- Kitine na Mkapa, Mwalimu's people tena damu damu, Mwalimu alipokuwa ana-retire akapelekwa Canada kula nchi, akilipiwa kila kitu na serikali yaani hela zetu walipa kodi anachokifanya hakieleweki, Mkapa kuwa rais tu akamuomba kurudi great friends akarudi, Mkapa akatumia ubabe na nguvu za ajabu within a month Kitine ni mbunge na waziri ofisi ya Mkapa, all this time hajaona ubovu wa uongozi wetu wala tatizo la integrity,
- The next thing Kitine anaota urais, ghafla kaanza kuvaa kanzu na barakashia bungeni, nini kaambiwa rais anayefuata Mkapa lazima awe Muisilamu, mara oooh mawaziri ni wala rushwa, haya Kitine tuambie majina yao, akadai oooh no waandishi wamekosea sikusema vile, next mke wake amechukua maelfu ya dola za walipa kodi kwenda kutibiwa nje, kumbe ameenda kuzifanyia shopping bila kwenda Hospital wala kwa Daktari yoyote huko Canada na wala haumwi chochote, sasa all this time Kitine haoni ubovu wala tatizo la integrity na uongozI wetu,
- The next thing Kitine amehonga honga na kujaribu kuzuia uchunguzi wa kamati ya bunge kuhusiana na wizi wa mkewe wa hela zetu walipa kodi alizotumia nje tena kwa uharibifu sana, wabunge kuja juu sana ndio Kitine baada ya kubanwa sana na wabunge kukubali kujiuzulu na kulazimishwa kulipa nusu ya zile pesa tena katika mazingara yaliyojaa uhuni uhuni, badala ya mkewe kwenda jela kwa wizi wa mchana wa hela zetu walipa kodi, all this time Kitine haoni matatizo ya uongozi wetu na integrity yake kua hovyo!
Sasa leo he is supposed to be a hero kwa sababu amesema maneno ya kuponda serikali ya CCM, akitukana ubovu ule ule uliomponya yeye na mkewe, sometimes huwa ninajiuliza hivi vita tunavyopigana na mafisadi, kwa mfano tukiwatoa mafisadi wote leo, eti ni kweli tutaweza kuweka viongozi wapya ambao hawatakuwa mafisadi? Ningeelewa kwamba Kitine sasa ameamua kwamba wananchi wa Tanzania wameonewa vya kutosha na kuweka mfano anataka mkewe afunguliwe mashitaka kwanza ya kuiba hela zetu walipa kodi huko nyuma maana sasa anataka to come clean, no sasa yeye na Mbilinyi ni mashujaa against uozo wa uongozi wetu uliowaponya.
Tuangalie sana ndugu zangu tusije kua kama wenzetu weusi huko US, kabla ya Obama kukosekana kwa real heros kuliwafanya kuanza kuamini hata yule Ferguson aliyeuwa wazungu kwenye LIIR Train bila sababu kuwa shujaa, badala ya a murdereeer!
Mungu Aibariki Tanzania!