SoC04 Kivipi mikopo itawainua watanzania hasa vijana na sio kuwa janga linalo sababisha maafa na kuaribu ndoto za wengi

Tanzania Tuitakayo competition threads

thefather

New Member
Dec 14, 2020
2
1
Mikopo rahisi na rafiki ni miongoni mwa njia bora kabisa inayo weza kuwainua watanzania wengi hasa vijana kwa kutoa fursa ya kupata mitaji na kuwezesha ndoto,ubunifu ,ujuzi na vipaji mbalimbali walivo navyo vijana hii itapelekea kupunguwa kwa wimbi kubwa la vijana wasio na ajira mitaani na kutengeneza tanzania bora kwa miaka mingi mbele.

Swali: Je sera na mifumo iliyopo ina wezesha utoaji wa mikopo salama na rafiki?

Jibu ni hapana.licha ya kuwepo kwa sheria mbali mbali kama vile B.O.T Act no 4 of 2006,Banking and financial institutions Act of 2016 na sheria nyingine pia miongozo mbali mbali kutoka benki kuu na wizara ya fedha lakini imeshindwa kukomesha mikopo kandamizi na vitendo visivyo vya haki na kinyume na sheria vinavyo fanywa na mashirika ya utoaji wa mikopo hali inayo pelekea mikopo badala ya kuwa mkombozi imegeuka na kuwa ndio chanzo kikubwa cha watu kujiua,kufilisi na kuzidisha umasikini.

Nini kifanyike ili kudhibiti taasisi zinazo jihusisha na utoaji wa mikopo kandamizi kinyume na sheria

1. Zitungwe sheria maalumu kwaajili ya kumlinda mteja na udhibiti wa riba kwenye mikopo.
Licha ya kuwepo kwa sheria kama B.O.T Act,BANKING AND FINANCIAL INSTITUTIONS ACT, na nyingine zinazo toa muongozo wa kumlinda mteja kwa taasisi za utoaji wa mikopo mfano section 49 of BANKING AND FINANCIAL INSTITUTIONS ACT OF 2016 imetoa muongozo wa juu ya ukopeshaji na ukusanyaji wa madeni lakini sheria hizi zimeacha mwanya na kuna hitajika sheria nyingine zitakazo kuja kutilia mkazo na kumlinda mteja (mlaji).
mfano USA wanazo sheria mbali mbali kama vile usury laws(hizi ni sheria zinazo dhibiti viwango vya riba kwenye mikopo isivuke kiwango kilicho wekwa),The Dodd-frank Act,Truth in lending Act(TILA),Federal Deposit insurance Act (FDI) na sheria nyingine ambazo zina walinda wateja na kudhibiti taasisi zinazo jihusisha na utoaji wa mikopo pamoja na mabenki kutofanya vitendo vya uongo,uonevu na vitendo visivyo vya haki kwa wateja.

2.
kuundwa kwa taasisi maalumu ya kusimamia na kulinda usalama na kaki za wateja wa mabenki na taasisi za utoaji wa mikopo;


Kuundwa kwa taasisi itakayo kuwa inapokea malalamiko na kero za wateja,kuzifanyia uchunguzi na kuzifikisha kwenye vyombo husika pia kutoa elimu kwa ujumla juu ya mikopo na mambo ya fedha pia taasisi hii iwe na ushirikiano wa karibu na benki kuu ili kurahisisha uchukuliwaji wa hatua kwa taasisi na mabenki yatakayo enda kinyume na utaratibu uliopo. mfano USA wanayo  Consumer financial protection bureau (CFPB) inayoshughulikia matatizo ,kero na shida pia kutoa elimu ya mambo ya fedha kwa wateja.

3. Kuundwa kwa mfumo wa kidigitali utakao dhibiti na kusimamia utoaji wa mikopo;
Benki kuu ndio ina dhamana ya kusimamia taasisi zote za fedha kama ilivyo elezwa kwenye section 6 of B.O.T Act of 2006 .basi kuwepo na mfumo wa kidigitali wa utoaji wa huduma ya mikopo kwenye taasisi ulio onganishwa moja kwa moja na benki kuu utakao kuwa una dhibiti viwango vya riba kwenye mikopo ili kuepusha uongezwaji wa riba nje na kiwango kilicho wekwa na benki kuu ambao ni kinyume na sheria na pia ndio umekuwa ukiwaumiza wateja pia mfumo huo utakuwa una peleka taarifa moja kwa moja na pia utarahisisha zoezi la ukaguzi

Kwa kudhibiti tasisi kandamizi za utoaji wa mikopo na kuweka mazingira rafiki ya mikopo kutaitoa nchi yetu katika janga kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini na maafa yanayo sababishwa na mikopo kandamizi.

Kwa nafasi hii naomba radhi kwa sehemu yoyote nitakayo kuwa nimekosea kwani lengo ni kuchangia mawazo katika ujenzi wa taifa letu.

Ahsante.

0742546327
Makavelidullah@gmail.com
Thefather
 
1. Zitungwe sheria maalumu kwaajili ya kumlinda mteja na udhibiti wa riba kwenye mikopo.

kuundwa kwa taasisi maalumu ya kusimamia na kulinda usalama na kaki za wateja wa mabenki na taasisi za utoaji wa mikopo

Kwa kudhibiti tasisi kandamizi za utoaji wa mikopo na kuweka mazingira rafiki ya mikopo kutaitoa nchi yetu katika janga kubwa la ukosefu wa ajira, umasikini na maafa yanayo sababishwa na mikopo kandamizi.
Katika point nyingi umezungumzia kumlinda mteja. Mteja yupi mwananchi au benki? Maana chini ya BOT walioko huko ni wateja wao kuanzia mabenki, watu hadi taasisi za mikopo😀

Kimsingi tu sheria ziwe za haki kuwalinda wote, wakopaji na wakopeshaji. Anayekopa alipe koasi stahiki na asiyelipa alipishwe kiwango stahiki na usumbufu pia alipie. Asipendelewe mtu wala asihurumiwe asiyetimiza upande wake. Tuwe makini kutoa HAKI
Screenshot_20240428-153845_Chrome.jpg


Kwa nafasi hii naomba radhi kwa sehemu yoyote nitakayo kuwa nimekosea kwani lengo ni kuchangia mawazo katika ujenzi wa taifa letu
Sie pia tunashukuru chief. Ahsante sana
 
Back
Top Bottom