Mkuu hebu iweke habari yako katika aya.Hili lilikuwa ni somo dogo katika Somo kubwa la Kiswahili darasa la tano.Maada iliitwa "UTUNGAJI",hapa unakutana na imla,kutunga sentensi n.k
Turudi kwenye hoja:Huwezi kuitikia mwito ambao umekiuka sheria au una utata kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Dsm,ambapo katika anuani ya bunge hainyoshi kuwa Mbowe ni Mkazi wa mji huo,hana "nguvu" ya kumuita Mbunge wa Jimbo la Hai,mkazi wa Hai,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,na Waziri Mkuu Kimvuli kama vile anamuita Wema Sepetu.
Huyu ni kiongozi,ni mbunge...na ukumbuke wakati anaitwa ilikuwa ni kipindi cha Bunge,hivyo mwito huo ulipaswa kuwa rasmi kupitia kiongozi wa bunge ambaye ni Spika.Huwezi kumuita "kienyeji" Mbunge na KUB ambaye ktk nchi za Jumuiya ya Madola huyu ni Waziri Mkuu Kimvuli,sauti ya upinzani na vyama mbadala ktk nchi.Jamani hamjui hata "Concept ya Political Pluralism" ktk nchi?
Huyu ni VIP...Ana diplomatic Pass...Huwezi kumuita kihuni huni kwa sbb ya "tuhuma tu".Yeye kuitikia mwito wako,ni kukubaliana na upuuzi wa uvunjaji wa taratibu ulioufanya.
Huyu Makonda madaraka yake mwisho daraja la mto Ruvu,ni uzuri wa teknolojia tu kwamba yale majina anayotangaza anatumia radio na Tv zilizofika mpaka Kalambo,Nkasi na Kibondo.Huyu ilitakiwa atangaze kupitia E-Fm na Praise Power Radio ambazo mawimbi yake yanaishia Mapinga Bagamoyo na Mlandizi-Kibaha.