sasa wabongo hapo ndoa zitavunjika kisa ni Iphone 8. Waume watalazimishwa walipe milioni mbili ili wake wang'are na Iphone 8.
Isiwe tabu wewe kama Tecno yako au Huwaee ina WhatsApp na FB uko vizuri.
Hivi vitu kwa wenzetu haviumizi sana kichwa. Kwanza bili ya simu ni kwa mwezi si ya bando la halichachi. Na mtu anaweza kuwa na plan yenye uprade. Simu mpya ikitoka anarudisha ya zamani anapewa mpya.
Pia mtu anaweza kuchukua simu mpya bila ya kulipa chochote akalipa kidogo kidogo kwenye bili yake ya kila mwezi.
Mwingine anaweza kuzinguana na bima. Akasema simu imepotea akapata mpya.
Yote tisa kumi ni nusu ya vitu vilivyomo kwenye hizi simu babu kubwa havina shughuli yeyote Bongo.
Tuache masihara simu zinamalizia watu hela Bongo kichizi. Wanalalamika bei ya sembe lakini hawapigi hesabu wanapoteza pesa ngapi kwenye hivi visimu.
Halafu wachunguzwe hawa kina Voda kama wamesajiliwa na wanalipa kodi. Wasijekuwa ni wale wale kina mchanga wa dhahabu.