Kiuhalisia Mbowe kakosea sana kutoripoti Polisi

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,438
32,248
Kwenye hili sakata la madawa ya kulevya kwa namna lilivyokuwa likiendeshwa na bwana Makonda ilikuwa ni nafasi nzur sana kwa yeye Mbowe kumuonesha Makonda hakuwa sahihi.

Hii ingetoa nafasi ya kujijengea imani kwa wapenzi wa UKAWA na CHADEMA ni kwa namna gani serikali inavyopambana na upinzani kuumaliza kwa kuwazushia mambo. Kitendo cha kutokwenda kinawaweka njia panda wapenzi wa CHADEMA kama anasingiziwa kiongozi wao au ni ukweli kulikuwa hakuna haja ya kutunishiana misuli baina yake na Makonda.

Mfano mzuri ni ndugu Gwajima kwa sasa anatembea kifua mbele na ataongea lolote bila hofu mana kapekuliwa kila kona na hajapatikana na hatia.

Kwanini akimbie ikiwa ni kiongozi mkubwa wa Kambi ya Upinzani? Hapa anatakiwa alimalize hili suala hata akisimama ktk majukwaa aongee bila kuacha viulizo kwa maana tayari atakuwa amewashinda na hili suala liende vizuri yafaa lisihusishwe na chama alikabili yeye mwenyewe.
 
Kama mapambano yenyewe tunamuhusisha MADABIDA aliyetuuzia arv feki! Bado tunaita shughuli ya kitaifa.......
Hongera sana mbowe kwa kujielewa na mpaka watume polisi hakuna kwenda!
Mkuu hatuwezi kwenda sawa na serikali yafaa kuwaonesha wao hawapo sahihi tukifanya hayo ina maana hakuna wa kumkosoa mwenzie hapo hamna maana ya upinzani
 
Hapo anampa ushindi makonda angalia gwajima kamgalagaza makonda kila kona

Wameshampelekea Summons??Commissioner kasema waliotajwa waende kwake na si Polisi.Hivyo wataitwa kwa heshima na watatoka support.

Mbowe yupo right amesimamia sheria.Anajua haki zake za msingi.Unaita watu Polisi kwa kutumia aka Binge,aka chumv,aka Kiboko utawapata??

Issue ilikuwa ya kisiasa na Commissioner amejua amesema mbele yake.Mbowe yuko right.Big up to Mbowe.
 
Kama mapambano yenyewe tunamuhusisha MADABIDA aliyetuuzia arv feki! Bado tunaita shughuli ya kitaifa.......
Hongera sana mbowe kwa kujielewa na mpaka watume polisi hakuna kwenda!
Hawa ni wanaccm wanao support chama cha Mauaji financially siyo rahisi kuguswa.

Hawa hata wakiua wataulizwa Umeya Mpinzani au RAIA wa kawaida.Na watatoka kwamba alikuwa anajiprotect.Hiyo ndiyo CCM. Wauza madawa watoto wa watawala hawajaguswa wameguswa watumiaji.Ajabu na kweli.
 
Kwenye hili sakata la madawa ya kulevya kwa namna lilivyokuwa likiendeshwa na bwana makonda ilikuwa ni nafasi nzur sana kwa yeye mbowe kumuonesha makonda hakuwa sahihi.
hii ingetoa nafasi ya kujijengea imani kwa wapenzi wa ukawa na chadema ni kwa namna gani serikali inavyopambana na upinzani kuumaliza kwa kuwazushia mambo kitendo cha kutokwenda kinawaweka njia panda wapenzi wa chadema kama anasingiziwa kiongozi wao au ni ukweli kulikuwa hakuna haja ya kutunishiana misuli baina yake na makonda.
Mfano mzuri ni ndugu gwajima kwa sasa anatembea kifua mbele na ataongea lolote bila hofu mana kapekuliwa kila kona na hajapatikana na hatia.
Kwa nini akimbie ikiwa ni kiongozi mkubwa wa kambi ya upinzani hapa anatakiwa alimalize hili suala hata akisimama ktk majukwaa aongee bila kuacha viulizo kwa maana tayari atakuwa amewashinda na hili suala liende vizuri yafaa lisihusishwe na chama alikabili yeye mwenyewe.

Unataka wote wapange msitari kwa namna moja kumwonyesha makonda kakosea? Mbowe yuko mbele sana kulki unavowaza wewe. Gwajima kafanya namna moja, Mbowe kaenda mahakamani, na wengien watafanya namna tofauti . Iko namna nyingi sana ya kuthibitisha makosa yaliyosahihi. Siyo watu wote ni wana ccm waliochoka kufikiri na badala yake wanabaki kusema "NAUNGA MKONO HOJA'.

Mbowe na aina yake ni habari nyingine wewe achana nao.
 
WhatsApp Image 2017-02-14 at 11.06.54.jpeg


Yaani aende kwa ushahidi upi, huo hapo juu..?
 
kuna watu mumekuja mjini juzi but for your information,mbowe na manji familia zao zimekuwa na hela hata kabla unga haujaingia tanzania enzi hizo madawa pekee ni bangi tu,wamekuwa matajiri kabla ya uhuru wa tanzania,kabla nyerere hajafika dar
 
mimi sio ukawa wala ccm, na wazaaa hapa kwa uchambuzi wangu, i think amekosea mbowe kuto kwenda kituoni kama yeye ana jiamini na yeye ni mwenyekiti wa chama chake ange chukua jukumu ilo kwenda aengeitikia wito kwenda tuh kutoa support regardless nini baada ya kutoka ndo ange zi sema kasoro zote, mwisho kabisa yeye mmliki wa club kubwa tuh hapa town bilcanaz sio kama ana isimamia hatakua ana watu kawa ajiri kwajili ya kuismamia club yake so pengine wafanya kazi wake wanausika? maana kwenye club kuna mengi kuna wauza unga wanakuja kuwauzia watu pale etc, club nikama kijiwe inakua ndo maana mko wa mkoa alikua ana waita baadhi ya wamiliki sio kua wanatumia au wanauza pengine unapewa report kwamba club yako ina tumika vibaya tusaidie. na WAZA TU sitaki matusi na mtu
 
Kwanini alijibu kama sio yeye?
Watu wenye akili hawaitwi kipuuzipuuzi ndio maana mbowe kawajibu na kuwapuuza kutokwenda. Wanasubiri nini kumkamata kama kweli walimaanisha ni mbowe KUB?
List imesema PHILEMON MBOWE jina limetajwa FREEMAN MBOWE. Tuamini jina lipi? Hawako serious na kazi hao watu. [HASHTAG]#Ukurupukaji[/HASHTAG].com
 
mimi sio ukawa wala ccm, na wazaaa hapa kwa uchambuzi wangu, i think amekosea mbowe kuto kwenda kituoni kama yeye ana jiamini na yeye ni mwenyekiti wa chama chake ange chukua jukumu ilo kwenda aengeitikia wito kwenda tuh kutoa support regardless nini baada ya kutoka ndo ange zi sema kasoro zote, mwisho kabisa yeye mmliki wa club kubwa tuh hapa town bilcanaz sio kama ana isimamia hatakua ana watu kawa ajiri kwajili ya kuismamia club yake so pengine wafanya kazi wake wanausika? maana kwenye club kuna mengi kuna wauza unga wanakuja kuwauzia watu pale etc, club nikama kijiwe inakua ndo maana mko wa mkoa alikua ana waita baadhi ya wamiliki sio kua wanatumia au wanauza pengine unapewa report kwamba club yako ina tumika vibaya tusaidie. na WAZA TU sitaki matusi na mtu

Kweli mkuu ingekaa poa sana hata kupambana na makonda ingekuwa rahisi sana
 
Inawezekana mtoa mada hakumsikiliza vizuri Mbowe alifanya press conference, au kwa makusudi ameamua Ku_ignore alichosema.Alisema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo halali.

Makonda hana mamlaka ya kuita watu kwenda polisi.
Tafsiri ya matendo ya Makonda inaweza kuwa alitimiza lengo alilokuwa nalo la kumtaja Mbowe ndipo akasitisha zoezi la kutaja majina.Maana alipofika episode 3 hakutaja majina ila alikabidhi kwa muhusika.
 
Mkuu hebu iweke habari yako katika aya.Hili lilikuwa ni somo dogo katika Somo kubwa la Kiswahili darasa la tano.Maada iliitwa "UTUNGAJI",hapa unakutana na imla,kutunga sentensi n.k

Turudi kwenye hoja:Huwezi kuitikia mwito ambao umekiuka sheria au una utata kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm,ambapo katika anuani ya bunge hainyoshi kuwa Mbowe ni Mkazi wa mji huo,hana "nguvu" ya kumuita Mbunge wa Jimbo la Hai,mkazi wa Hai,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,na Waziri Mkuu Kimvuli kama vile anamuita Wema Sepetu.

Huyu ni kiongozi,ni mbunge...na ukumbuke wakati anaitwa ilikuwa ni kipindi cha Bunge,hivyo mwito huo ulipaswa kuwa rasmi kupitia kiongozi wa bunge ambaye ni Spika.Huwezi kumuita "kienyeji" Mbunge na KUB ambaye ktk nchi za Jumuiya ya Madola huyu ni Waziri Mkuu Kimvuli,sauti ya upinzani na vyama mbadala ktk nchi.Jamani hamjui hata "Concept ya Political Pluralism" ktk nchi?

Huyu ni VIP...Ana diplomatic Pass...Huwezi kumuita kihuni huni kwa sbb ya "tuhuma tu".Yeye kuitikia mwito wako,ni kukubaliana na upuuzi wa uvunjaji wa taratibu ulioufanya.

Huyu Makonda madaraka yake mwisho daraja la mto Ruvu,ni uzuri wa teknolojia tu kwamba yale majina anayotangaza anatumia radio na Tv zilizofika mpaka Kalambo,Nkasi na Kibondo.Huyu ilitakiwa atangaze kupitia E-Fm na Praise Power Radio ambazo mawimbi yake yanaishia Mapinga Bagamoyo na Mlandizi-Kibaha.
 
Back
Top Bottom