Hii mada inatusaidia nini?Wanabodi,
Angalizo la uchangiaji: Kuna watu humu wana vijiba vya roho, akitokea mtu akapendeza wao wanakereka au akisifiwa wao wanakereka na kukasirika. Kama wewe ni mmoja wa kundi hili, nakuomba ushia hapa ili huko mbele usikereke.
Kufuatia mimi mwana jf mwenzenu umri wangu umesonga songa, nimefikia level ya kustaafu, hivyo nakuwa sina tena zile mada moto moto au maswali magumu magumu kama enzi zile kijana nikiendesha kipindi cha Kiti Moto.
Kufuatia neno "ukubwa dawa", mimi sasa ni mtu mzima hivyo napandisha mabandiko ya dawa kama bandiko hili.
Declaration of Understanding. Naomba kukiri, naaandikia kwa members wenye uwezo tofauti tofauti wa uelewa, hivyo ukikutana na bandiko langu ukajiona kama huelewi elewi, nakushauri jipitie zako tuu uendelee na safari yako, maana mabandiko mengine, nawaandikia watoto wa chekechea, wewe wa Ph.D utaishia chaka.
Leo naomba kutoa somo kuhusu mavazi fulani fulani, jee wajua mavazi yanazungumza?. Jee wajua dress code ni kiashiria cha the state of mind ya mvaaji na action anayoweza kufanya?.
Psychoanalysis: Je, wajua dress code ya mtu ina represent the soundness of his mind?
Salaam, Declaration of Interest. Hili ni bandiko kuhusu hypothetical situation tuu na sio any real situation, lunazungumzia a hypothetical being not a real being na halimlengi mtu yoyote specific kwa sababu jf ni home of great thinkers, great thinkers don't discuss people, they discuss ideas...www.jamiiforums.com
Mfano mtu akikukaribisha kwake ukaenda the way utakavyomkuta amevaa utajua amekuitia nini na ni nini kitafuatia.
Wenzetu wazungu wana dress code kabisa ya matukio mbalimbali, kwa matukio serious wana vaa formal dress, yaani kuiambia, na kwa matukio ya kawaida, wanavaa kawaida, yaani casual but smart, sisi wabongo hatuna any specific dress code kwa matukio serious na yale ya kawaida.
Pia aina ya mavazi ni kwa maeneo au matukio fulani, mfano ukienda beach, unavaa beach wear, ukienda church unavaa vazi la heshima na ukitoka out kama ni first date out, usually wadada they dress to kill!.
Leo nimemuona Mama kavaa Combat, kwa jinsi hiyo combat ilivyo mkaa, imemtoa kweli kweli na kumpendezea, hivyo Mama ametokelezea.
Kwa sisi wenye jicho la tatu, hiyo combat ya mama inaongea, only wenye jicho la tatu ndio wanaona, na wenye sikio la tatu ndio wanaweza kusikia hiyo dress code inaongea nini.
View attachment 2011474
Kwa vile macho hayafanani, na kwa vile hakuna taarifa zozote za mama kuwa mjeshi kabla, hivyo wale wenye macho ya kawaida tuu, wakiona hii picha ya amevaa combat, wao wanaona ni mtu tuu wa kawaida yule yule Mama Samia waliyemzoe ila tuu leo amebadilika kwa kuvaa sare za jeshi, lakini sisi wenye jicho la tatu, hatuoni sare tuu tunamuona mtu ambaye ni mjeshi kweli kabisa, ndani ya sare yake, ila kabla ya kuvaa sare za jeshi, hatukumjua, kuwa ni mjeshi mpaka alipovaa sare ya jeshi, kwa jinsi zilivyo mkaa, ndipo macho yetu yamefunguka, kuona na kubaini kumbe ni mjeshi kabisa!.
Zingatia tofauti kati ya mtu asiye mjeshi by nature na kuvaa sare za jeshi na mtu mjeshi by nature na kuvaa sare za jeshi. Asiye mjeshi by nature,
View attachment 2011725
kama huyu, akivaa sare za jeshi anakuwa amevaa tuu sare,
Lakini mtu mjeshi by nature, hata kama sio mwanajeshi, akivaa sare za jeshi, anakuwa ni mwake mwake!, huyu ni jeshi kama huyu
View attachment 2011739
Hata huyu Mzee wetu
Mwalimu Nyerere, alikuwa mjeshi.
View attachment 2011753
Naomba kutoa onyo kwa wale wenzangu na mimi waliozoea, rais ikitokea upande ule, wa ma ustaadhi, basi wanajiachia na kupanga kufanya au kuleta ile michezo michezo yao!. Kama hata baada ya kusoma hapa na kumjua ni mjeshi na kama wanaweza kumletea mchezomchezo mjeshi...endeleeni ila msilalamike kuwa hamkujua, au hamkuambiwa, mlidhani ni sare tuu za jeshi! hii ni taarifa kwenu kuwa sio sare tuu!, msithubutu, na mkithubutu, shauri yenu!. Mimi mwenzenu Paskali Mayalla, japo wengi humu mnanifahamu kama mwandishi tuu wa habari wa kujitegemea, wengi humu wasicho kijua kuhusu mimi, kabla ya uandishi wa habari nilikuwa mjeda from JKT straight to JWTZ!. Chezea vitu vingine vyote ila geshi, usichezee kabisa!. Chezea watu wengine wote, ila Wajeda usichezee kabisa. Kazi ya jeshi ni moja tuu... "zikimkosa mbili...utaandika maelezo"!.
Kwa wale wenzangu na mimi wasio na uwezo wa kuisikia sauti ya mavazi fulani, this is a very loud and clear signál she is a very serious person, she is no nonsense lady, sio mtu wa kuletea mchezo mchezo, hivyo huu ni ujumbe mzito loud and clear kwa wote wanaopanga kuleta au kufanya mambo yao ya ile michezo michezo yao ya ajabu ajabu, before they do, they better think twice, and if possible waache kabisa!. kama hapo mwanzo iliyokuwa "hapa kazi tuu" naona sasa kuna relaxation mood na laxity ya watu ku relax na kuanza kuleta tena ile michezo michezo..., hii dress code ya leo inaniambia ile slogan ya "hapa kazi tuu", inaendelea kwa "kazi iendelee".
Paskali
View attachment 2011746