Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Sifikiri kama serikali inaweza kuacha watu eti watu wafaulu tu ipate sifa ya muda,kwani mtunga sera ni nani?
 
Hivi kuwambia watu warudishe mfumo wa zamani kwa kuwa uliopo hauna tija ni mihemko? Nikwambie tuu mfumo wa GPA kamwe haufai kwa muundo wetu wa elimu ya chini..zaidi unatumika kuwabeba watu kwa marks za kupewa bure na walimu wao....hakuna chombo cha kupima kama kweli hizo marks za maendeleo wanazopewa ni halali...mfumo huo ni wakuwapumbaza watu tuu!

Kama kweli walikuwa na sababu za msingi wasinge weza kushindwa hata kuuelezea kisayansi hata siku hiyo hiyo waliyo pewa tasks!

Yani tuchukue mfumo kisa tuu unatumika na nchi nyingine? Je tunaweza kumonitor alama za maendeleo wanazo pewa wanafunzi?
wewe GPA unaielewaje(elezea ubaya wake)?,niambie uzuri wa division!,kivipi walimu wanatoa alama za bure?majibu aliyopewa na NECTA umeyaona?unahisi angeuboresha mfumo wa GPA bado usingefaa?.unakumbuka alivyokuwa anamshurutisha katibu matendaji amtaje kwa jina aliyeleta mfumo wa GPA!unajua ni kwa nini?.ipo haja ya kupata sera ya Elimu ambayo haitaruhusu mihemko hii kutokea,kwasababu haiwezekani katika nchi ya kidemokrasia mambo yaende kienyeji namna hii.
 
Hakuna sababu ya kutumia gharama kubwa kwa matokeo yale yale !!
Go on Prof. Ndalichako
^^
 
Prof. Ndalichako amerejesha mfumo wa zamani uliobadilishwa bila utafiti wala ushirikishi wa wadau. Prof. Ndalichako ameirudisha wizara kwenye ground zero au back to square one ili ijipange kutafuta mfumo mpana wa kupima ufaulu wa watahiniwa katika ngazi mbali za elimu. Mfumo utakaopatika sharti utokane na utafiti ambao matokeo yake yaongoze mjadala shirikishi wa kitafa. Waziri alichokiuka ni kutoa agizo badala kanuni na kuzitangaza kwenye gazeti la serikali. It can be done retrospectively
kumbe kuna kanuni za kufuata?ikiwa necta hawatotii maagizo yake itakuwaje?
 
Prof Kitila kazi yake si utafiti? aende sasa akafanye research mfumo upi ni bora na unaopendwa na jamii, coz kwa sasa hata yeye hana base ya kumlaumu waziri ambaye kimsingi alichofanya ni ku restore mfumo wa zamani. Mfano kwa kufuatilia comments mbalimbali za jamii wengi wanaunga mkono uamuzi wa waziri.
Profesa hajakosea kumkosoa mama Ndalichako, nadhani anakubaliana naye, sasa kama vipi wananchi waulizwe kuwa wanataka mgumo upi?
Ila thuu wa division wakati unaendelea ndio wananchi na wadau mbali mbali waulizwe..
 
Mfumo wa GPA ni international standard hapa cha kufanya wangerekebisha zile point zilizokuwa za division zitumike kwenye huu mfumo wa GPA. Kuwa na passmark limit watopata chini ya hapo wahesabiwe failures. Grading iwe ktk distinction, merit, credid na pass na fail badala ya division. That's my opinion
 
Mpaka sasa ukiniambia nitetee uamuzi wa waziri wa elimu Mh Joyce Ndalichako wa kufuta mfumo wa GPA na kurudisha ule wa madaraja yaani DEVISION siwezi nikawa na sababu za msingi hasa kwani sipo kwenye akili yake.

Ninachokiona ni muendelezo wa viongozi wa nchi hii kupinduapindua mambo kwa matakwa yao pasi kuushirikisha umma, alichokifanya Ndalichako amekifanya katika namna ileile aliyoitumia Mtangulizi wake kufuta mfumo wa devision na kuuleta huu wa GPA.

The issue supposed to be submitted to public debate in order to come with a good and suitable solution to the extent that one can defend the decision with reasonable arguments, hii ingejenga msingi imara na kwamba yeyote ajaye na kutaka ku over rule atapaswa ajipange kwa sababu hasa za kwanini anataka kubadili mfumo!

I am willing to concur with Professor Kitila Mkumbo herein;

Hili la upangaji wa madaraja ya kufaulu (grading system) linapaswa kutufurahisha kidogo, na kutuudhi sana!

Miaka mitatu iliyopita serikali ilipoleta pendekezo la kubadili mfumo wa madaraja ya ufaulu katika elimu msingi baadhi yetu tulipinga.

Kimsingi wataalamu wote wa elimu tulipinga hili jambo. Tulipinga kwa sababu tulibaini nia ovu ya serikali katika jambo hili. Nia yenyewe ni ukweli kwamba serikali ilikuwa inatafuta namna ya kuficha aibu ya wanafunzi wa kidato cha nne kuendelea kufeli katika mitihani ya mwisho. Kufikia mwaka 2012 zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa walifeli mitihani ya kidato cha nne. Kilio cha umma kilikuwa kikubwa.

Kwa kutambua kwamba ilikuwa haina muujiza wa kurekebisha hili, huku tukielekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kwa kutaka kuepuka kuadhibiwa na wananchi katika sanduku la kura, serikali ikaibuka na uamuzi wa kubadili mfumo wa kupanga madaraja. Ndiyo ikaja na huu mfumo wa GPA. Na kwa kweli mara baada ya kubadili mfumo wa kufaulu, ghafla kiwango cha kufaulu kikapanda katika mitihani ya mwaka 2013 na 2014 na serikali kupitia kwa Waziri Kawambwa ikaanza kujivunia mafanikio katika elimu. Wenye akili tulicheka vicheko vya kubeza!

Kwa hiyo uamuzi wa Profesa Joyce Ndalichako (WEST) wa kurudi katika mfumo wa zamani wa Division ni wa kupongezwa kwa kiasi fulani kwa upande mmoja, lakini pia ni uamuzi unaouudhi kwa upande mwingine, kama nitakavyoeleza hapa chini.

Kimsingi mfumo wa GPA sio mbaya kama mfumo. Nchi nyingi duniani zinatumia mfumo huu wa GPA. Tatizo la kwetu ni kwamba tulishusha viwango vya kufaulu. Hili ndilo tatizo la msingi, lakini sio mfumo wenyewe wa GPA. Naamini Prof. Ndalichako analijua vizuri jambo hili kwa kuwa yeye ni mtaalamu mahiri wa upimaji katika elimu (educational assessment) na uzoefu wa miaka takribani nane ya kuendesha Baraza letu la mitihani.

Uamuzi wa Profesa Ndalichako unaudhi kwa sababu unatukumbusha machungu ya Ndugu Mungai aliyebadili mitaala kibabe bila sababu za msingi za kitafiti na kisayansi, wala kushirikisha wadau wa elimu.

Leo mwalimu wangu Prof. Ndalichako amebadili mfumu huu bila mjadala wowote mpana kitaifa. Hakuna taarifa ya kitafiti. Hakuna uchambuzi yakinifu. Hakuna Kamati ya Bunge iilyokaa na kujadili. Hatujui waziri mwingine atakayekuja miaka miwili, mitatu, mitano au kumi ijayo atakuja na nini. Hili ni jambo linalotisha katika nchi inayofanya bidii ya kujenga demokrasia na mfumo wa utawala bora.

Hata kama uamuzi ni mzuri kiasi gani lakini mfumo wa kufanya maamuzi unaacha ukakasi mkubwa mno. Kwa mtindo wetu wa kufanya maamuzi tunakuwa nchi isiyotabirika wala kuaminika. Tutakuwa na maswali ya kujibu kila siku tunapohusiana na wenzetu katika mataifa mengine.

Miaka miwili iliyopita tumekuwa na kazi ya kuwaeleza wenzetu katika nchi nyingine kwamba tulibadili mfumo wetu wa madaraja ya kufaulu na sasa tunatumia GPA. Sasa siku chache zijazo tutaanza tena kuwaambia wenzetu kwamba ooh samahanini tumebadili tena na sasa tunarudi kule kwa zamani. Ebo!

Tusikubali kuzoea mambo makubwa kama haya yafanywe na mtu mmoja mwenye dhamana au serikali peke yake. Mambo haya yaanze na uchambuzi wa kisayansi, yafuatiwe na mjadala wa kitaifa na maamuzi ya mwisho yafanywe na Bunge au Kamati husika ya Bunge baada ya serikali kuyawasilisha na kushawishi.

Ni sahihi kabisa kwa waziri kuwa na mawazo na mapendekezo yake ya kisera. Lakini si sahihi waziri peke yake kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa ya kutuathiri na kuathiri nchi leo na kesho.

Kazi kubwa ya waziri iwe ni kuibua sera na kushawishi ubora wa sera husika lakini uamuzi wake lazima ufuate mkondo mpana wa kitaifa ili hatimaye uamuzi huo tuweze kuumbatia wote kama taifa bila ukakasi.

Ifike mahala tuimarishe nguvu za kitaasisi na kimfumo katika maamuzi ya kisera badala ya kutegemea nguvu za mwanasiasa mmoja mmoja mwenye madaraka".
IMG-20160123-WA0002.jpg
JPM hana budi kuunda tume ichunguze aina ya Uprofesa alionao Kitila
 
Inabidi baadhi ya vitu viwekwe kama Dogma katika nchi hii.

Baadhi ya mifumo hasa wa elimu unatakiwa uwe sticky na kila kiongozi akiingia aufuate.

Haya mambo ya kubadilibadili sio ishu, tunaharibu kizazi.
 
Back
Top Bottom