Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Wabongo vigeugeu sana!Maneno miingi! Juzi tu ndo hawahawa walitaka mfumo wa zamani urudishwe.Sasa hivi umerudishwa hawataki tena!Wanataka makongamano ya kujadili kwanini urudishwe,halafu mwisho wa siku ndo wakubali!Acheni uswahiliswahili!!
 
First nilikua sijui huu mfumo wa GPA kumbe upo nchi nyiingi tu

kumbe tatizo sio mfumo
tatizo ni viwango vya ufaulu

Kuna tatizo lingine Ndalichako halizungumzi kabisa

kuondolewa kwa vitabu bora kama vya Shaaban Robert kwenye mtaala
na kupachikwa vitabu vya kina Shigongo

na la wabunge ku lobby vitabu vyao viingizwe kwenye mtaalaa
hatari sana
 
Mpaka sasa ukiniambia nitetee uamuzi wa waziri wa elimu Mh Joyce Ndalichako wa kufuta mfumo wa GPA na kurudisha ule wa madaraja yaani DEVISION siwezi nikawa na sababu za msingi hasa kwani sipo kwenye akili yake ninachokiona ni muendelezo wa viongozi wa nchi hii kupinduapindua mambo kwa matakwa yao pasi kuushirikisha umma, alichokifanya Ndalichako amekifanya katika namna ileile aliyoitumia Mtangulizi wake kufuta mfumo wa devision na kuuleta huu wa GPA, The issue supposed to be submitted to public debate in order to come with a good and suitable solution to the extent that one can defend the decision with reasonable arguments, hii ingejenga msingi imara na kwamba yeyote ajaye na kutaka kuover rule atapaswa ajipange kwa sababu hasa za kwanini anataka kubadili mfumo! I am willing to concur with Professor Kitila Mkumbo herein. "
Hili la upangaji wa madaraja ya kufaulu (grading system) linapaswa kutufurahisha kidogo, na kutuudhi sana!
Miaka mitatu iliyopita serikali ilipoleta pendekezo la kubadili mfumo wa madaraja ya ufaulu katika elimu msingi baadhi yetu tulipinga. Kimsingi wataalamu wote wa elimu tulipinga hili jambo. Tulipinga kwa sababu tulibaini nia ovu ya serikali katika jambo hili. Nia yenyewe ni ukweli kwamba serikali ilikuwa inatafuta namna ya kuficha aibu ya wanafunzi wa kidato cha nne kuendelea kufeli katika mitihani ya mwisho. Kufikia mwaka 2012 zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa walifeli mitihani ya kidato cha nne. Kilio cha umma kilikuwa kikubwa. Kwa kutambua kwamba ilikuwa haina muujiza wa kurekebisha hili, huku tukielekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kwa kutaka kuepuka kuadhibiwa na wananchi katika sanduku la kura, serikali ikaibuka na uamuzi wa kubadili mfumo wa kupanga madaraja. Ndiyo ikaja na huu mfumo wa GPA. Na kwa kweli mara baada ya kubadili mfumo wa kufaulu, ghafka kiwango cha kufaulu kikapanda katika mitihani ya mwaka 2013 na 2014 na serikali kupitia kwa Waziri Kawambwa ikaanza kujivunia mafanikio katika elimu. Wenye akili tulicheka vicheko vya kubeza!
Kwa hiyo uamuzi wa Profesa Joyce Ndalichako (WEST) wa kurudi katika mfumo wa zamani wa Division ni wa kupongezwa kwa kiasi fulani kwa upande mmoja, lakini pia ni uamuzi unaouudhi kwa upande mwingine, kama nitakavyoeleza hapa chini.
Kimsingi mfumo wa GPA sio mbaya kama mfumo. Nchi nyingi duniani zinatumia mfumo huu wa GPA. Tatizo la kwetu ni kwamba tulishusha viwango vya kufaulu. Hili ndilo tatizo la msingi, lakini sio mfumo wenyewe wa GPA. Naamini Prof. Ndalichako analijua vizuri jambo hili kwa kuwa yeye ni mtaalamu mahiri wa upimaji katika elimu (educational assessment) na uzoefu wa miaka takribani nane ya kuendesha Baraza letu la mitihani.
Uamuzi wa Profesa Ndalichako unaudhi kwa sababu unatukumbusha machungu ya Ndugu Mungai aliyebadili mitaala kibabe bila sababu za msingi za kitafiti na kisayansi, wala kushirikisha wadau wa elimu. Leo mwalimu wangu Prof. Ndalichako amebadili mfumu huu bila mjadala wowote mpana kitaifa. Hakuna taarifa ya kitafiti. Hakuna uchambuzi yakinifu. Hakuna Kamati ya Bunge iilyokaa na kujadili. Hatujui waziri mwingine atakayekuja miaka miwili, mitatu, mitano au kumi ijayo atakuja na nini. Hili ni jambo linalotisha katika nchi inayofanya bidii ya kujenga demokrasia na mfumo wa utawala bora. Hata kama uamuzi ni mzuri kiasi gani lakini mfumo wa kufanya maamuzi unaacha ukakasi mkubwa mno. Kwa mtindo wetu wa kufanya maamuzi tunakuwa nchi isiyotabirika wala kuaminika. Tutakuwa na maswali ya kujibu kila siku tunapohusiana na wenzetu katika mataifa mengine. Miaka miwili iliyopita tumekuwa na kazi ya kuwaeleza wenzetu katika nchi nyingine kwamba tulibadili mfumo wetu wa madaraja ya kufaulu na sasa tunatumia GPA. Sasa siku chache zijazo tutaanza tena kuwaambia wenzetu kwamba ooh samahanini tumebadili tena na sasa tunarudi kule kwa zamani. Ebo!!
Tusikubali kuzoea mambo makubwa kama haya yafanywe na mtu mmoja mwenye dhamana au serikali peke yake. Mambo haya yaanze na uchambuzi wa kisayansi, yafuatiwe na mjadala wa kitaifa na maamuzi ya mwisho yafanywe na Bunge au Kamati husika ya Bunge baada ya serikali kuyawasilisha na kushawishi. Ni sahihi kabisa kwa waziri kuwa na mawazo na mapendekezo yake ya kisera. Lakini si sahihi waziri peke yake kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa ya kutuathiri na kuathiri nchi leo na kesho. Kazi kubwa ya waziri iwe ni kuibua sera na kushawishi ubora wa sera husika lakini uamuzi wake lazima ufuate mkondo mpana wa kitaifa ili hatimaye uamuzi huo tuweze kuumbatia wote kama taifa bila ukakasi. Ifike mahala tuimarishe nguvu za kitaasisi na kimfumo katika maamuzi ya kisera badala ya kutegemea nguvu za mwanasiasa mmoja mmoja mwenye madaraka".

Kitila, hapana. Hilo la mjadala litafanyika baadaye. Sio sasa ambapo watoto wanategemea matokeo ya mtihani muda mfupi ujao. Anaepuka watoto kudanganywa kuwa wamefaulu kama ulivyosema. Prof, just think as bit!
 
Nimepata kichefuchefu unaposema eti kamati ya Bunge ijadili. Wale wenye sifa za kujua kusoma ma kuandika? Pytuuuuuuuu
 
Eti nini? Huyu si ndio leprofeseri?
 
Attachments

  • IMG_20160122_192436.jpg
    IMG_20160122_192436.jpg
    101.1 KB · Views: 30
Kitila nae anazingua tu. Watu siku hizi wanajua umaarufu ni kiongeaongea hovyo.. Nonsense
 
Kwa mawazo yangu kitila yupo sahihi,
Kwa sababu kile kilichopelekea wakabadili mfumo bado hakijapata majawabu ya kutosha,kama kungekuwa na mjadala wa kitaifa ingesaidia kutafuta majawabu juu kile kilichotokea hadi kuitia aibu serikali kwa kuzalisha zilo nyingi.

Ninachokiona Ndalichako kama Wazili mwenyewe dhamana ya elimu amejiandaa kuwa na uso mugumu usio na aibu.
Kwani ile aibu iliyoikumba serikali kwa kudhalisha zilo nyingi iko njiani inakuja.
Kwani sidhani kama kuna mikakati ya kuridhisha kuinua kiwango cha ufaulu kwa shule za uma.
 
Mpaka sasa ukiniambia nitetee uamuzi wa waziri wa elimu Mh Joyce Ndalichako wa kufuta mfumo wa GPA na kurudisha ule wa madaraja yaani DEVISION siwezi nikawa na sababu za msingi hasa kwani sipo kwenye akili yake ninachokiona ni muendelezo wa viongozi wa nchi hii kupinduapindua mambo kwa matakwa yao pasi kuushirikisha umma, alichokifanya Ndalichako amekifanya katika namna ileile aliyoitumia Mtangulizi wake kufuta mfumo wa devision na kuuleta huu wa GPA, The issue supposed to be submitted to public debate in order to come with a good and suitable solution to the extent that one can defend the decision with reasonable arguments, hii ingejenga msingi imara na kwamba yeyote ajaye na kutaka kuover rule atapaswa ajipange kwa sababu hasa za kwanini anataka kubadili mfumo! I am willing to concur with Professor Kitila Mkumbo herein. "
Hili la upangaji wa madaraja ya kufaulu (grading system) linapaswa kutufurahisha kidogo, na kutuudhi sana!
Miaka mitatu iliyopita serikali ilipoleta pendekezo la kubadili mfumo wa madaraja ya ufaulu katika elimu msingi baadhi yetu tulipinga. Kimsingi wataalamu wote wa elimu tulipinga hili jambo. Tulipinga kwa sababu tulibaini nia ovu ya serikali katika jambo hili. Nia yenyewe ni ukweli kwamba serikali ilikuwa inatafuta namna ya kuficha aibu ya wanafunzi wa kidato cha nne kuendelea kufeli katika mitihani ya mwisho. Kufikia mwaka 2012 zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa walifeli mitihani ya kidato cha nne. Kilio cha umma kilikuwa kikubwa. Kwa kutambua kwamba ilikuwa haina muujiza wa kurekebisha hili, huku tukielekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kwa kutaka kuepuka kuadhibiwa na wananchi katika sanduku la kura, serikali ikaibuka na uamuzi wa kubadili mfumo wa kupanga madaraja. Ndiyo ikaja na huu mfumo wa GPA. Na kwa kweli mara baada ya kubadili mfumo wa kufaulu, ghafka kiwango cha kufaulu kikapanda katika mitihani ya mwaka 2013 na 2014 na serikali kupitia kwa Waziri Kawambwa ikaanza kujivunia mafanikio katika elimu. Wenye akili tulicheka vicheko vya kubeza!
Kwa hiyo uamuzi wa Profesa Joyce Ndalichako (WEST) wa kurudi katika mfumo wa zamani wa Division ni wa kupongezwa kwa kiasi fulani kwa upande mmoja, lakini pia ni uamuzi unaouudhi kwa upande mwingine, kama nitakavyoeleza hapa chini.
Kimsingi mfumo wa GPA sio mbaya kama mfumo. Nchi nyingi duniani zinatumia mfumo huu wa GPA. Tatizo la kwetu ni kwamba tulishusha viwango vya kufaulu. Hili ndilo tatizo la msingi, lakini sio mfumo wenyewe wa GPA. Naamini Prof. Ndalichako analijua vizuri jambo hili kwa kuwa yeye ni mtaalamu mahiri wa upimaji katika elimu (educational assessment) na uzoefu wa miaka takribani nane ya kuendesha Baraza letu la mitihani.
Uamuzi wa Profesa Ndalichako unaudhi kwa sababu unatukumbusha machungu ya Ndugu Mungai aliyebadili mitaala kibabe bila sababu za msingi za kitafiti na kisayansi, wala kushirikisha wadau wa elimu. Leo mwalimu wangu Prof. Ndalichako amebadili mfumu huu bila mjadala wowote mpana kitaifa. Hakuna taarifa ya kitafiti. Hakuna uchambuzi yakinifu. Hakuna Kamati ya Bunge iilyokaa na kujadili. Hatujui waziri mwingine atakayekuja miaka miwili, mitatu, mitano au kumi ijayo atakuja na nini. Hili ni jambo linalotisha katika nchi inayofanya bidii ya kujenga demokrasia na mfumo wa utawala bora. Hata kama uamuzi ni mzuri kiasi gani lakini mfumo wa kufanya maamuzi unaacha ukakasi mkubwa mno. Kwa mtindo wetu wa kufanya maamuzi tunakuwa nchi isiyotabirika wala kuaminika. Tutakuwa na maswali ya kujibu kila siku tunapohusiana na wenzetu katika mataifa mengine. Miaka miwili iliyopita tumekuwa na kazi ya kuwaeleza wenzetu katika nchi nyingine kwamba tulibadili mfumo wetu wa madaraja ya kufaulu na sasa tunatumia GPA. Sasa siku chache zijazo tutaanza tena kuwaambia wenzetu kwamba ooh samahanini tumebadili tena na sasa tunarudi kule kwa zamani. Ebo!!
Tusikubali kuzoea mambo makubwa kama haya yafanywe na mtu mmoja mwenye dhamana au serikali peke yake. Mambo haya yaanze na uchambuzi wa kisayansi, yafuatiwe na mjadala wa kitaifa na maamuzi ya mwisho yafanywe na Bunge au Kamati husika ya Bunge baada ya serikali kuyawasilisha na kushawishi. Ni sahihi kabisa kwa waziri kuwa na mawazo na mapendekezo yake ya kisera. Lakini si sahihi waziri peke yake kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa ya kutuathiri na kuathiri nchi leo na kesho. Kazi kubwa ya waziri iwe ni kuibua sera na kushawishi ubora wa sera husika lakini uamuzi wake lazima ufuate mkondo mpana wa kitaifa ili hatimaye uamuzi huo tuweze kuumbatia wote kama taifa bila ukakasi. Ifike mahala tuimarishe nguvu za kitaasisi na kimfumo katika maamuzi ya kisera badala ya kutegemea nguvu za mwanasiasa mmoja mmoja mwenye madaraka".[/QUOT/ Huyo Kitila kachemka, hamna haja ya kuweka mijadara wakati hii ndiyo system tuliyokuwa na nayo na ndiyo imetoa watu ambao ni compitent.
Na siyo hii inayoficha sufuri.

Mwambie kitila aweke siasa mbeni tuna imani ni Ndalichako.
 
Mimi nadhani wadau wasitumie muda mwingi kumshambulia Prof Kitila Mkumbo badala yake waangalie mzizi wa hoja.....

Hofu ya Watanganyika sio kuacha GPA na kufuata division ni kwa jinsi huo mfumo wa GPA ulivyokuwa unaendeshwa kwa kupunguza viwango vya ufaulu ili wanafunzi waonekane wamefaulu ilhali wana uwezo mdogo sana.....

Pamoja na Waziri wa elimu kuuondoa mfumo wa GPA lakini pia aangalie na viwango vya ufaulu...ili kupata wahitimu wenye tija kwa taifa na ikiwezekana dunia kwa ujumla...
 
Kitu cha kipumbavu huna haja ya kutafuta maoni ya wananchi!!!
 
wao n
Profesa hajakosea kumkosoa mama Ndalichako, nadhani anakubaliana naye, sasa kama vipi wananchi waulizwe kuwa wanataka mgumo upi?
Ila thuu wa division wakati unaendelea ndio wananchi na wadau mbali mbali waulizwe, wasisikilize vilio vya mashehe misikitini
wao ndio wataalam nashangaa mnataka kuwapa uwezo huu wananchi ambao hawajui a wala b. sio sahihi hata kidogo. mnataka mfanye maamuzi ya kitaalam kwa kutumia mihemko ya wananchi. sio sawa kabisa! !! acheni wataalam wafanye kazi yao.
wataalam waliokuwepo waliulizwa nini sababu za kutoka katika mfumo wa zamani na kuanzisha huu mpya wa GPA. halikupatikana jibu kutoka kwa wataalam hao wakina Dr Msonde. sasa kama ni hivyo wananchi mnataka kuwaangushia zigo wasilolifaham? ?? sio sawa
 
Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
Kaka huyu prof. Mkumbo usimfuate sana ni mwanasiasa (active) hivyo hawezi kuwa objective lazima hivyo alivyo awe hivyo
 
Division four ilizarauliwa sana na kuonekana ni daraja dhaifu kwa mwanafunzi aliyepata na kuonekana hana akili na hafai kuendelea mbele,jamii ikawa na mtazamo huo.GPA ilipoletwa ilivuruga kabisa mtazamo huo.
 
prof unasema bunge lishirikishwe bunge lenyewe limejaa wakina nape unazani watashauri nini.Mtu kama maji marefu what do you expect in bunge
zamani wakati wa mfumo wa div,katika wanafunzi 80 wanaofaulu walikuwa hawazidi 10,lakini walipopanua goli na kuweka gpa weeeee!wanafaulu 79 anafeli 1.wengine hata majina kuandika hawajui lakini wamefaulu
 
GPA ni jipu kama hao watoto wao wanaowasomesha shule za.kimataifa.hawaelewi msiiharibu elimu yetu. Hata wale waliopita.kwa mfumo huo wapangwe upya.
 
GPA ni sawa na kuongeza ukubwa wa goli ili mpiga penalt afunge kwa urahisi.
 
GPA ni sawa na kuongeza ukubwa wa goli ili mpiga penalt afunge kwa urahisi.
Tatizo sio mfumo wa GPA, kimsingi mfumo wa GPA ndo mfumo international, nchi nyingi hawaujui mfumo wa division, na kama issue ni kupanua goli hata mkiwa na mfumo wa division mtapanua tu, division haizuii kutopanuliwa goli lama serikali au necta walitaka
 
Back
Top Bottom