Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

Kila atakayeusema vibaya utawala huu ataonekana shujaa tu. Mambo hayakuanza kuharibika leo. Taabu ya viongozi wetu wengi wa zamani wanayaona mabovu wakishawekwa kando.

Yote tisa wewe ndiye kumi.Umesema ukweli mtupu.
 
Kitine: Nchi sasa yaongozwa kienyeji

na Edward Kinabo
Tanzania Daima~Sauti ya watu​

MKURUGENZI Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk. Hassy Kitine, amesema taifa linakabiliwa na tatizo kubwa la uongozi, ambalo halijawahi kutokea katika historia ya nchi.

Kitine ambaye aliiongoza idara hiyo nyeti kwa karibu miaka 30 zama za Serikali ya Awamu ya Kwanza na ya Pili, alisema ukosefu huo wa uongozi umesababisha nchi iongozwe kienyeji.

Kachero huyo namba moja kwa miaka mingi, ambaye alilazimika kujiuzulu wadhifa wa uwaziri wa nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) wakati wa utawala wa Benjamin Mkapa, mwishoni mwa miaka ya 1990 kutokana na kuhusishwa na kashfa ya mkewe kufuja fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 40, alirejea kutoa kilio chake cha miaka mingi cha kuporomoka kwa maadili ya uongozi nchini.

Kitine ambaye aliwahi pia kuwa Mbunge wa Makete kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitoa matamshi hayo mazito katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa vyombo kadhaa vya habari.

“Hali tuliyofikia si nzuri, tena niseme ni mbaya sana. Kuna kuporomoka kwa kiasi kikubwa kwa maadili ya uongozi. Na hii nawaambia, nchi haijawahi kuwa katika hali mbaya huko nyuma kama ilivyo sasa. Kwa hali tuliyofikia, ni vigumu kurekebisha maadili ya uongozi.

“Tatizo kubwa ni viongozi kukosa integrity (uadilifu). Kwanza ni integrity ya viongozi wenyewe, pili ni commitment (wito), tatu ni nationalism (utaifa). Haya ndiyo yalikuwepo wakati wa Mwalimu,” alisema Dk. Kitine.

Akizungumza kwa kujiamini kama ilivyo kawaida yake, Kitine alisema viongozi wengi wa serikali wamepoteza sifa kuu tatu za uongozi ambazo ni kuwa na uadilifu, wito na kuweka mbele utaifa, sifa ambazo alisema ndizo zilikuwa nguzo ya uongozi wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, chini ya Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“That was possible (hilo liliwezekana) chini ya Mwalimu. Kama alikuwa akifanya kosa, basi kosa hilo lilikuwa likitokea tu wakati akifanya jambo kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania.

“Philosophy (falsafa) ya Mwalimu, ilikuwa kwanza Mungu, pili Tanzania, halafu yeye binafsi. Kila kiongozi anayetofautiana na Mwalimu tu hulifikisha taifa hili kubaya, if you differ with him, utaishia kubaya,” alisema Dk. Kitine akionyesha hali ya masikitiko.

Alisema uteuzi mbaya wa viongozi, hususan ule wa mawaziri, umechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa viongozi wasio waadilifu, wengi wao wakijihusisha na vitendo vya rushwa.

“Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao …sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).

“Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia,” alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote.

Kitine ambaye wakati wote wa mazungumzo yake alisema alikuwa anataka kujadili masuala muhimu na si watu, alieleza namna asivyo na imani na hatua zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na tatizo la rushwa kubwa.

Kwa mujibu wa kachero, mwanasiasa na mwanazuoni huyo, hatua hizo ambazo zinahusisha baadhi ya watu wenye majina makubwa kufikishwa mahakamani, zimechukuliwa kwa ajili tu ya maandalizi ya uchaguzi ujao.

“Nilikuwa kiongozi wa kwanza kuzungumzia rushwa kubwa miaka 10 iliyopita. Nilisema ndiyo inayovuruga uchumi kuliko hata rushwa ya nesi, hakimu, polisi,.… hakuna hata mkubwa mmoja aliyekamatwa. Ilinigharimu sana, na mimi nilipata adhabu ya kuzuiliwa kikao kwa miezi miwili, kama huyu nani huyu, Zitto (Kabwe). Wakati huo ilikuwa ndani ya CCM.

“Mimi nadhani hatua hizi zinazochukuliwa hazilengi kukomesha tatizo la rushwa, ni siasa tu za uchaguzi,” alisema Dk. Kitine.

Alipoulizwa nini kifanyike ili kukabiliana na tatizo hilo la uongozi mbaya, pamoja na mambo mengine, alielekeza changamoto zake kwa Idara ya Usalama wa Taifa.

“Usalama wa Taifa should be completely clean (unapaswa kuwa safi kabisa). Idara hii inatakiwa kuwa, juu ya mambo ya rushwa, iwe safi kabisa. Usalama wa Taifa ndiyo unayoteua viongozi, ndiyo inayoshirikiana na rais kwa kumshauri katika kuteua mawaziri. Sasa kama Usalama wa Taifa ukiwa mchafu ndio tunapata viongozi wala rushwa. Nafikiri vigezo vinavyotumika kuteua viongozi pia vina matatizo,” alisema Dk. Kitine.

Kada huyo wa CCM ambaye kitaaluma ni mchumi na mwanasheria, akizungumzia hali ya uchumi nchini, alisema kwa kiasi kikubwa uchumi umeshikiliwa na wageni kuliko wazawa, na kuelezea kusikitishwa kwake juu ya kuwepo kwa pengo kubwa kati ya matajiri na maskini.

Akitoa mfano alisema, miongoni mwa mambo yanayoonyesha kuparaganyika kwa mambo ni kukithiri kwa idadi ya ombaomba mitaani.

“Mwalimu asingeruhusu watu hawa waombeombe barabarani. Kazi za Watanzania ni udereva teksi, daladala, mabasi, kazi ya uboi ndani ya nyumba na kazi ya kufagia barabarani. Hizi ndizo kazi za Watanzania na hawa ndio wenye mali.

“Uchumi huu wa Watanzania si wa kwao. Watanzania ambao ni matajiri hawazidi hata watano. Hakuna sera bora za kusaidia kutumia maliasili zetu ili zitupe fedha ya kujenga shule, madaraja, hospitali…..” alisema Dk. Kitine.

Akizungumzia utendaji wa kazi wa Bunge katika kusimamia utendaji wa serikali, Kitine alisema kazi inayofanywa na taasisi hiyo hivi sasa ni kubwa kuliko ilivyopata kuwa wakati wowote huko nyuma.

Hata hivyo katika kuusifia utendaji wa kazi wa Bunge, aliupongeza mchango mkubwa na muhimu wa wabunge wa upinzani katika kuiimarisha taasisi hiyo muhimu.

“Ni Bunge zuri kuliko lilivyowahi kuwa huko nyuma. Linaonyesha kila dalili za uhuru. Upinzani unafanya kazi nzuri. Bunge liko wazi zaidi na wabunge wanatoa michango mingi yakinifu, yenye manufaa kwa taifa. Likiendelea hivi tutafika mahali pazuri,” alisema.
kitine hana jipya kabisa. ni muhanga wa kisiasa za kuwindana na kulindana na ameamua kuwa mfa maji. atueleze ana track record gani katika kuleta maendeleo hata kwa watu wa makete waliomwingiza bungeni na kuukwaa uwaziri aloupoteza gafla??

jamani magazeti ya ipp natumai nipashe pia yameripoti tofauti sana na hawa taz daima kuhusu kauli ya kitine jana.

kunani ipp media na mzee BEN???
 
Kila atakayeusema vibaya utawala huu ataonekana shujaa tu. Mambo hayakuanza kuharibika leo. Taabu ya viongozi wetu wengi wa zamani wanayaona mabovu wakishawekwa kando.

Hivi wakuu sasa hayo maovu ndani ya chama aachiwe nai kuyasema ? maana kila anyesema ana matope.
Katika viongozi wa Tanzania wa leo hakuna aliye safi, Mr Clean hayupo tena.
Ukweli unatabia moja ,haupingiki hata ukisemwa na shetani!
Bado aliyosema mzee Kitine yana ukweli ambao ni changamoto kwa utawala uliopo.
Ni bora tujisahihishe na tugange yajayo
 
- Mkuu wangu Kitine, amekuwa mkurugenzi wa usalama na waziri wa usalama, sasa kama kweli anataka kuja clean, basi kwanza aanze na mkewe, halafu aseme lugha inayoeleweka maana anajua mengi sana maovu kuliko anayoyasema na hasa wizi wake yeye mwenyewe wa hela zetu walipa kodi! Hivi mkuu katika uwaziri wake wa muda mfupi unajua amelimbikiza mali ngapi usije uakaangua kilio mkuu ukijua!
 
Big up Mzee Kitine endelea kukosoa vijana wenu wanaharibu kweli kweli, maadili inaonyesha hamkuwafundisha vizuri, hayo ni matokeo ya mtoto umleavyo................
 
- Mkuu wangu Kitine, amekuwa mkurugenzi wa usalama na waziri wa usalama, sasa kama kweli anataka kuja clean, basi kwanza aanze na mkewe, halafu aseme lugha inayoeleweka maana anajua mengi sana maovu kuliko anayoyasema na hasa wizi wake yeye mwenyewe wa hela zetu walipa kodi! Hivi mkuu katika uwaziri wake wa muda mfupi unajua amelimbikiza mali ngapi usije uakaangua kilio mkuu ukijua!

Sema tu mkuu FMES, sema tu JF.
uwanja wa ukweli, ikibidi kuwa huyu mzee naye aonyeshe mfano wa uadilifu so much the better.
Na ni vyema ikawa hivyo maana du pandora box ya wakuu wetu ni hatari!
 
- Mkuu wangu Kitine, amekuwa mkurugenzi wa usalama na waziri wa usalama, sasa kama kweli anataka kuja clean, basi kwanza aanze na mkewe, halafu aseme lugha inayoeleweka maana anajua mengi sana maovu kuliko anayoyasema na hasa wizi wake yeye mwenyewe wa hela zetu walipa kodi! Hivi mkuu katika uwaziri wake wa muda mfupi unajua amelimbikiza mali ngapi usije uakaangua kilio mkuu ukijua!

Pia atuoe solutions, haya anayoyasema kwa kiasi kikubwa kila mtu anayajua, tunataka solutions zinazotekelezeka, sio blahblah za kisiasa tulizozizoea. Anatuhumu kuwa yanayofanyika (kufikisha watu wakubwa mahakamani ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi), well, tunajuaje kuwa na anayoyasema yeye si maandalizi ya uchaguzi?
Anasema kuwa TISS imechafuka, nani ameichafua? Yeye lazima atajua kwa sababu ameshaiongoza idara hiyo. Inasafishwaje?
Kama anataka kutusaidia aachane na politicking na tirejee kwenye hoja za msingi
 
“Haiwezekani viongozi wakateuliwa kwa misingi ya mitandao …sijui, kwa msingi wa politics of division (siasa za makundi) ndani ya chama. Haiwezekani nchi ikaendeshwa kienyeji. Integrity should be number one (uadilifu unapaswa kuwa kitu cha kwanza kuzingatiwa).

“Mtu anajiuzulu, anafukuzwa uwaziri kwa sababu ya kashfa, kwa sababu ya kukosa maadili, halafu anabakia kuwa mbunge na mjumbe wa kamati kuu ya chama, nini hii? Hii haifai. Waziri akikosa uadilifu anatakiwa aondolewe mara moja nyadhifa nyingine zote alizobakiwa nazo. Nadhani hii itasaidia,” alisema Dk. Kitine pasipo kutaja jina la kiongozi yeyote.
Hata hivyo haya yote yametokea tangu serikali ya awamu ya pili na Dr.mwenyewe alikuwa kwenye system hadi alipojiuzuru wadhifa wake kwa kashfa Tshs 40M mali ya serikali.Tangu tukio hilo litokea hadi hivi leo ni muda mrefu umepita,na hakuzungumzia haya mambo ambayo kwa kiasi kikubwa ni sahihi.
Halafu,viongozi wengi wakitanzania wakiwa madarakani haya mambo hawazungumzi;na nina amini Dr.Kitine kama angekuwepo katika system hadi hivi leo asingeweza kusema hayo aliyoyasema au hata kurekebisha hayo aliyosema akishirikiana na wenzake.
 
Jamani kama kuna aliye msafi ajitokeze kumpiga Kitine mawe.

Kila mtu ana mapungufu yake, ila kupinga rushwa na ku challenge status quo ni muhimu hata kwa aliye mchafu!
 
Alichokisema Kitine ni sawa. Lakini na yeye anakumbuka kilichosababisha kutimuliwa kutoka Ukurugenzi na Nyerere ilikuwa ni issue ya kfisadi na mitumba ya magari ya 504? N kashfa ya wife wake? Hata hivyo tunafurahi kuwa anasema
 
Wanaompinga Kitine ni wale tu wasioitakia mema tanzania hasa mafisadi, marafiki zao na familiya zao.

Kitine kasema ukweli mtupu. Hasa kanifurahisha aliposema Bunge la sasa hivi linafanya kazi nzuri kuliko mabunge yote yaliyotangulia toka enzi za Mwalimu. Hongera Mh Sitta na wabunge wote wanaoweka mbele maslahi ya Taifa hasa wabunge wa kambi ya upinzani!

Big up Kitine! Big up Sitta! Big up kambi ya upinzani bungeni!
 
Huyu jamaa anajua kuweka dongo pahala pake, jambo ambalo kila siku hapa huwa nalikumbusha kuwa wapinzani waisakame serikali na sio kumsakama mtu mmoja mmoja kwani kutumia kumsakama mmoja mmoja hakuna faida kisiasa zaidi ya kupigwa goli mbele ya wananchi na hapo ndipo Wananchi wanapokuoneni hamna jipya ambalo litaihangaisha serikali na kujiona haifai na hata kufikia kuachia ngazi.

Ya kubomolewa na kupondwa ni serikali tu ,kila mkikutana na wananchi basi iwe ni kuiponda serikali ,yaani mwisho serikali itashindwa kuvumilia ndipo hapo mtakapoona viongozi wa upinzani wanakamatwa kamatwa na kufunguliwa kesi hazina kichwa wala miguu.

Kitine ameiponda serikali nzima hakuchagua mtu mmoja mmoja ,ni mfano wa polisi wa kuzuia fujo akifika sehemu ambayo anapaswa kuzuia fujo huwa hachagui ni rungu tu na pata shika mpaka amehakikisha watu wote wamechawanyika na hapo ndio hukamata wale wa kuwafungulia kesi iwe wamehusishwa na kuanzisha fujo.

Hivyo alichofanya Kitine hakuchagua ameiponda serikali nzima na Chama chake tawala mtindo mmoja ,na utaona hata wasomaji hapa wameunga mkono maneno yake ndio hivyo hivyo kwa wananchi utakapowasomea makaburasha ya ufisadi Katiba na mambu mengine kwa kuishirikisha serikali basi hakikisha ,watu wataihama serikali na kuiona haina maana kabisa ndivyo ilivyo.

lakini kwa kufichua ufisadi na kumsaka mtu mmoja mmoja hatufiki mbali tutakwama tu.
 
FMES

Huyu Kitine is another has-been. Hakuwa karibu na Mwalimu wala BWM. Mwalimu alimfukuza kazi UWT period mtu yoyote asikundanganye. Ndio sababu ya yeye kwenda Canada na inabidi ishukuru serikali kwa kumsomesha hio PHD yake. Alafu kitu kingine Kitine alikuwa anategemea kwamba kwenye lile soo la mke wake BWM angemsaidia. Haikutokea. The lobbying he did to become minister in 1995 was enough to annoy everyone. Ndio maana BWM alimtosa the first chance he got. Jamaa is bitter with the system. This guy had the audacity to think he could run for President in 2005. What a Joke! The rest of what you said is spot-on.
 
This is rubbish!!! completely escaping to comment on the message given by kitine, if his message real reflects the situation our country is facing now!! resorting to personal attack!! I dont think if people do need to hear such words!!
 
Mimi naona ni wimbo ule ule ambo umekuwa ukiimbwa na wanasiasa ambao ni victimis wa siasa za mgawanyo. Siasa za mtandao na asili zimewaumiza hawa waheshimiwa na sasa hivi wameanza kupigana madongo hadharani. Yeye kama mwanauslama mwandamizi kwanini anazungumzia uozo wa usalama, chama na serikali gazetini? Kwani anashindwa kumface RO na kumueleza, nini kinamzuia kumface JK na kumuambia hili mpaka awaambie watanzania ambao hawajui what is actually at stake? Anataka kutuambia usalama umeanza kuwa ovyo leo? Mbona katika utawala wote wa Mzee ruksa usalama ulikuwa ovyo zaidi kuliko hata sasa, why didn't he say then and say now.
 
we are busy attacking kitine as an individual instead of analysing what he just said...former viongozi wa ccm whether wasafi au wachafu wakianza kuponda chama chao chenye usiri its a good sign from all angles (its a step towards the same goals we all want here..good governance, accountability and transparency)..tusubiri wengi wataongea mwaka huu...

to me this is good news..
field marshall kitine sio mpumbavu kuita waandishi wakati anajua kabisaa aliyoyafanya yeye wakati akiwa waziri na uwt sio siri especially kwa waandishi (keep that in mind when ur busy attacking his past actions na za mkewe)
 
Mimi naona ni wimbo ule ule ambo umekuwa ukiimbwa na wanasiasa ambao ni victimis wa siasa za mgawanyo. Siasa za mtandao na asili zimewaumiza hawa waheshimiwa na sasa hivi wameanza kupigana madongo hadharani. Yeye kama mwanauslama mwandamizi kwanini anazungumzia uozo wa usalama, chama na serikali gazetini? Kwani anashindwa kumface RO na kumueleza, nini kinamzuia kumface JK na kumuambia hili mpaka awaambie watanzania ambao hawajui what is actually at stake? Anataka kutuambia usalama umeanza kuwa ovyo leo? Mbona katika utawala wote wa Mzee ruksa usalama ulikuwa ovyo zaidi kuliko hata sasa, why didn't he say then and say now.

Kwa hiyo akiongea na RO au JK watanzania hawapaswi kujua kama mambo yanakwenda mrama!

Mbona unamchagulia namna ya kutoa ujumbe!
 
Kwa hiyo akiongea na RO au JK watanzania hawapaswi kujua kama mambo yanakwenda mrama!

Mbona unamchagulia namna ya kutoa ujumbe!

Mkuu, huyu mheshimiwa ana haki ya kuto ujumbe popote anapopenda. Lakini ukiangalia caliber yake hakuwa mtu wa kwenda kwenye magazeti na kuanza kuongea uozo wa serikali, chama a usalama wa taifa. Akiwa ni insider anatakiwa kurekebisha mambo kupitia channels. Linalonifanya niweke viulizo, mbali na kuita waandishi wa habari na kuwaambia kitu ambacho watanzania kwa sasa tunajua, kwa nini anasema leo na sio jana, na kwanini vyombo vya habari? Au anataka kujifanya yeye ndio msafi na muadilifu kuliko hao anaowakemea kwenye vyombo vya habari?
Uozo mwingi na dhuluma tulizofanyiwa na serikali yeye anazijua fika, na anajuakuwa hazikuanza na serikali ya sasa. Kwanini asiseme toka zamani?
 
wazee wamechoka
ila hekima wanayo
maozo wanayaona
ndio maana wanayasemea
wanamwambia nani?
huenda ni ujumbe kwa vijana
maana mnazo nguvu
wajibu wa vijana basi;
do something
 
Tukubaliane just for the sake of argument:

a. Mke wa Kitina aliwahi kuhusishwa na vitendo vya kifisadi never prosecuted.
b. Kitine alitaka kuwa Waziri sana hakupewa nafasi
c. Kitine bado ana machungu ya kuwekwa pembeni
d. Kitine naye ni fisadi (I'll go to that extreme).

Sasa:

a. Hoja zake juu ya tatizo la uongozi uliopo sasa hivi zina nguvu yoyote?
b. Je mtazamo wake kuhusu wajibu wa Usalam wa Taifa ni sahihi?
c. Assessment yake ya siasa za makundi ndani ya chama zina mantiki yoyote?
d. Je, kuna jambo lolote ambalo amelisema ambalo lina chembe ya ukweli au yote ni fabrication of his bitter mind?
 
Back
Top Bottom