Watumishi wa ardhi kukaa kituo kimoja cha kazi kwa miaka 20 sio sawa. Wao sio madiwani wahamishwe

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,278
2,040
Kwako Waziri wa Ardhi, Mh. Jerry Silaa. Pole sana na majukumu ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Bila kupepesa macho, chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi ni watendaji. Watendaji wanapokuwa wamekaa kituo kimoja kwa zaidi ya miaka 5, hutengeneza urafiki mkubwa na matapeli wa ardhi ili kufanikisha mambo yao.

Watendaji huwapa hao matapeli nyaraka mbalimbali za ardhi ili wazifanyie utapeli huo mitaani kwa watu mbalimbali.

Kama kweli Mh. Jerry Silaa unataka kujua kuhusika kwa watendaji wako katika huo utapeli, basi fanya maamuzi magumu ya kuwahamisha wote kama alivyofanya Mzee Lukuvi mwaka 2010 alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar alizifunga ofisi zote za ardhi manispaa na kuomba kibali cha kuwatanyawa mikoa na wilaya mbalimbali kwani kulikuwa na watendaji toka waajiriwe wana miaka 20 hawajawahi kuhamishwa utadhani ni madiwani. Ukweli alifanikiwa sana ktk zoezi lile madudu na uchafu mwingi uligundulika, wapo walioshtakiwa, wapo waliofukuzwa kazi na hali ya urendaji ktk manispaa za Dar es Salaam ilitulia kabisa.
 
Kuna mahakimu wa mahakama za ardhi hapa Dar es salaam, hao wamekaa hapa miaka zaidi ya 15, kinachofanywa ni kuwatoa Temeke, anaenda Ilala, Kinondoni anaenda Kigamboni, hawa wamesuka mfumo ambao unawafanya waachiane mafaili ya kesi. Hamisha wote hapo leta sura mpya

Ukienda mahakama za kawaida, hakimu hakai kituo kimoja zaidi ya miaka mitatu
 
Back
Top Bottom