Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Thibitisha kufanikiwa kwa mtu kutumia uchawi onyesha connection
Mafanikio kamili ya mwanadamu huja ikiwa kuna uwiano sahii( balance)wa nguvu ya Roho, nafsi na mwili. Roho, nafsi na mwili ni vitu ambavyo vipo katika state/dimension ( hali) tatu tofauti.
Kwa mwanadamu kazi kuu ya mwili ni kuchukua maelezo kutoka rohoni na kuyafanyia kazi na uchawi unaoungelea hufanya kazi katika dimension ya rohoni hivyo basi,nguvu hii huweza kuufanya mwili kuweza au kushindwa kufanya mambo flani ambayo mwisho wa siku humfanya mtu kupata au kukosa kitu flani katika dimension ya mwili.
Najua unaweza kufikiri kuwa ubongo ndo huongoza mwili, ila si kweli.Ubongo ni chombo tu ambacho akili hutumia ili kufanya mambo yake na akili yenyewe ni sehemu ya roho.Kwa kifupi ubongo ni sehemu ya mwili tu kama ulivyo mkono au mguu.
Mfano mwepesi ni kwamba, wapo wenye miguu lakini hawatembei, wapo wenye macho lakini hawaoni ni hii ni kuashiria kwamba miguu haitufanyi tuweze kutembea. Ila ipo nguvu inayotuwezesha kutembea ambayo huitumia miguu ili kufanikisha lengo hilo.Hivyo basi kama nguvu ya kutembea haitokuwepo basi miguu haitiweza kutembea kamwe na nguu hii huwa ipo kwenye dimension nyingine.
 
🤣🤣🤣🤣Mnapenda Sana kumsingizia newton wa watu...kina Einstein.. skia kipindi hicho ukiwa atheist unapingwa na jamii nzima. Nitajie modern scientist ambae anaamini uchawi. Ambao hawaamini wapo kibao bill gates Elon musk etc nitajie wanaoamini...modern scientists nasubiria
Kwani Gate na Elon ni scientists?
 
Siyo wataalamu kila kitu kipo wazi vipo vtabu wikipedia, academy apps kote huko wanaelezea na ukitaka kufanya majaribio uprove fanya.

Embu thibitisha huyo mtu alitibiwa kwa wiki mbili?

Tunajua unatafuta kuwaibia watu na sasahivi watu wame elimika.

Nasubiri jibu unipe connection
Wajibu ni wako, kama unataka tu kuthibitsha sema upelekwe. Itakugharimu nauli yako tu utakutana na wagonjwa wa juzi, Jana na hata wa leoleo. Nawe utaasses majeraha yao, kisha utafuatilia matibabu na uponaji wao.

Zingatia: Sikusema week mbili, NI MOJA TU.
 
Mafanikio kamili ya mwanadamu huja ikiwa kuna uwiano sahii( balance)wa nguvu ya Roho, nafsi na mwili. Roho, nafsi na mwili ni vitu ambavyo vipo katika state/dimension ( hali) tatu tofauti.
Kwa mwanadamu kazi kuu ya mwili ni kuchukua maelezo kutoka rohoni na kuyafanyia kazi na uchawi unaoungelea hufanya kazi katika dimension ya rohoni hivyo basi,nguvu hii huweza kuufanya mwili kuweza au kushindwa kufanya mambo flani ambayo mwisho wa siku humfanya mtu kupata au kukosa kitu flani katika dimension ya mwili.
Najua unaweza kufikiri kuwa ubongo ndo huongoza mwili, ila si kweli.Ubongo ni chombo tu ambacho akili hutumia ili kufanya mambo yake na akili yenyewe ni sehemu ya roho.Kwa kifupi ubongo ni sehemu ya mwili tu kama ulivyo mkono au mguu.
Mfano mwepesi ni kwamba, wapo wenye miguu lakini hawatembei, wapo wenye macho lakini hawaoni ni hii ni kuashiria kwamba miguu haitufanyi tuweze kutembea. Ila ipo nguvu inayotuwezesha kutembea ambayo huitumia miguu ili kufanikisha lengo hilo.Hivyo basi kama nguvu ya kutembea haitokuwepo basi miguu haitiweza kutembea kamwe na nguu hii huwa ipo kwenye dimension nyingine.

Thibitisha kuna kitu kinaitwa roho kabla hatujaendelea. Umeandika stori zako
 
Nikiwa shule msingi miaka ya nyuma nikitoka shule Mwadui shinyanga ndani ya mgodi nilipishana na mtu tulipokaribiana nilishangaa kuna nguvu inanilazimisha kumpisha yule mtu umbali wa mita 5 pembeni mwa barabara hadi baada ya kupishana ndipo nikarudi barabarani. Hadi leo sijapata majibu yule mtu alikuwa na nguvu gani. Maana watu huwa wanapishana nusu mita au mita.
Kumbe umesomea mwadui?
 
Ndugu embu kuwa muelewa kidogo...
Hata nikitengeneza baiskeli ni Sayansi ndio, na kunapimika Maabara. Yaelekea hujui maana ya Sayansi (nafikiri umri unahusika hapa)
Ikiwa Sayansi ni mchakato wa kutatua matatizo, nini kinafanya mtofautishe Sayansi na mkiitacho Uchawi, maana nao ni mchakato wa kutatua matatizo?

Ndugu:
Sayansi ni Laws and Principles.... Ndio maana ninakuambia Hata mnachoita Uchawi ni Sayansi maana una Laws and Principles.
Bas soma definition ya uchawi google afu urudi hapa...naona hujui unachoongea
 
Eti video za behind the scenes... Ndugu, yaani kumbe HATA MAZINGAOMBWE UNAYAONA KWENYE VIDEO??????

SIO KOSA LAKO NDUGU! Mazingaombe SIO CUMPUTER FICTIONS, yapo hata kabla hatujajua TV ni nini.
Sijasema computer fictions jamani afu unakera kinoma....unazunguka hapa hapa. Nimekuambiaje, tafuta breaking the magician codes au video zinazoelezea mazingaombwe na wewe uelewe. Kama hutaki acha, Baki kuamini kuwa ni uchawi. Ile ni talent Kama zingine tu, Kama mtu kujua kudance lazma ujifunze skills fulani
 
Kweli nimeamini alichosema member mmoja huko juu kuwa nyie ni wanafunzi bado watoto wadogo, ukikuwa na kutoka kwa mjomba wako pengine ndio utajione hali ilivyo.

Karibu JF naona ndio kwanza una miezi miwili tu.
🤣🤣🤣🤣🤣We unajuaje mi sijaoa Nina watoto...skia Kama Kuna umri wa kuona uchawi utaje bac...tuambie ikifika umri fulani utaona uchawi
 
Ni kwa Sheria na Kanuni Asilia za Matibabu, kinyume na mnazofundishana Darasani. Ukitaka kuzijua ingia Darasani.

Ninachoweza kukuonesha mgonjwa anayepona kwa mnachoita Uchawi, kujua mechanism gani inafanyika ni professional ya mtu.
Si ndo Sayansi yenyewe...hayo matibabi asilia ni Sayansi...Sayansi sio lazma uchomwe sindano...hujui Sayansi ni Nini ndo maana unaongea ujinga tu..hujui hata uchawi wenyewe unaoongelewa huku ni Nini...hatuongelei kutibu kutumia miti... tunaongelea watu kutokewa na majini usiku...so rejea kichwa husika please
 
eti mbona watu matajiri hawatokewi na hivi vitu,una ushahidi?
Ndio...watu wanaoamini uchawi most of them ni watu wa uswahilini, au vijijini watu ambao hawana elimu au fikra za kisayansi...wanaendeshwa kwa hisia na upepo wa fikra za jamii.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom