Kitu kipya kinakuja Iphone 8


Sawa mkuu tusubiri September. Mimi iphone 7 plus yangu wamenipa upgrade plan September mwaka huu. Na pia huu ni mwaka wa kumi tokea iphone ya kwanza itoke. Watakuwa na kijisherehe.
 
Mimi na kitecno changu JF inafunguka baas inatosha.

Uko vizuri mkuu. Bei za hizi simu ziko juu sana kwa sababu ya vitu vingi ambavyo haviko Bongo.

Kwenye simu yangu nimedownload app ambayo inaniwezesha kuangalia channel zote karibu elfu za TV kwenye simu. Sihitaji kuwa nyumbani kuangalia live gemu za Chelsea au Barcelona.

Sasa hivi wametoa app ambayo unaweza kukaa nyumbani ukaagiza chakula uletewe nyumbani au unaenda kuchukua mwenyewe.

Kampuni za usafiri zina apps zao unadowload kwenye simu na kupanga safari zako.

Unaweza kuunganisha server ya email za kazini kwako.

Conference calls mtu anaweza kuwa ndani ya teksi akahudhuria mkutano muhimu wa kazini na watu wa majimbo tofauti mwingine yuko Chicago, mwingine California, mwingine Canada.


Security unaweza kufunga camera nyumbani kwako ukaangalia kinachoendelea nyumbani kwako wewe mwenyewe uko kazini au mbali sana na nyumbani kwako.

Google voice na Siri ni balaa. Unauliza swali unajibiwa mpaka unazima sigara.

GPS nimegundua inafanya kazi Bongo lakini sijajaribu kuona kama voice yake inafanya kazi au iko sahihi. Sijui itakupa muongozo gani ukiiambia ikatize mitaa ya Tabata

Kuna vitu vingi sana kiasi kwamba hata Laptop zimepungua shughuli. Kimsingi hata wazee wakoloni wakoloni wanaapreciate hizi simu ni muhimu sio luxury tena.

Sasa unapotoa milioni mbili kununua Iphone Bongo na unaiutumia kwa WhatsApp na Instgram tu Internet yenyewe tete huwezi hata kuangalia movie. Kwa kifupi ni uzembe.

Ukizingatia ikiibiwa imeibiwa hakuna chs bima wala nini.
 

Mkuu umeandika bandiko zuri na refu ila kuna sehemu nitapingana na wewe.

iPhone huwa hawatabiriki sana katika matoleo yake hvyo kutaja hilo gape la miaka 4 ndo kunakuwa nachange kubwa ni uongo. Tangu zianze huwa zinatoka kila mwaka hvyo toleo kuu hufuatiwa na toleo (s). Mfano iPhone 4 ikaja 4s. 5,6 na tunategemea 7 pia.

Kusema pia kuwa iphone 5s na 6 zinafanana kabisa kiutendaji ni uongo labda kama ulikuwa ukimaanisha SE.
6s ina tofauti nyingi na hiyo 7 unayotaka kuilinganisha nazo.
Ila kwingine kote naungana na wewe.
 
waambie itakua na fingerprint kabisa
 
Ila iPhone wanaibia watu ukiangalia product zao hakuna mabadiliko makubwa sana toka iPhone 5 huuu wizi jamani do
Iphone 5 ina tofauti kubwa na 5s labda kama.unaangalia umbo.
Kwanza 5 ina 32 bits processor
Halafu siyo mult task
Njoo kwenye camera pia
Inaelekea we si mtumiaji ni mtazamaji kwa hiyo waona zinafanana fanana kwenye maumbo wadhani ziko sawa.
 
ILE SIRI NI UNYAMA NA WAMESEMA WAMEIBOROSHA ZAIDI NA KUONGEZA LUGHA
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…