Loyalist
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 411
- 884
Ni kitu gani kinawazuia kununua mashamba kama wanavyonunua watanzania wengine?
Wachagga wangapi wamenunua na wanamiliki mashamba makubwa Morooogoro, pwani, Tanga na kwengineko?! Sio kana kwamba wachagga hupewa ardhi bure na serikali, wengi wamenunua na wanamiliki mashamba na maeneo mmakubwa sana mikoa mbalimbali hili liko wazi, hata Mimi nina shamba langu Geita kijiji cha IISULWA BUTINDWE, nilinunua kwa jamaa mmoja wa ukoo wa MABINA.
Kujibu swali lako ni rahisi sana, watu wakule vijijini wangapi wanajua maeneo makubwa yasiyo na watu kwenye mikoa mingine?!
Wakiomba ardhi ili wapate mashamba ya kulima ni kosa kisheria?!
Kwani wakina bakhera na wengine waliopewa ardhi na serikali wasingenunua kwa fedha zao?!