Kitu pekee kitakachoitoa CCM madarakani ni mgawanyiko wa ndani ya chama na sio vinginevyo

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,299
Nimekuwa nikisoma mashambulizi mbalimbali mitandaoni dhidi ya chama kilichobeba matumaini ya watanzania wote wakiwemo wanaokiponda hasa CHADEMA na kujikuta wakati mwingine niwaze kitakachoitoa CCM madarakani. Ukisoma maandishi ya wapinzani unaweza ukatishika na kudhani mwisho wa CCM ndo umewadia. Baada ya kutafakari nikagundua jambo pekee litakalofanya CCM ianguke ni kama itashindwa kudhibiti migogoro na migawanyiko ndani ya chama kwa haraka.

Mwaka 2015 sisi wanaCCM tulipata funzo ambalo hatutakaa tulisahau. Uchaguzi ulikuwa mgumu sana kutokana na kuchelewa sana kudhibiti vikundi vilivyoleta mgawanyiko mkubwa chamani kiasi kwamba kwenye uchaguzi ule tulishuhudia mwanachama akiwa na nguvu kubwa kisiasa huenda zaidi ya mwenyekiti wa chama. Kura zetu nyingi zillienda upinzani kupitia mwanachama yule na wafuasi wake waliokihama chama wakati wanahitajika sana. Isitoshe usaliti ulikuwa wa hali ya juu kwenye uchaguzi. Kwa sababu CCM inajua umuhimu wa kuwa madarakani haikurudia kosa 2020 na inazidi kujirekebisha.

Shukrani kwa waasisi wa chama waliohakikisha Rais anakuwa pia mwenyekiti wa CCM. Hizi kofia mbili zinamfanya mwenyekiti wa chama na Rais kupata urahisi wa maamuzi yenye tija. Kwa wale wanaojipa ujasiri wa kutumia lugha mbaya zilizokosa ustaarabu dhidi ya Rais niwakumbushe kuwa mnapiga ukuta ngumi na mtaumia wenyewe. Rais wa Tanzania ana namna nyingi sana za kudili nanyi. Wakati wa Magufuli mlisema kwanini anafanya maamuzi kivyake bila kushirikisha bunge ila sasa hivi Rais anashirikisha bunge mnalia na kudai bunge la CCM wakati mna wabunge 19 viti maalum CHADEMA na mmoja wa kuchaguliwa kupitia CHADEMA.

Ninatoa wito kwa wale ambao hawana kadi za CCM hakikisheni mnazipata. CCM bado sana iko madarakani kwa miaka mingi sana ijayo. Vitukuu vyetu wataikuta CCM iliyo imara.
 
CHADEMA Kwa sasa hawaweziitoa CCM kwani walikubali muafaka bila kutumia ajili Bali wakatangukiza manufaa Yao na chukua shidi ya Magufuri
 
CCCM uhai wake hauzidi 2025.

Sikitiko langu kuhusu chama hiki ni,

Kinakufa bila kuacha mrithi,

CCCm inakufa bila kuandika wosia,

Kila mara ulimposhauriwa kuwa, andika urithi kabisa Kwakuwa mambo hubadilika,

Ulijibu Kwa dharau kwamba Bado upo upo sana,

Ni Kweli CCCm Si chama Cha siasa, ni Dini, dini ambayo kuondolewa lazima ilete mtikisiko,

Chama hiki ni nyoka ambaye hazeeki, Kila mara hujivua gamba na kurudi ujanani,

Umejisahau, na adui zako wamekuotea, watakuponda KICHWA Kwa ghafula.

Narudia, ungeandika wosia na kutuachia mrithi, tungebaki salama,

Kutokuwepo mrithi, kutasababisha majirani kuja kudai shamba letu ni Mali Yao na itatupa shida kuwabishia,

Andika mrithi, na aga kabisa maana kifo chako kimewadia.

Tusubiri.
 
CCM ife kwani hata upinzani haiwezi imezoea vya Dezo vya kusotea haiviwezi.

Bye Bye Mafisadi.
 
Back
Top Bottom