Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 45
Anachosema Mzee Kitine kuhusu nchi kuongozwa kienyeji ni kweli kabisa. Viongozi wengi wamekuwa wababaishaji mno na sijui wamepata vipi huo uongozi. Wanapenda mno uongo kwa sisi wadanganyika!!! Hivi hatuna namna ya kujua watu kabla ya kupewa nyazifa za juu za uongozi? Ama ndio urafiki na undugu wa kugawana nafasi za umma.
Kweli tunahitaji mabadiliko na We need strong leaders when it comes to bold changes...we should never allow things to take us by chance!!! Sasa leo hii we spend more time dealing with petty issues and forget about development.
Nafikiri tufikirie kuwa na mfumo wenye nia ya makusudi ya kuawaandaa vijana wenye uwezo wa kuwa leaders right from the scratch kuwa viongozi wa baadae
Tusiwaachie mafisadi wakaendelea kutuchagulia wapendwa wao. Watayaendeleza matatizo tuliyo nayo leo mpaka yatumalize mana yanafanana fanana Cancer
Mkuu Ndahani, unachosema ni kweli kabisa. Utaratibu uliopo umeshindwa kukindhi mahitaji ya nchi kwa sasa. Huko tuendako, hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
Kitine anajua anachosema. Amekuwa kwenye system kwa muda mrfu kuliko Chiligati. In fact, Chiligati amezunguka kauli za Kitine kwa kuanza kuzungumzia amani na utulivu. Ila inashangaza sana kusikia kauli kama hiyo wakati kama huu. Ukiniuliza kama kweli kuna utulivu, nitakataa kwa kiapo. Utulivu umekosekana na ndio maana Kitine anasema mambo yanakwenda kienyeji. Watendaji na viongozi wetu hawajui nini cha kufanya ili tuendelee.
Mkuu, kubadili hali iliyopo sasa, inabidi kubadili Katiba ya nchi. Ni kweli kwamba inawezekana viongozi wa kisiasa wanaoteuliwa wakachambuliwa kabla ya kushika nyadhifa wanazopewa. Ila Katiba inampa madaraka Rais kuteua viongozi wa juu kabisa wa nchi kwa vigezo hafifu sana. Kwa mfano, Waziri Mkuu anatokana na Wabunge wa kuchaguliwa wenye viti vingi Bungeni. Mtu yeyote mwenye hadhi hiyo anaweza kuwa Waziri Mkuu kwa kuteuliwa na Rais na waBunge kusema "ndio" au "hapana". Madaraka makubwa ya Rais, huwafanya waBunge kusema ndio hata kama wana sababu za kusema hapana (ili wasiudhi utawala).
Lingekuwa jambo muhimu pia kwa Mawaziri wote kuteuliwa kutoka popote (kati ya Raia wa Tanzania) bila kujali kama ni waBunge (in fact wangekuwa sio waBunge ingekuwa vyema zaidi). Na wapitishwe na Bunge kwa kujadiliwa kama Baraza zima la Mawaziri ili mchakato huo uwe wa haraka na wa moja kwa moja. Hii yote inategemea mabadiliko ya Katiba. La sivyo haitadumu sana.