sasa Bibi A Burra na timu ya wataaamu kutoka Wizara ya Ardhi walitenda ufisadi mkubwa sana wa ardhi kupitia Mradi wa uendelezaji wa maeneo yaliyoko pemebezoni mwa Jiji la Dar es Salaam (Luguruni Satellite City) ambapo fedha nyingi sana za serikali zimefujwa kwa njia za ulipaji fidia hewa, watumishi kulipwa posho na masurufu kana kwamba wanasafiri mikoani ilihali wanakwenda kufanya kazi hapa hapa jijini n.k. Inahofiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 3 (Tatu) za Serikali zilifujwa.

Chini wake wanakaya 259 waliokuwa wakiishi eneo la Luguruni walilipwa fidia kwa kutumia fedha na hundi za Serikali pasipo kuwa wamefanyiwa uthamini wowote wa mali zao, na kasha kutakiwa kuhama kupisha utekelezaji wa mradi huo ndani ya siku 30 tu. Sheria ya Ardhi Namba 4 na % za 1999 zinataka mwanachi kupatiwa notisi ya siku 90 endapo anatakiwa kuhama kutoka katika ardhi/makazi yake. Hivyo kwa kuwapatia wakazi hao notisi ys siku 30 tu Bibi A Burra na timu yake walienga kuficha ubadhirifu wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ulipaji fidia wakazi hao.

Kati ya wananchi hao wapo wachache waliotumiwa na watumishi wa Wizara ya Ardhi chini ya Bibi A Burra kuchukua fedha nyingi sana za fidia wakidai kuwa wanamiliki majengo yenye thamani ilihali ukweli ni kwamba walikuwa wakimiliki vibanda vya nyasi tu. Aidha watumishi waliokuwa chini ya Bibi A Burra walichukua picha za majengo mbali mbali na kuzitumia ckuchota fedha za fidia katika viwanja vitupu na fedha zote hizi kuishia mifukoni mwa watumishi wasio waaminifu wa Wizara ya Ardhi waliokuwa chini ya Bibi Albina Burra.

Bibi A Burra na timu yake waliwalipa wakazi wa Luguruni fedha kidogo sana takribani Shilingi 300 kwa Mita Moja ya Mraba ya Ardhi mwaka 2007. Malalamiko makubwa ya wanachi yalimfanya Waziri wa Ardhi wa wakati huo Mhe John Magufuli kutembelea eneo la Luguruni na kuagiza uchunguzi kufanyika na akamkabidhi mwakilishi wa Kamanda Tibaigana orodha ya walipwaji fidia wote kwa uchunguzi zaidi.

Kuhamishwa kwa Waziri Magufuli kutoka Wizara ya Ardhi kuliwapatia nafuu Bibi Albina Burra na timu yake ya watumishi wasio waaminifu. Baadaye mwaka 2008 (zaidi ya miezi 9 kutokea wakazi wa Luguruni kupatiwa malipo bila ya kufanyiwa uthamini wa mali zao ) Serikali ililazimika kuingia gharama upya za kulipwa watumishi, magari na posho ili kufanya uthamini wa mali za wakazi wa Luguruni na hatimaye kuwalipa fidia kwa kiwango kipya cha Shilingi 1800 kwa Mita Moja Mraba; ikiwa ni 600% ya kiwango kilichotumika awali.

Kwa maneno mengine kwa kitendo cha Bibi Albina Burra na timu yake kuwataka wana kaya 259 wa eneo la Luguruni wahame kutoka katika makazi yao ndani ya siku 30 tu huku wakiwa wamewalipa fidia pungufu kwa kiwango cha 600% kilikuwa na cha wizi na ubadhirifu na ufisadi kwa kuwa laiti wakazi hawa wangekubali kuhama kimya kimya kama wafanyavyo wanachi wengi wangepoteza ya fidia kwa kiwango cha 600%.

Hadi sasa hakuna hata mtumishi mmoja wa mradi huu aliyechukuliwa hatua zozote za kinidhamu wala kisheria kwa kuisababishia serikali hasara kwa kulazimika kurudia zoezi la uthamini upya.

Licha ya kiwango cha fidia kuongezwa bado kiliendelea kuwa kidogo sana na kuwatumbukiza wakazi hao katika lindi la Umaskini, wengi wao walilazimika kwenda kuishi maisha duni katika maeneo yasiyipimwa na yasiyo na huduma za kijamii kama vile maji, shule, n.k. Baadaye 2009 Wizara ya Ardhi iliuza ardhi iliyotwaa kutoka kwa wananchi hao pasipo maendelezo yoyote kwa bei ya kati ya Shilingi 25,000/= hadi 30,000/= kwa Mita Moja Mraba. Huu ni ufisadi mkubwa kuwahi kutekelezwa na watumishi wa Serikali kwa jina na mgongo wa Serikali na uliratibiwa na Bibi Albina Burra.

Baada ya kumaliza ufisadi katika eneo la Luguruni, timu hiyo ikawageukia wananchi wa eneo la Kwembe Kati na kuwanyang’anya ardhi yao kwa kisingizo kuwa wanapitisha miundo mbinu na kuwalipa fidia kidogo sana kwa kiwango cha Shilingi 1800 kwa Mita Moja Mraba. Baada ya hapo Timu ya Bibi A Burra ikapima viwanja katika ardhi na makzi ya wananchi wa Kwembe Kati pasipo kujali Master Plan iliyokuwepo, hati miliki zilizokuwepo n.k Na kasha kuwauzia wananchi hao ardhi hiyo hiyo pasipo maendeleo yoyote kwa kiwango cha Shilingi 6500 kwa Mita Moja Mraba.

Katika upimaji viwanja eneo la Kwembe Kati timu ya Bibi Albina Burra (Mkurugenzi wa Miapngo Miji Wizara ya Ardhi) walitenganisha nyumba za wakazi wa Kwembe Kati na visima vyao vya maji, maegesho ya magari, mabanda ya mifugo na hata vyoo. Huu ndio utendaji wa Mkurugenzi wa Mipango Miji anayetarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Lukuvi!!!!!

Kutokana na utendaji wa ubabaishaji wa Bibi Albina Burra na timu yake Serikali imelazimika kusimamisha utekelezaji wa miradi ya Luguruni na Kwembe hadi hapo mapungufu yaliyojitokeza yatakaporekebishwa; hali hii itaiingiza hahsara kubwa Serikali kutokana na kazi za marudio.

Kwa upande wa Mradi wa Luguruni tarehe 21 Mei 2010 Serikali ililazimika kutangaza kutafuta Mshauri Mwelekezi ambaye pamoja na mambo mengine atatayarisha Mater Plan ya eneo husika. Hii ikiashiria kuwa Mkurugenzi Mipango Miji wa wizara ameshindwa kutayarisha “a workable Master Plan” .

Kwa upande wa Kwembe Kati Serikali inafanya uchunguzi wa kina kuhusu madai makubwa ya ufisadi uliojitokeza.

Hivyo kuwepo kwa Bibi Albina Burra ndani ya Tume ya Lukuvi kutawasaidia zaidi maafisa wanaotuhumiwa kuliko Serikali na Wananchi wake kwa kuwa ni mtu ambaye ana tabia ya kupotosha ukweli, hivyo atatumia nafasi yake kama mtaalamu wa Mipango Miji kuwapotosha wajumbe wengine kwa nia kuwanusuru maafisa wanaotuhumiwa.
 
na pale drive in hapakuwa kweli eneo la wazi? Lakini sheria ya ardhi si imempa rais mamlaka ya kubadilisha matumizi ya ardhi? Hivi sio yeye ambaye anapelekewa maombi kupitia ardhi na kuyakubali kweli? Prof. Tiba usijekuwa unamshughulikia ali hassan mwinyi, mkapa na jk bila kujua!!

si ndio kazi ya jk kushughulikia maadui zake kwa kasi zaidi
 
msipate taabu sana:

1. Babu mlalamishi ni huyo wa MWALIMU NYERERE FOUNDATION

2. Mlalamishi mwenzie ni Dr Dr HASSY KITINE ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa

Huyo Namba 2 aliwahi kula njama na mkewe kuibia serikali (Wizara ya Afya) Dola 50,000 kwa ajili ya matibabu ya huyo mama ambaye hakuwa anaumwa chchote. Baadaye akamchomea utambi Mmiliki wa gazeti lililoibua kashfa hiyo kwamba siyo raia na Mkulu alikubaliana naye na mara moja akamvua uraia.
Nchi hii -- SINA HAMU!!!!!
 
Mbona ukisoma "between lines" wanafahamika kirahisi kabisa- tafakari.

Si wote wenye uwezo wa kutafakari kama wewe. Si wote tunaowajua waheshimiwa wa hapa nyumbani. Kwa hali hiyo hamna haja ya ambiguity wakati uwezo wa kuweka wazi upo. Kwa kuwataja, ametuweka wote kwenye kurasa moja.

Amandla....
 
msipate taabu sana:

1. Babu mlalamishi ni huyo wa MWALIMU NYERERE FOUNDATION

2. Mlalamishi mwenzie ni Dr Dr HASSY KITINE ambaye aliwahi kuwa mkurugenzi wa Usalama wa Taifa
Sawasawa,
Now you are talking. Mimi Hassy Kitine simfahamu. Lakini Butiku namfahamu. Nimekutana naye DSM mapema Novemba akanieleza kisa kizima cha malalamiko yake. Inaonekana Kikwete hakutaka hiyo Nyerere Foundation plan itekelezwe. Ni plan ya kujenga jengo la orofa 16. Hela zimeshapatikana na mjenzi ni Mchina. Ikulu ikaleta malalamiko eti ni karibu sana kwa usalama kwa sababu itakuwa na orofa 16. Butiku akasema mbona kuna jengo jengine upande wa Ocean Road je hilo si tishio kwa usalama? Akajibiwa kuwa eti litabomolewa. Anyway, to make the long story short ukapendekezwa huo uwanja wa Avalon wabadilishane na City council. Butiku akakubali na nadhani ujenzi unaanza early February. Jengo hilo litakapomalizika Nyerere Foundation itachukua 4 floors ambako makumbusho yote ya Mwalimu yatawekwa pamoja na ofisi za Foundation. Zilizobaki zitakodishwa na fedha hizo zitasaidia kuendesha foundation hiyo bila kutegemea tena misaada ya akina Museveni, Kagame na Mandela, ambao ndio wamekuwa wafadhili wakubwa. That is the plan as far as I know. Ilifikia hatua Kikwete anampigia simu Museveni aache kutoa fedha kwa foundation. But that is another story for another time.
 
Naomba kuthibitisha kuwa yale yalyoandikwa na Jasusi hapo juu. Yaani huyu Mkwere ana visasi sana!
 
Jasusi,

..ungependekeza kwa Butiku kuwe na Presidential Library ya Mwalimu chuo kikuu Dodoma, au Dar-Es-Salaam.

..hiyo ingeleta chachu kwa vijana wasomi kujifunza na kufaidika na kazi za waasisi wa taifa letu.

..jukumu la kuhifadhi kazi za Mwalimu lisiachiwe wasaidizi wake karibu tu. hii shughuli lazima iwe endelevu ndiyo maana napendekeza jukumu hilo lihamishiwe kwenye taasisi ya elimu ya juu.
 
Wow I'm speechless!.
 
jokaKuu,
Nadhani wanapanga kuweka library kwenye hilo jengo jipya. Sijui which is better: pale mjini au UDSM?
 
Lakini Butiku namfahamu. Nimekutana naye DSM mapema Novemba akanieleza kisa kizima cha malalamiko yake. Inaonekana Kikwete hakutaka hiyo Nyerere Foundation
Butiku alikwambia anataka uje ku publish hiyo michongo humu kwenye ma blog ili Kikwete amwone mnafiki?
 
Hapana.
Butiku hana habari na mambo ya JF wala nini. Umekerwa?
"hana habari na mambo ya JF" maana yake hajui kwamba kuna mjomba mmoja akipewa michongo ya faragha anakuja kuibandika humu kwenye ma blogu kwamba Butiku alimwambia ham-maindi Kikwete.

ambalo Butiku hajalisema hadharani usimsemee kwenye ma blogu
 
Naulizia pale nyuma ya ppf tower kuna mjengo umeamka kwenye kiwanja ambacho hakijawai kujengwa na mtu vipi pale? Je yalipo majengo ya tgo na voda pale ohio ni halali kujenga vibanda vile city centre?
 
Jasusi,

..ungependekeza kwa Butiku kuwe na Presidential Library ya Mwalimu chuo kikuu Dodoma, au Dar-Es-Salaam.

..hiyo ingeleta chachu kwa vijana wasomi kujifunza na kufaidika na kazi za waasisi wa taifa letu.

..jukumu la kuhifadhi kazi za Mwalimu lisiachiwe wasaidizi wake karibu tu. hii shughuli lazima iwe endelevu ndiyo maana napendekeza jukumu hilo lihamishiwe kwenye taasisi ya elimu ya juu.

Subutu, mkwere si ataichomelea mbali na tutapewa ripoti ya moto wa umeme!!!
The country's administration sucks!!!
 
BUTIKU: siku hizi kawa kimyaaaaa hata zile marathon za Press conference kaacha. Cha ajabu kupewa yeye na hiyo foundation yake anaona sawa, lakini wale ambao kawanyanganya kile kiwanja nao wakifanya Press Conference kuelezea alivyowafanyia uhuni atakubali?

Na si hivyo tuuu huyu huyu alitaka kuvamika kile kiwanja kingine lakini naona kule alikutana na wajanja zaidi yake wakawahi kumilikishwa hivyo alishindwa kwenda kulalama wavuliwe kama alivyofanya hiki cha Avalon Cinema.

Halafu mmeona ile michoro ya hilo jengo lenyewe la MNF? if anything ni litaingia kwenye listi ya majengo yanayoongoza kwa ubaya Dar, la kwanza likiwa lile mall lililo opposite na Seacliff Village.

KITINE: well huyu tangu apewe nyumba aliyokuwa analilia apewe (japo hakuwa mfanyakazi wa serikali) na baada ya kupewa aka demand apewe kwa bei ya Bure kule Masaki sasa naona kaacha naye kufanya Press Conference kwa ma elites (or whatever you wanna call them) wenzie pale Gymkhana Club.

Halafu TIBAIJUKA anatafuta wachawi...
 
Naulizia pale nyuma ya ppf tower kuna mjengo umeamka kwenye kiwanja ambacho hakijawai kujengwa na mtu vipi pale? Je yalipo majengo ya tgo na voda pale ohio ni halali kujenga vibanda vile city centre?

Mama MMANGA wa PSPF anafanya vitu vyake pale...kile hakina mgogoro
 
BUTIKU: siku hizi kawa kimyaaaaa hata zile marathon za Press conference kaacha. Cha ajabu kupewa yeye na hiyo foundation yake anaona sawa, lakini wale ambao kawanyanganya kile kiwanja nao wakifanya Press Conference kuelezea alivyowafanyia uhuni atakubali?

Na si hivyo tuuu huyu huyu alitaka kuvamika kile kiwanja kingine lakini naona kule alikutana na wajanja zaidi yake wakawahi kumilikishwa hivyo alishindwa kwenda kulalama wavuliwe kama alivyofanya hiki cha Avalon Cinema.

Halafu mmeona ile michoro ya hilo jengo lenyewe la MNF? if anything ni litaingia kwenye listi ya majengo yanayoongoza kwa ubaya Dar, la kwanza likiwa lile mall lililo opposite na Seacliff Village.

KITINE: well huyu tangu apewe nyumba aliyokuwa analilia apewe (japo hakuwa mfanyakazi wa serikali) na baada ya kupewa aka demand apewe kwa bei ya Bure kule Masaki sasa naona kaacha naye kufanya Press Conference kwa ma elites (or whatever you wanna call them) wenzie pale Gymkhana Club.

Halafu TIBAIJUKA anatafuta wachawi...
Sliding,
In defense of Butiku, hajakaa kimya. Ameugua for sometime ilibidi aende India kufanyiwa operesheni. Utamsikia tu muda muafaka. Kile kiwanja hakunyang'anywa mtu. Wamebadilishana na city council.
 
Back
Top Bottom