William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Hii ni Black propaganda tu, ajue faili lake takukuru laweza pelekwa kwa DPP pia.
- Eddy tupo pamoja mkuu!
Hii ni Black propaganda tu, ajue faili lake takukuru laweza pelekwa kwa DPP pia.
Mkuu FMES,
Nimekusikia. Nakubaliana na mengi unayosema lakini ujumbe wangu umelenga zaidi
aliyoyasema Kitine. Unajua hapa Marekani kuna benki ilimwajiri mwizi aliyekubuhu katika bank robbery awasaidie kupambana na wizi huo. Sasa kama Kitine ni fisadi naye ameona kuwa mambo nchini hayaendi vizuri, tusikilize ujumbe wake. He may have some inside information, no?
Katika mkutano wake maalum na baadhi ya vyombo vya habari katika mgahawa wa Gymkana jijini Dar es Salaam pamoja na mambo mengine Kitine alisema mfano wa kuoza kwa maadili ndani ya CCM upo wazi pale waziri anapojiuzulu wadhifa wake kwa tuhuma, lakini bado anabaki kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mbunge.
Kama Kitine alikuwa fisadi zamani basi kwa maneno aliyoyasema kuhusu uongozi wa nchi yetu sasa ameokoka, amebadilika.
- Kitine ameiba akafukuzwa na Mwalimu uwt, mkewe akaiba akajizulu uwaziri, lakini sio ubunge mpaka wananchi wa Makete, walipoamua kumtosa kwa sababu ya ufisadi wake kwa taifa, huko kote hakuona madhara ya kuiba na kubaki mbunge huku akijiuzulu uwaziri tu,
- Leo baada ya kuwa on the sidelines kwa muda mrefu sana, sasa anataka mabadiliko, lakini yaanzie na wengine sio yeye, lakini ninatakiwa hapa nisimjadili Kitine maana ninakuwa siitakii mema Tanzania, haya mnaoitakia mema Tanzania kwa kujadili hoja yake tu endeleeni wakuu.
Kwenye kitabu kitakatifu hakuna mtu aliyekuwa mchafu kama Saulo. Lakini leo hii Wakristo wote tunajitahidi kufuata maagizo ya Saulo ambaye baada ya kuona mwanga akiwa njiani kuelekea Damascus aligeuka na kuwa Mtakatifu Paulo. Kitine naye huenda ana madhambi yake, lakini tusikilize ujumbe wake. Je,anayoyasema ni kweli? Tukianza kutafuta watakatifu peke yake katika vita vya ufisadi hatutafika mbali.
Mhe. Koba, nakushukuru kwa uungwana wako....st-upid kuokoka my a$$!
Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji
na Edward Kinabo
Tanzania Daima~Sauti ya watu
MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, amesema taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi.
Kitine ambaye aliiongoza idara hiyo nyeti kwa karibu miaka 30 zama za Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema ukosefu huo wa uongozi umesababisha nchi iongozwe kienyeji.
Kachero huyo namba moja kwa miaka mingi, ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, mwishoni mwa miaka ya 1990 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya mkewe kufuja fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 40, alirejea kutoa kilio chake cha miaka mingi cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi nchini.
Kitine ambaye aliwahi pia kuwa Mbunge wa Makete kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitoa matamshi hayo mazito katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa vyombo kadhaa vya habari.
Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia, ni vigumu kurekebisha maadili ya uongozi.
Tatizo kubwa ni viongozi kukosa integrity (uadilifu). Kwanza ni integrity ya viongozi wenyewe, pili ni commitment (wito), tatu ni nationalism (utaifa). Haya ndiyo yalikuwepo wakati wa Mwalimu, alisema Dk. Kitine.
Akizungumza kwa kujiamini kama ilivyo kawaida yake, Kitine alisema viongozi wengi wa serikali wamepoteza sifa kuu tatu za uongozi ambazo ni kuwa na uadilifu, wito na kuweka mbele utaifa, sifa ambazo alisema ndizo zilikuwa nguzo ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, chini ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
That was possible (hilo liliwezekana) chini ya Mwalimu. Kama alikuwa akifanya kosa, basi kosa hilo lilikuwa likitokea tu wakati akifanya jambo kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania.
Philosophy (falsafa) ya Mwalimu, ilikuwa kwanza Mungu, pili Tanzania, halafu yeye binafsi. Kila kiongozi anayetofautiana na Mwalimu tu hulifikisha taifa hili kubaya, if you differ with him, utaishia kubaya, alisema Dk. Kitine akionyesha hali ya masikitiko.
Alisema uteuzi mbaya wa viongozi, hususan ule wa mawaziri, umechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa viongozi wasio waadilifu, wengi wao wakijihusisha na vitendo vya rushwa.
Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).
Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia, alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote.
Kitine ambaye wakati wote wa mazungumzo yake alisema alikuwa anataka kujadili masuala muhimu na si watu, alieleza namna asivyo na imani na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo la rushwa kubwa.
Kwa mujibu wa kachero, mwanasiasa na mwanazuoni huyo, hatua hizo ambazo zinahusisha baadhi ya watu wenye majina makubwa kufikishwa mahakamani, zimechukuliwa kwa ajili tu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.
Nilikuwa kiongozi wa kwanza kuzungumzia rushwa kubwa miaka 10 iliyopita. Nilisema ndiyo inayovuruga uchumi kuliko hata rushwa ya nesi, hakimu, polisi,. hakuna hata mkubwa mmoja aliyekamatwa. Ilinigharimu sana, na mimi nilipata adhabu ya kuzuiliwa kikao kwa miezi miwili, kama huyu nani huyu, Zitto (Kabwe). Wakati huo ilikuwa ndani ya CCM.
Mimi nadhani hatua hizi zinazochukuliwa hazilengi kukomesha tatizo la rushwa, ni siasa tu za uchaguzi, alisema Dk. Kitine.
Alipoulizwa nini kifanyike ili kukabiliana na tatizo hilo la uongozi mbaya, pamoja na mambo mengine, alielekeza changamoto zake kwa Idara ya Usalama wa Taifa.
Usalama wa Taifa should be completely clean (unapaswa kuwa safi kabisa). Idara hii inatakiwa kuwa, juu ya mambo ya rushwa, iwe safi kabisa. Usalama wa Taifa ndiyo unayoteua viongozi, ndiyo inayoshirikiana na rais kwa kumshauri katika kuteua mawaziri. Sasa kama Usalama wa Taifa ukiwa mchafu ndio tunapata viongozi wala rushwa. Nafikiri vigezo vinavyotumika kuteua viongozi pia vina matatizo, alisema Dk. Kitine.
Kada huyo wa CCM ambaye kitaaluma ni mchumi na mwanasheria, akizungumzia hali ya uchumi nchini, alisema kwa kiasi kikubwa uchumi umeshikiliwa na wageni kuliko wazawa, na kuelezea kusikitishwa kwake juu ya kuwepo kwa pengo kubwa kati ya matajiri na maskini.
Akitoa mfano alisema, miongoni mwa mambo yanayoonyesha kuparaganyika kwa mambo ni kukithiri kwa idadi ya ombaomba mitaani.
Mwalimu asingeruhusu watu hawa waombeombe barabarani. Kazi za Watanzania ni udereva teksi, daladala, mabasi, kazi ya uboi ndani ya nyumba na kazi ya kufagia barabarani. Hizi ndizo kazi za Watanzania na hawa ndio wenye mali.
Uchumi huu wa Watanzania si wa kwao. Watanzania ambao ni matajiri hawazidi hata watano. Hakuna sera bora za kusaidia kutumia maliasili zetu ili zitupe fedha ya kujenga shule, madaraja, hospitali .. alisema Dk. Kitine.
Akizungumzia utendaji wa kazi wa Bunge katika kusimamia utendaji wa serikali, Kitine alisema kazi inayofanywa na taasisi hiyo hivi sasa ni kubwa kuliko ilivyopata kuwa wakati wowote huko nyuma.
Hata hivyo katika kuusifia utendaji wa kazi wa Bunge, aliupongeza mchango mkubwa na muhimu wa wabunge wa upinzani katika kuiimarisha taasisi hiyo muhimu.
Ni Bunge zuri kuliko lilivyowahi kuwa huko nyuma. Linaonyesha kila dalili za uhuru. Upinzani unafanya kazi nzuri. Bunge liko wazi zaidi na wabunge wanatoa michango mingi yakinifu, yenye manufaa kwa taifa. Likiendelea hivi tutafika mahali pazuri, alisema.
Hata kama anayosema Kitine ni kweli, uzito wa anayosema unapungua kwa sababu naye anatuhuma zinazofanana fanana na za hao anaowasema. Ndio maana criticism za Nyerere, hasa kwenye mambo ya ufisadi, umomonyokaji wa maadili ya viongozi na mengineyo zilikuwa na nguvu na watu angalau walikuwa wanajaribu kusikiliza.
Yaani Kitine aliyeiba US$64,000 mwaka 1997 akishirikiana na Mkapa leo ana nguvu za kusema nchi inaongozwa kienyeji? Huyu ndie alitakiwa apelekwe kisutu faster faster kwa kuiba na kutumia madaraka vibaya....tunapoteza muda kuwajadiri akina Masha wakati ushahidi wa wizi wa Kitine ni more convincing.
Kwanza Kitine atueleze jitihada alizofanya kuzirudisha US$64,000 alizoiba ndipo atupe msimamo wake juu ya mapungufu ya serikali ya sasa. Vinginevyo anakuwa kama padre anayehubiri kuacha usherati baada ya kushinda tuzo kadhaa za usherati.
Mhe. Koba, nakushukuru kwa uungwana wako.
That was possible chini ya Mwalimu. Kama alikuwa akifanya kosa, basi kosa hilo lilikuwa likitokea tu wakati akifanya jambo kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania.
Mwalimu asingeruhusu watu hawa waombeombe barabarani...
Kwenye kitabu kitakatifu hakuna mtu aliyekuwa mchafu kama Saulo. Lakini leo hii Wakristo wote tunajitahidi kufuata maagizo ya Saulo ambaye baada ya kuona mwanga akiwa njiani kuelekea Damascus aligeuka na kuwa Mtakatifu Paulo. Kitine naye huenda ana madhambi yake, lakini tusikilize ujumbe wake. Je,anayoyasema ni kweli? Tukianza kutafuta watakatifu peke yake katika vita vya ufisadi hatutafika mbali.
"Mmesikia habari za mwenendo wangu zamani kwamba nililiudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikariharibu
"Kweli, mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu Mnazareti;
Nami nikayafanya hayo Yerusalemu;
Niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na wakuu wa makuhani; na walipouawa nalitoa idhini yangu. Na mara nyingi katika masinagogi yote naliwaadhibu, nikawashurutisha kukufuru; nikawaonea hasira kama mwenye wazimu, nikawaudhi hata katika miji ya ugenini. Basi katika kazi hiyo nilipokuwa nikienda Dameski, mwenye mamlaka na maagizo ya wakuu wa makuhani ... nikasikia sauti ikisema nami kwa lugha ya kiebrania, Sauli! Sauli! Mbona waniudhi?
Ni vigumu kwako kuupiga mateke mchokoo."
Kitine lacks the moral high ground to be running his mouth like this....