Jambo la ajabu limetendeka Makongo juu, mgonjwa kapelekwa hospitali Mwananyamala juzi akalazwa. Walioenda kumjulia hali jana asubuhi wakarudi wanalia kwamba mtu wetu kafariki. Taarifa zikasambaa ukawekwa msiba, maturubai, watu kibao tumelala msibani. Rambirambi zimechangwa.
Ajabu asubuhi hii aliyeenda hospitali kukamilisha taratibu za huko kaleta taarifa kuwa mgonjwa alikuwa hajafa, ila alihamishwa kitanda! Hivi ndo kila mtu kabaki mdomo wazi. Ndo tunaondoa maturubai na kurudisha makochi ndani.
My take: Tuwe makini, kabla ya kusambaza taarifa mtu kafa, tucomfirm kabisa na daktari na ikibidi ushuhudie mwili kabisa. Usumbufu mkubwa watu wamepata na itaathiri sana maisha katika familia ya mgonjwa.
Mungu aendelee kumponya. Amen.