Uchaguzi 2020 Kituo nilipopiga kura hakuna wakala wa CHADEMA wala ACT-Wazalendo

Dah..wapi hii kaka
Come on Mshana, yaani wewe hujajua tu huyu jamaa anachojaribu kukifanya? Kiingereza inaitwa voter suppression . Maana yake ni kutaka kuwakatisha wapiga kura tamaa kama chama chao au mtu wao anashinda ili wafuasi wakate tamaa na kuacha kupiga kura.
 
Hata Mimi hema nilio ingia nimeona wakala wa CCM.... Dah, sijui kama ni ile figisu ya kutopewa barua za utambulisho?!
 
Itakuwa hawajalipwa posho na VYAMA vyao. CCM tupo?
 
Ni kituo gani, Jimbo, wilaya, mkoa upi ili tuwaambie Lissu na Maalim wapeleke wakala haraka
 
Anatafuta uchochezi wa kuandamana jamaa maana hakuna njia nyingi kwa CDM zaidi ya kutengeneza mazingira ya fujo kuingia Ikulu.
 
Hata Mimi kituo nilichopiga hakuna wakala wa Cdm. Walikuepo wa Ccm na Cuf, nimeondoka pale nimekata tamaa kabisa . Halafu ni kituo cha mjini huwezi kusingizia usafiri mbovu
 
Mimi nimeenda kupiga kura ndani mimekuta watu wa tatu tu mmoja anasoma namba na mwingine anaandika na mwingine anakupa karatasi za kupigia kura. Nimeshindwa kuelewa pale yupi ni wakala wa chama na yupi ni mtu wa tume ya uchaguzi.
Sasa hapo ni kwamba hakuna wakala au hujaelewa yupi ni wakala maaana Title ya thread haiendani na ulicho kiandika ndani πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Waache ujinga
 
Tulia dawa iingie vizuri. Ndio mjue hakuna kuvuna bila kupanda. Chama ccm kimesukwa vibaya mno, tangu mizizi mpaka matunda. Msione vyaelea, vyaundwa.
 
Pengine wameshawapeleka kusiko julikana. Kumbuka hadi sasa tuna vifo kama kumi hivi nafikiri, na bado ni asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…