Kiwanda cha Tumbaki (TTPL) Morogoro Kufungwa?

Kiwanda cha Tumbaki (TTPL) Morogoro Kufungwa?

ya KAIZARI mpe Kaizari ya MUNGU mpe MUNGU... JP njema
 
Morogoro kuna kampuni mbili kubwa za tumbaku:
Alliance One and Tanzania Leaf Tobacco.
Ipi kati ya hizo inayoondoka?
 
Tabora huko watu wameuza tumbaku tangu mwezi wa nne hawajalipwa hadi wa leo, wengine tumbaku bado ipo nyumbani hawana uhakika wa kuuza tena
 
Kipindi cha nyuma,Enzi za Neema za JK hayo makampuni yalikuwa yanawalipa wakulima kwa dollar!
 
Wewe ni fala sana...Mh Rais ndio chanzo cha matatizo...suala la TTPL analijua vizuri narudia kusema pamoja na mazuri anayofanya hapa kaharibu sana
Kaharibu nini? Unataka wafanyebiashara bila kulipa kodi? Hapo haitawezekani kwenye awamu hii.
 
Hatari
Hapo Kuna Alliance One Na Philip Morris
Yaani Vinafungwa Na Wanaondoka Hivi Hivi
 
Morogoro kuna kampuni mbili kubwa za tumbaku:
Alliance One and Tanzania Leaf Tobacco.
Ipi kati ya hizo inayoondoka?
Nina uhakika wa Tanzania Leaf Tobacco kuwa wamekwishafunga, labda atabakia mfilisi kushughulikia na madeni
 
Wewe ni fala sana...Mh Rais ndio chanzo cha matatizo...suala la TTPL analijua vizuri narudia kusema pamoja na mazuri anayofanya hapa kaharibu sana
usitukane watu wewe hujui vizuri kuna watu wanaelewa kuzidi unavyofikiria tumia akili vizuri.
nimeshafanya kazi nao kwa zaidi ya miaka kumi.
ungejua walivyokuwa wanakwepa kodi usingewasupport.
waanzia toka kushusha thamani ya bei ya tumbaku kwenye export permit unajua hili? ili iwasaidie thamani ya bidhaa zao zionekane kuwa chini wapate kulipa kodi na gharama ndogo katika kuisafirisha.
ndo maana ulikuwa unaweza ukasikia tanzania tunadaiwa tumesafirisha tumbaku ya milion labda 40 wakati wanunuzi wanasema wamenunua tumbaku ya milion 500.
sasa kwa mazingira ya sasa huwezi cheza hivyo.
achilia mbali hawa walikuwa waagizaji wazuri wa farm inputs zinazowasaidia kuweka mzania wa export na import katika kodi kwamba wanaweza kutumia kuwa wameagiza bidhaa nyingi ili kumbe kidogo.
nisikueleze mengi kwa kuwa hata taratibu zilishabadilika sana tokea wakati wa Kikwete sema utekelezaji wa maana unaanza kuonekana sasa.
bora tutumie josho jingi wakati wa mazoezi kuliko kupoteza askali wengi kwenye vita.
lakini pia kumbuka na uelewe soko la tumbaku duniani pia limepungua wavutaji sigara wamepungua na kusababisha wanunuzi wakubwa kama philip moris british americaan tobacco kuhamia kwenye biashara zingine na hii unaweza kuona hata kwa kwetu vijana wanaovuta sigiara kati ya vijana 10 labda watatu ndio wanaovuta na mbaya zaidi kwa nchi zetu wale wenye kipato cha kati na kikubwa ambao wangepaswa kuwa walengwa ndo hawavuti kabisa.
 
sasa wanaondokaje bila kulipa? walipe kwanza azawais wawekwe ndani
 
Kama hawalipi kodi hakuna kuwalealea na waende tu..hao Alliance one walianza kama Dimon ni wakwepaji wa kodi wazuri sana na wanatumia vizuri ile sheria ya kodi ya miaka kumi..walianza kama Dimon walipoona miaka kumi ya kuoperate bila kodi imeisha wakasajili tena kampuni na kuiita Alliance one wakapata tena msamaha wa kodi kwa miaka kumi naona wamenogewa sasa hata baada ya muda wa msamaha wa kodi ya miaka kumi ilipoisha wameendelea kukwepa kodi..TTPL nao ndio walewale nchi haiwezi kuendeshwa kijanja janja namna hiyo kuna vitu vingine sio vya kumlaumu raisi kwa kusema sijui kabana..Hapana mwacheni afanye kazi japokuwa na yeye ana mapungufu yake mengi tu ila kwa upande wa pili wa shillingi anakula nao sahani moja wanaorudisha maendeleo nyuma
Nimekupata mkuu Ila kwenye hili hata Rais alionekana kutokubaliana na lilivyoshughulikiwa. Alilisemea siku ya uapishwaji wa mkuu mpya wa Moro . impact yake itakua kubwa
 
TTLC ndio najua wanaondoka na waliwapa mkataba wa mwaka mmoja wafanyakazi wao ambao unaisha hivi mapema, alliance one nao wanatimka?
 
Back
Top Bottom