Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Decree Holder

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,556
3,741
Mpaka sasa ukiniambia nitetee uamuzi wa waziri wa elimu Mh Joyce Ndalichako wa kufuta mfumo wa GPA na kurudisha ule wa madaraja yaani DEVISION siwezi nikawa na sababu za msingi hasa kwani sipo kwenye akili yake.

Ninachokiona ni muendelezo wa viongozi wa nchi hii kupinduapindua mambo kwa matakwa yao pasi kuushirikisha umma, alichokifanya Ndalichako amekifanya katika namna ileile aliyoitumia Mtangulizi wake kufuta mfumo wa devision na kuuleta huu wa GPA.

The issue supposed to be submitted to public debate in order to come with a good and suitable solution to the extent that one can defend the decision with reasonable arguments, hii ingejenga msingi imara na kwamba yeyote ajaye na kutaka ku over rule atapaswa ajipange kwa sababu hasa za kwanini anataka kubadili mfumo!

I am willing to concur with Professor Kitila Mkumbo herein;

Hili la upangaji wa madaraja ya kufaulu (grading system) linapaswa kutufurahisha kidogo, na kutuudhi sana!

Miaka mitatu iliyopita serikali ilipoleta pendekezo la kubadili mfumo wa madaraja ya ufaulu katika elimu msingi baadhi yetu tulipinga.

Kimsingi wataalamu wote wa elimu tulipinga hili jambo. Tulipinga kwa sababu tulibaini nia ovu ya serikali katika jambo hili. Nia yenyewe ni ukweli kwamba serikali ilikuwa inatafuta namna ya kuficha aibu ya wanafunzi wa kidato cha nne kuendelea kufeli katika mitihani ya mwisho. Kufikia mwaka 2012 zaidi ya asilimia 60 ya watahiniwa walifeli mitihani ya kidato cha nne. Kilio cha umma kilikuwa kikubwa.

Kwa kutambua kwamba ilikuwa haina muujiza wa kurekebisha hili, huku tukielekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 na kwa kutaka kuepuka kuadhibiwa na wananchi katika sanduku la kura, serikali ikaibuka na uamuzi wa kubadili mfumo wa kupanga madaraja. Ndiyo ikaja na huu mfumo wa GPA. Na kwa kweli mara baada ya kubadili mfumo wa kufaulu, ghafla kiwango cha kufaulu kikapanda katika mitihani ya mwaka 2013 na 2014 na serikali kupitia kwa Waziri Kawambwa ikaanza kujivunia mafanikio katika elimu. Wenye akili tulicheka vicheko vya kubeza!

Kwa hiyo uamuzi wa Profesa Joyce Ndalichako (WEST) wa kurudi katika mfumo wa zamani wa Division ni wa kupongezwa kwa kiasi fulani kwa upande mmoja, lakini pia ni uamuzi unaouudhi kwa upande mwingine, kama nitakavyoeleza hapa chini.

Kimsingi mfumo wa GPA sio mbaya kama mfumo. Nchi nyingi duniani zinatumia mfumo huu wa GPA. Tatizo la kwetu ni kwamba tulishusha viwango vya kufaulu. Hili ndilo tatizo la msingi, lakini sio mfumo wenyewe wa GPA. Naamini Prof. Ndalichako analijua vizuri jambo hili kwa kuwa yeye ni mtaalamu mahiri wa upimaji katika elimu (educational assessment) na uzoefu wa miaka takribani nane ya kuendesha Baraza letu la mitihani.

Uamuzi wa Profesa Ndalichako unaudhi kwa sababu unatukumbusha machungu ya Ndugu Mungai aliyebadili mitaala kibabe bila sababu za msingi za kitafiti na kisayansi, wala kushirikisha wadau wa elimu.

Leo mwalimu wangu Prof. Ndalichako amebadili mfumu huu bila mjadala wowote mpana kitaifa. Hakuna taarifa ya kitafiti. Hakuna uchambuzi yakinifu. Hakuna Kamati ya Bunge iilyokaa na kujadili. Hatujui waziri mwingine atakayekuja miaka miwili, mitatu, mitano au kumi ijayo atakuja na nini. Hili ni jambo linalotisha katika nchi inayofanya bidii ya kujenga demokrasia na mfumo wa utawala bora.

Hata kama uamuzi ni mzuri kiasi gani lakini mfumo wa kufanya maamuzi unaacha ukakasi mkubwa mno. Kwa mtindo wetu wa kufanya maamuzi tunakuwa nchi isiyotabirika wala kuaminika. Tutakuwa na maswali ya kujibu kila siku tunapohusiana na wenzetu katika mataifa mengine.

Miaka miwili iliyopita tumekuwa na kazi ya kuwaeleza wenzetu katika nchi nyingine kwamba tulibadili mfumo wetu wa madaraja ya kufaulu na sasa tunatumia GPA. Sasa siku chache zijazo tutaanza tena kuwaambia wenzetu kwamba ooh samahanini tumebadili tena na sasa tunarudi kule kwa zamani. Ebo!

Tusikubali kuzoea mambo makubwa kama haya yafanywe na mtu mmoja mwenye dhamana au serikali peke yake. Mambo haya yaanze na uchambuzi wa kisayansi, yafuatiwe na mjadala wa kitaifa na maamuzi ya mwisho yafanywe na Bunge au Kamati husika ya Bunge baada ya serikali kuyawasilisha na kushawishi.

Ni sahihi kabisa kwa waziri kuwa na mawazo na mapendekezo yake ya kisera. Lakini si sahihi waziri peke yake kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi makubwa ya kutuathiri na kuathiri nchi leo na kesho.

Kazi kubwa ya waziri iwe ni kuibua sera na kushawishi ubora wa sera husika lakini uamuzi wake lazima ufuate mkondo mpana wa kitaifa ili hatimaye uamuzi huo tuweze kuumbatia wote kama taifa bila ukakasi.

Ifike mahala tuimarishe nguvu za kitaasisi na kimfumo katika maamuzi ya kisera badala ya kutegemea nguvu za mwanasiasa mmoja mmoja mwenye madaraka".
 
Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
 
Profesa hajakosea kumkosoa mama Ndalichako, nadhani anakubaliana naye, sasa kama vipi wananchi waulizwe kuwa wanataka mgumo upi?
Ila thuu wa division wakati unaendelea ndio wananchi na wadau mbali mbali waulizwe..
 
Profesa huyu ana matatizo sana. Basi na atueleze ni lini akawashirikisha wadau kupanga mfumo wa acreditation huko chuo kikuu.
 
Tafiti ya nini kama ile iliyotenguliwa haikuja na tafiti mujarabu si unarudi kule ulikokuwa mpaka ije tafiti nyingine ya kubadilisha hii ya DIVISHENI.

Waliulizwa siku ile mbele ya press na umma wakawa wanajiumauma tu.
 
Professa Mkumbo usifate mkumbo,hakuna kipya hapo kilichofanywa.....lazima turudi tulipojikwaa hapo sasa ndo wadau washirikishwa na si tulipoangukia....ulitaka muitwe kwenye vikao Ngurdoto mkale Pizza kwa hili la restoration....Hapa alipoparudisha Prof.Ndalichako ndo pakuanzia c pale pa Dr.Kawambwa ambako tulianguka.
 
[QUOTE=" The issue supposed to be submitted to public debate in order to come with a good and suitable solution to the extent that one can defend the decision with reasonable arguments, hii ingejenga msingi imara na kwamba yeyote ajaye na kutaka kuover rule atapaswa ajipange kwa sababu hasa za kwanini anataka kubadili mfumo!
.[/QUOTE]
Acha kuleta usomi katika kila kitu. You are too bookish Dr Kitila, the public is not proficient enough in the art of curricula development and examinations. Prof, Ndalichako is a professor of education proficient in curricula development and examinations. Hence, when she says or decides, that's it.
 
Katika hali halisi huwezi kupanga au kuamua jambo lolote lile duniani na likakosa WAKOSOAJI; Kitila Mkumbo katumia vyema haki yake ya msingi kukosoa na nina muunga mkono kwa uamuzi wake but sio mawazo yake. Ndalichako ameifanya hi kitu kidiplomasia kweli, mbele ya kamera za TV na magazeti, mama huyu aliwaambia Baraza la Mitihani wampe sababu za Kisayansi za kwanini walibadiri mfumo wa division to GPA, tena aliwapa muda wa wiki 1 kama sikuosei.

Kihalisia kama wale jamaa walikua na sababu za msingi kuubadiri mfumo wa zamani to mfumo mpya kwangu mimi naona hata hiyo wiki 1 ilikua kubwa sana, wangeweza kutetea uamuzi wao hata pale pale, kwasababu yalikua maamuzi ya kisiasa ya kupanua GOLI (kama ambavyo prof Kitila ulivyosema mwenyewe) ili hata wasio na uwezo waonekane kua wamefauru.

Tulitaka profesa Joyce aitishe mjadara wa kitaifa ju ya jambo hili? Kitila you must be joking brother; watu wanaosimamia elimu (NECTA) wameshindwa kutetea uamuzi wao then nani mwingine angeweza kujenga hoja hapo? Sana sana tunachoweza kukisema kama wadau wa elimu (mimi na wewe) ni kuongeza limits za division kwamfano labda A ianze 100 hadi wapi/ngapi.
 
yeye prof kitila mkumbo amefanya utafiti gani hadi kuandika hiyo article yake au anatokwa povu tu manake sioni data zozote ku sapport alichoandika
 
Kwahiyo ishu hapa ni kwamba hujushirikishwa kwenye maamuzi ila sio maamuzi yenyewe?
 
Back
Top Bottom