Kiwanda cha Maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiwanda cha Maji

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by wimbi la mbele, Jan 6, 2011.

 1. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Forum nzuri hiii.

  Nauliza, mfano nataka nifungue kiwanda cha maji, yaani kufunga mashine mpya, madumu ya maji etc, bora ni ninunue mashine wapi? Mpya za China au used za ulaya?

  Je, kuna websites naweza kutembelea kuona kama naweza kupata mashine hizi?

  Je chupa itakuwaje?
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,201
  Likes Received: 4,084
  Trophy Points: 280
  Duuuu set nzima itakugharimu kama sh 100m hivi. Investment yake imesimama kidogo....hapo badp space na nyumba ya uzalishaji....machine zipo china ndio bei rahisi...machine 5 zinatakiwa ili uwe fit zaidi......

  Nakushauri kama unataka urahisi zaidi nenda kwa kiwanda cha A1 kinatengeneza maji ya MO Dewji..utapata nembo yako na utatengenezewa maji yako uyapelekee...sokoni
   
 3. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Budget yako kiasi gani?
   
 4. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  milioni 150 mpaka 200

  benki kuna mtu yuko tayarii kupitisha mkopo mwingine wa 50
   
 5. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  TZS 250m bado kiasi kidogo kama unataka kuanzisha kiwanda cha maji kwa ajili ya biashara.

  Kuanzisha kiwanda cha maji unahitaji kuwa na aina nne za machine ambazo ni mashine ya kusafishia maji, mashine ya kutengenezea chupa za maji, mashine ya kuwekea maji kwenye chupa na mashine ya kuwekea label. Gharama ya mashine (complete set and / with accessories) ex China au India au Taiwan hadi Dar-es-salaam pamoja na kodi ni kiasi cha TZS 355m.

  Mashine ya kusafishia maji (water purifying mashine) = 50m
  Mashine ya kutengenezea chupa za maji (bottle manufacturing machine) = 70m
  Mashine ya kuwekea maji kwenye chupa (purified water bottling machine) = 50m
  Mashine ya kuwekea label (labelling machine) = 7m
  Usafiri na bima (freight & insurance) = 35m
  Kodi (tax 67%) = 142m

  Hapo bado hujajumlisha gharama za kununulia au kukodisha eneo la kuweka kiwanda, malighafi, wafanyakazi / vibarua, gharama za kuendesha mitambo, gharama za maji na umeme, gharama za kujitangaza, usafiri na kadhalika.

  Start up cost ni kama TZS 500m, kwa kubana sana.
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  wasikutishe mpendwa. ukitoa gharama za banda na van, kama utaanza na chupa ndogondogo itabidi uwe na angalau dola 40,000 za kuanzia kwa mshine pekee, lakini kama ni chupa kubwa, hata dola 15,000 utapata mashine za kuanzia. na unaweza kuendelea kuexpand kidogokidogo hadi kufikia scale unayotaka. kwa kuwa umesema una 200m+ unaweza kuanza na chupa za ujazo mbalimbali. kuna mtu tumeishamsaidia na sasa kiwanda kinafanya kazi tayari, so we have practical experience. mashine tulinunua china. za ulaya hazikuwa na advantage, kuna mambo mengi oinabidi ufanye kama kupima aina ya maji kutoka kwenye chanzo chako (water analysis) na uwe na laboratory report ambayo itakuongoza kujua mitambo yako iwe ya technolojia gani nk pia ni vizuri mambo ya tbs na tfda uyazingatie. kuna mengi hapo ndugu. best wishez
   
 7. m

  maridadioh Member

  #7
  Mar 12, 2015
  Joined: Feb 19, 2015
  Messages: 48
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Mkuu naomba kujua icho kiwanda cha A1 kipo wapi au kama una contact zao naomba please
   
Loading...