Kiuhalisia Mbowe kakosea sana kutoripoti Polisi

Kiuhalisia Mbowe kakosea sana kutoripoti Polisi

Hawa ni wanaccm wanao support chama cha Mauaji financially siyo rahisi kuguswa.

Hawa hata wakiua wataulizwa Umeya Mpinzani au RAIA wa kawaida.Na watatoka kwamba alikuwa anajiprotect.Hiyo ndiyo CCM. Wauza madawa watoto wa watawala hawajaguswa wameguswa watumiaji.Ajabu na kweli.

Acha hasira, taja mmoja ashughulikiwe,
 
Kiongozi anaogopa kulala selo,mapambano atayaweza vipi?
Kitendo cha Gwajima kwenda polisi,kusachiwa na kupimwa kisha akaonekana safi,kimemsafisha kiasi kwamba hahitaji hata kuombwa radhi,lakini bwana mkubwa anahangaika jinsi ya kuzuia kuitwa kwake.
Kibaya zaidi gharama zinazotumika zinalipwa na chadema,ruzuku inatafunwa kama mchwa kwa kisingizo cha kuwalipa mawakili wa kusimamia kesi mahakamani
Kesi ya kikatiba ile itakusaidia hata wewe utakapokutana na kadhia za Kijinga za hawa Wakuu wa mikoa na Wilaya wasiofuata sheria za Nchi
 
FB_IMG_1486992228571.jpg
 
hivi wewe ndo unajua kutukana saana au???? asa kulikua kuna haja gani kutukana au umetumwa uwezi kuchangia ukaeleweka au hi ni sehemu ya mipasho, yani una maana yoyote, mtu mzima umesha poteza muelekeo tayari uko right ila una maana kabisa, uchawa ndo tatizo lenu mnakua right ila mnapitiliza na ndo mnapo pigwa bao hapo, asa matako mwenywe nimekueshimu ila sio kama sijui kutukana na kamusi hapa ya matusi , mbwa wewe mxiiiuuuw
 
Walimkosa na skendo ya madawa wakaingilia masuala ya pesa kama anatakatisha lakin bado hawamkupata huyu atatembea kifua mbele makonda hana chake hapo ila mbowe yupo kwenye hatar ya kudakwa na kuongezewa kes ya ukaid wanaijua serikali ya ccm ilivyo
Kesi ya nini tena wakati hajaitwa na jeshi la polisi? Sirro ana akili Sana, ndo maana kwenye sakata hili alikuwa anakwepa kwa kutaja kila mara mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na salama na wala siyo jeshi la polisi
 
Mi nafikir kwanza alipaswa kwenda kumaliza hilo tatizo la kashfa kisha akiwa safi arud kupambana na njia walizotumia nafikir kila mmoja angejionea ukweli wa mambo.
Kwenda ilikuwa Ni kutii Amri aramu ya Makonda Na ingemshushia heshima Sana lakini pia ingempa kiburi Makonda cha kumuita hovyohovyo na anavyotaka, Makonda asubiri tu Defamation.
 
Wa
kuipata haki ni ngumu sana hasa ukiwa mpinzani wa serikali hilo lipo wazi ila tukirud kwa alichofanya mbowe kina madhara kwake mana wataendelea kumuwinda tu hata akisema makonda hana mamlaka ya kumuita kumbuka kama ulivyosema kuna mhimili upo chini zaidi je utakubali kumuacha bila kwenda kulitatua tatizo lake?
Waende wamkamate Kama walivyofanya Kwa Lissu, Mbowe ameshawaambia tena kupitia Press conference kwamba hata enda,
 
Wewe na yule aliyemuita wote hamjielewi, kwani hata angeamua kwenda kwa kukuridhisha wewe ungekosa cha kuandika leo? Mbowe sio standard yako ktk uelewa wa demokrasia kaa mbali naye la sivyo utakuwa mtu wa kupigiwa indicator kila siku.
 
na wale engine 61 sijui , nawao walikosea?anyway yumkini alikua busy na shughuli za bunge wangeenda kumkamata hukohuko. mimi naona wote ni sungura mjanja sema mbowe akawa sungura mjanja zaidi kutokwenda kuripoti zaidi ya yule sungura mwenye dar. Na kama mAKO pIA alisema haendi bungeni kwa maana taratibu za kumuita zilikiukwa na ufafanuzi ukatoka , Mbowe nae alisema haendi kuripoti kwa kuwa taratibu za kumuita yeye kwenda kuripoti hazikufuatwa na mamlaka husika. wakiweka ugoko unaweka jiwe....by mwana jf mmoja username nimeisahau
mie siko upande wa yoyote maana hata nitukane ni ponde ni tukane ni sifie niko pale pale na ugali wangu, sema hapa kuna kitu sio picha la kawaida na watu tunachezewa akili saana sio kawaida
 
Mkuu hebu iweke habari yako katika aya.Hili lilikuwa ni somo dogo katika Somo kubwa la Kiswahili darasa la tano.Maada iliitwa "UTUNGAJI",hapa unakutana na imla,kutunga sentensi n.k

Turudi kwenye hoja:Huwezi kuitikia mwito ambao umekiuka sheria au una utata kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Dsm,ambapo katika anuani ya bunge hainyoshi kuwa Mbowe ni Mkazi wa mji huo,hana "nguvu" ya kumuita Mbunge wa Jimbo la Hai,mkazi wa Hai,Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,na Waziri Mkuu Kimvuli kama vile anamuita Wema Sepetu.

Huyu ni kiongozi,ni mbunge...na ukumbuke wakati anaitwa ilikuwa ni kipindi cha Bunge,hivyo mwito huo ulipaswa kuwa rasmi kupitia kiongozi wa bunge ambaye ni Spika.Huwezi kumuita "kienyeji" Mbunge na KUB ambaye ktk nchi za Jumuiya ya Madola huyu ni Waziri Mkuu Kimvuli,sauti ya upinzani na vyama mbadala ktk nchi.Jamani hamjui hata "Concept ya Political Pluralism" ktk nchi?

Huyu ni VIP...Ana diplomatic Pass...Huwezi kumuita kihuni huni kwa sbb ya "tuhuma tu".Yeye kuitikia mwito wako,ni kukubaliana na upuuzi wa uvunjaji wa taratibu ulioufanya.

Huyu Makonda madaraka yake mwisho daraja la mto Ruvu,ni uzuri wa teknolojia tu kwamba yale majina anayotangaza anatumia radio na Tv zilizofika mpaka Kalambo,Nkasi na Kibondo.Huyu ilitakiwa atangaze kupitia E-Fm na Praise Power Radio ambazo mawimbi yake yanaishia Mapinga Bagamoyo na Mlandizi-Kibaha.
KAMA MLETA MADA HAJAKUELEWA TU, BASI msameheni. Kuendelea ni kupoteza muda. MADA IMEFUNGWA.
 
Kama mapambano yenyewe tunamuhusisha MADABIDA aliyetuuzia arv feki! Bado tunaita shughuli ya kitaifa.......
Hongera sana mbowe kwa kujielewa na mpaka watume polisi hakuna kwenda!
Aisee duuuh na kweli hii kesi ya ARV feki imeishia wapi !!??
 
Kwenye hili sakata la madawa ya kulevya kwa namna lilivyokuwa likiendeshwa na bwana Makonda ilikuwa ni nafasi nzur sana kwa yeye Mbowe kumuonesha Makonda hakuwa sahihi.

Hii ingetoa nafasi ya kujijengea imani kwa wapenzi wa UKAWA na CHADEMA ni kwa namna gani serikali inavyopambana na upinzani kuumaliza kwa kuwazushia mambo. Kitendo cha kutokwenda kinawaweka njia panda wapenzi wa CHADEMA kama anasingiziwa kiongozi wao au ni ukweli kulikuwa hakuna haja ya kutunishiana misuli baina yake na Makonda.

Mfano mzuri ni ndugu Gwajima kwa sasa anatembea kifua mbele na ataongea lolote bila hofu mana kapekuliwa kila kona na hajapatikana na hatia.

Kwanini akimbie ikiwa ni kiongozi mkubwa wa Kambi ya Upinzani? Hapa anatakiwa alimalize hili suala hata akisimama ktk majukwaa aongee bila kuacha viulizo kwa maana tayari atakuwa amewashinda na hili suala liende vizuri yafaa lisihusishwe na chama alikabili yeye mwenyewe.
Sisi wana ukawa na cdm tuna imani kabwa sana na mh Mbowe
 
Kama mapambano yenyewe tunamuhusisha MADABIDA aliyetuuzia arv feki! Bado tunaita shughuli ya kitaifa.......
Hongera sana mbowe kwa kujielewa na mpaka watume polisi hakuna kwenda!
Mkuu hivi huyo jamaaa aliyekuwa anatengeneza arv feki bado yupo ndani ya chama kweli?
 
Kwenye hili sakata la madawa ya kulevya kwa namna lilivyokuwa likiendeshwa na bwana Makonda ilikuwa ni nafasi nzur sana kwa yeye Mbowe kumuonesha Makonda hakuwa sahihi.

Hii ingetoa nafasi ya kujijengea imani kwa wapenzi wa UKAWA na CHADEMA ni kwa namna gani serikali inavyopambana na upinzani kuumaliza kwa kuwazushia mambo. Kitendo cha kutokwenda kinawaweka njia panda wapenzi wa CHADEMA kama anasingiziwa kiongozi wao au ni ukweli kulikuwa hakuna haja ya kutunishiana misuli baina yake na Makonda.

Mfano mzuri ni ndugu Gwajima kwa sasa anatembea kifua mbele na ataongea lolote bila hofu mana kapekuliwa kila kona na hajapatikana na hatia.

Kwanini akimbie ikiwa ni kiongozi mkubwa wa Kambi ya Upinzani? Hapa anatakiwa alimalize hili suala hata akisimama ktk majukwaa aongee bila kuacha viulizo kwa maana tayari atakuwa amewashinda na hili suala liende vizuri yafaa lisihusishwe na chama alikabili yeye mwenyewe.
Hahahahah sasa angeendaje kamanda wakati anahisi kuna dili fulanifulani zitaweza kuibua maswali ambayo hayatakuwa na majibu. Usicheze na wanasiasa bana. Ndio maana Zito alisemaga usimwamini mwanasiasa hata siku moja. Tunaamini kwa kukataa kwake kwenda tunahisi kuna samsing kule. Si bure. Ngoja waje wamdake
 
Back
Top Bottom